Na. Lusungu Helela - Dodoma.
Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi amewataka Wajumbe wa Kamati za Ushauri za Ajira za Raia wa Kigeni katika Utumishi wa Umma kuhakikisha wanalinda taswira ya nchi kimataifa kwa kuyafanyia kazi na kuyawasilisha maombi hayo ya ajira za raia wa kigeni kwa wakati katika Ofisi ya Rais, UTUMISHI na Utawala Bora.
Amesema Kamati hizo kwa uzembe wake zimekuwa zikiharibu mahusiano ya kidiplomasia ya kimataifa kwa kufanya kazi kwa mazoea katika kushughulikia suala hilo nyeti la ajira za raia wa kigeni kwa kuwasilisha maombi hayo yakiwa yamechelewa na hayana viambatisho muhimu, hali inayochangia kuipa wakati mgumu Ofisi ya Rais, UTUMISHI katika kuyafanyia kazi.
Bw. Daudi ametoa kauli hiyo leo wakati akifungua mafunzo elekezi kwa Wajumbe wa Kamati hizo kwa ngazi ya Wizara yanayofanyika kwa muda wa siku mbili katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.
"Tumekuwa tukipokea kila aina ya lawama kuwa sisi Ofisi ya Rais, UTUMISHI na Utawala Bora ndio tunakwamisha mchakato ambapo wakati mwingine unakuta hata maombi hayo bado hayajawasilisha kwetu, hili jambo sio zuri badilikeni" amesisitiza Kaimu Katibu Mkuu Daudi.
Amesema Wajumbe wa Kamati hizo ambao hawatimizi jukumu hilo nyeti walilopewa wanapaswa kujisikia vibaya huku akiwataka kuacha tabia hiyo ya kufanya kazi kwa mazoea.
Amefafanua kuwa maombi hayo ya ajira yamekuwa hayawasilishwi kwa wakati na wakati mwingine yamekuwa yakiwaletwa Ofisi ya Rais, Utumishi ikiwa tayari raia hao wa kigeni wakiwa wameshawasili nchini, jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa nchi na ni kinyume cha sheria.
Awali, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu, Bi. Sophia Abdallah amesema wamelazimika kufanya mafunzo hayo kwa lengo la kuwakumbusha wajumbe hao juu ya wajibu wao wa kuyafanyia kazi na kuyawasilisha kwa wakati maombi hayo yakiwa na nyaraka zote zinazotakiwa ili kuondoa mkwamo huo.
Ameongoza kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwa wajumbe hao ikizingatiwa kuwa kwa sasa Tanzania haina uhaba wa wataalamu kama ilivyokuwa hapo awali, hivyo mafunzo hayo yanatumika kuwakumbusha kuwa makini katika uchambuzi wa maombi watakayokuwa wakiyawasilisha kwa kuangalia uhaba halisi wa ajira hizo za kigeni
Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi wakati akifungua mafunzo elekezi kwa Wajumbe wa Kamati za Ushauri za Ajira za Raia wa Kigeni katika Utumishi wa Umma kwa ngazi ya Wizara yanayofanyika kwa muda wa siku mbili katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu, Bi. Sophia Abdallah akizungumza kabla ya kumkaribisha Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi kwa ajili ya mafunzo elekezi kwa Wajumbe wa Kamati za Ushauri za Ajira za Raia wa Kigeni katika Utumishi wa Umma kwa ngazi ya Wizara yanayofanyika kwa muda wa siku mbili katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma
Mwezeshaji wa Mafunzo wa elekezi kwa Wajumbe wa Kamati za Ushauri za Ajira za Raia wa Kigeni katika Utumishi wa Umma ambaye pia ni Afisa Utumishi Mwandamizi kutoka Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu, Bw. Baraka Kango'ma akitoa ufafanuzi wa baadhi ya maswali yaliyoulizwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo kwenye mafunzo elekezi yanayofanyika kwa muda wa siku mbili katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambayo yamefunguliwa leo na Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi Mwezeshaji wa Mafunzo wa elekezi kwa Wajumbe wa Kamati za Ushauri za Ajira za Raia wa Kigeni katika Utumishi wa Umma ambaye pia ni Afisa Utumishi kutoka Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu, Bi. Geva Mbugi akitoa ufafanuzi wa baadhi ya maswali yaliyoulizwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo kwenye mafunzo elekezi yanayofanyika kwa muda wa siku mbili katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambayo yamefunguliwa leo na Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi
wezeshaji wa Mafunzo wa elekezi kwa Wajumbe wa Kamati za Ushauri za Ajira za Raia wa Kigeni katika Utumishi wa Umma ambaye pia ni Afisa Utumishi kutoka Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu, Bi. Sima Kamuzora akitoa ufafanuzi wa baadhi ya maswali yaliyoulizwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo kwenye mafunzo elekezi yanayofanyika kwa muda wa siku mbili katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambayo yamefunguliwa leo na Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati za Ushauri za Ajira za Raia wa Kigeni katika Utumishi wa Umma wa ngazi ya Wizara wakifuatilia mafunzo elekezi yanayofanyika kwa muda wa siku mbili katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambayo yamefunguliwa leo Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi.
Mwezeshaji wa Mafunzo wa elekezi kwa Wajumbe wa Kamati za Ushauri za Ajira za Raia wa Kigeni katika Utumishi wa Umma ambaye pia ni Afisa Utumishi Mwandamizi kutoka Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu, Bw. Emmanuel Luvanda akitoa ufafanuzi wa baadhi ya maswali yaliyoulizwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo kwenye mafunzo elekezi yanayofanyika kwa muda wa siku mbili katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambayo yamefunguliwa leo na Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi










No comments:
Post a Comment