Na Lusungu Helela-Dodoma
Serikali imesema kwamba katika Mwaka wa Fedha 2022/2023 imewapandisha vyeo watumishi 180,000 wakiwemo watumishi walioathirika na mwongozo wa upandaji madaraja wa miaka minne.
Mhe. Sangu amesema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Janejelly Ntate aliyetaka kujua Serikali imejipangaje kukwamua watumishi walioathiriwa na mwongozo wa upandaji madaraja wa miaka minne.
Aidha, katika utekelezaji wa Ikama na Bajeti ya Mwaka 2023/2024, Serikali imewapandisha vyeo watumishi zaidi ya 232,530 wakiwemo walioathirika na zoezi hilo, uhakiki wa vyeti feki na watumishi hewa
No comments:
Post a Comment