Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha miaka minne imepata mafanikio makubwa katika maeneo mbalimbali.
Amesema mafanikio haya yanatokana na azma ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutaka kuujenga Utumishi wa Umma kuwa wenye tija katika maendeleo ya taifa.
Mhe. Simbachawene ameyasema hayo leo tarehe 17 Aprili, 2025 wakati akizungumza na vyombo vya habari kuelezea mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita katika Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO Jijini Dodoma.
Ameyataja miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana kuwa ni
pamoja na
kusimamia
Mikataba ya Utendaji Kazi Serikalini ambapo Serikali ilijenga mfumo
wa Usimamizi wa Utendaji Kazi katika Utumishi wa Umma (e-UTENDAJI -
PEPMIS/PIPMIS) unaotumika kusimamia utendaji kazi wa watumishi wa umma na
taasisi za umma ili kuwezesha kubaini kiwango cha utendaji kazi na uwajibikaji
wa viongozi na watumishi wa umma.
Kusimamia Mipango na
Uendelezaji Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma baada ya kuona kuna
tatizo la upungufu wa watumishi katika maeneo mengi, ilitafuta namna bora ya
kuondoa changamoto hiyo kwa kujenga Mfumo wa Tathmini ya Mahitaji ya
Rasilimaliwatu (HR-Assessment).
“Mfumo huu wa Tathmini
ya Mahitaji ya Rasilimaliwatu ni msaada mkubwa kwani unabainisha idadi ya
watumishi walioko katika kila kituo cha kazi na upungufu au ziada iliyopo ili
kuwa na idadi ya watumishi sahihi katika sehemu sahihi za utekelezaji wa
majukumu yao.” ameeleza Mhe. Simbachawene
Katika eneo la Usimamizi wa
Maslahi na Stahiki za Watumishi wa Umma Mhe, Simbachawene amesema, Rais Mhe. Dkt. Samia
Suluhu Hassan ameyaangalia maslahi ya watumishi wa umma kwa jicho la pekee
ikiwemo kupunguza kodi ya mapato
(PAYE) kutoka 9% hadi asilimia 8%, kufuta tozo (retention fee) ya 6% iliyokuwa
ikitozwa kutoka katika mishahara ya watumishi wa Umma walionufaika na Mikopo ya
Elimu ya Juu, kulipa malimbikizo ya mshahara, kupandisha
vyeo, kubadilisha kada pamoja na kuundwa
kwa Mfumo wa Huduma Mtandao kwa Watumishi (Watumishi Portal) unaowawezesha
Watumishi wa Umma kupata huduma mbalimbali za kiutumishi moja kwa moja bila
kulazimika kwenda kwenye Ofisi za Waajiri wao.
Mhe.
Simbachawene amefafanua kuwa hadi kufikia tarehe 31 Machi, 2025 madai ya
malimbikizo ya mishahara ya watumishi 148,137 yenye jumla ya Sh. 248,528,998,254.79
yalipokelewa na kushughulikiwa. Aidha, katika kipindi hicho, madai ya
malimbikizo ya mishahara ya watumishi wastaafu 10,022 kutoka kwa waajiri yenye
jumla ya Sh. 33,290,109,780.75 yamepokelewa na kushughulikiwa na wahusika
wamelipwa kupitia kwa waajiri wao.
Ameongeza kuwa mpaka kufikia tarehe 31 Machi, 2025 Jumla ya watumishi wa umma 610,733 wamepandishwa vyeo, 42,515 wamebadilishwa kada, 3,208 wamepata uteuzi, 157,512 wamesafishiwa taarifa zao za kiutumishi, 10,725 wamebadilishiwa vyeo, 3,877 wamerekebishiwa majina, 9,269 wamefanyiwa mabadiliko ya mshahara binafsi, 2,558 wamerejeshwa kwenye utumishi wa umma na 133,317 wameajiriwa katika Taasisi mbalimbali za umma. Aidha, katika kipindi hicho, Jumla ya nafasi za ajira 155,008 zimetolewa na jumla vibali vya ajira mbadala 41,673 vimetolewa ili kujaza nafasi zilizobaki wazi kwa sababu mbalimbali.
Mhe. Simbachawene amesema, Mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita kwa kipindi cha miaka minne yameonekana pia kwa upande wa Mfuko wa maendeleo ya Jamii (TASAF) kwani, Mpango wa Miradi ya Kutoa Ajira za Muda kwa Walengwa kufikia Desemba, 2024, jumla ya miradi 27,863 ya kutoa ajira za muda kwa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini imetekelezwa.
Kwa upande wa TAKUKURU, Mhe. Simbachawene amesema, TAKUKURU imetekeleza majukumu yake kwa ufanisi kwa kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa nchini ambapo Programu ya TAKUKURU Rafiki ilizinduliwa ili kuleta mafanikio makubwa na kero nyingi zilizoibuliwa zilitatuliwa ikiwamo sekta za afya, elimu, maji, nishati, mawasiliano, maendeleo ya jamii, mazingira, ujenzi, ardhi, kilimo, ufugaji, usafirishaji, usalama na haku jinai, hivyo kuzuia vitendo vya rushwa na kuboresha huduma zinazotolewa kwa umma.
Waziri Simbachawene ameongeza kuwa, katika kuhakikisha Tanzania inakuwa ya kidijitali, Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) imetekeleza agizo la Mhe. Rais kwa kujenga na kusanifu mfumo wa pamoja wa Ubadilishanaji Taarifa Serikalini (Government Enterprise Service Bus-GovESB) ili kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi sambamba na kupunguza mianya ya rushwa, kuondoa urasimu na kurahisisha utekelezaji wa majukumu ya kila siku ya Serikali,
Aidha, katika kutengeneza Mfumo shirikishi utakaowezesha Mifumo ya Taasisi kuwasiliana na kubadilishana taarifa, mifumo 202 ya taasisi za umma 179 imeunganishwa na inabadilishana taarifa ikiwemo Taasisi za Sekta ya Haki Jinai zinazojumuisha Mahakama, TAKUKURU, Polisi na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.
Mhe. Simbachawene amempongeza na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa maelekezo na kusimamia kikamalifu
kuhakikisha yametekelezwa kwa ufanisi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza wakati wa Mkutano
wake na Waandishi wa Habari kuhusu Mafanikio ya Miaka 4 ya Serikali ya
Awamu ya Sita kwenye eneo la Utumishi wa
Umma na Utawala Bora leo tarehe 17, Aprili 2025 jijini
Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene (wa kwanza kushoto)
akimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Maelezo, Bw. Rodney Thadeus (hayupo
pichani) wakati akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri huyo
kuzungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Mafanikio ya
Miaka 4 ya Serikali ya Awamu ya
Sita kwenye eneo la
Utumishi wa Umma na Utawala Bora leo tarehe 17, Aprili 2025 jijini
Dodoma. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa Ofisi yake Bw. Juma Mkomi.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Shedrack Mziray (wa
kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Fedha na Utawala-TASAF, Bw. Godwin Mkisi
(katikati) na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya
Rais-UTUMISHI, Bi. Mary Mwakapenda (wa kwanza kulia) wakifuatilia hotuba ya Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
George Simbachawene wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Mafanikio ya
Miaka 4 ya Serikali ya Awamu ya
Sita kwenye eneo la
Utumishi wa Umma na Utawala Bora leo tarehe 17, Aprili 2025 jijini
Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akifafanua jambo wakati wa
Mkutano wake na Waandishi wa Habari kuhusu Mafanikio ya Miaka 4 ya Serikali ya Awamu ya Sita kwenye
eneo la Utumishi wa Umma na
Utawala Bora leo tarehe 17, Aprili 2025 jijini Dodoma.



No comments:
Post a Comment