Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Cosmas Ngangaji (aliyesimama) akizungumza na
Maafisa Bajeti wa Ofisi hiyo (hawapo pichani) wakati akifungua kikao kazi cha
kuwajengea uwezo maafisa hao mkoani Manyara. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa
Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathimini wa Ofisi hiyo Bw. Patrick Allute.
Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Cosmas Ngangaji (aliyesimama) akifafanua
jambo wakati akiwasilisha mada kuhusu namna ya kuandaa mpango na bajeti wakati
wa kikao kazi cha kuwajengea uwezo Maafisa Bajeti wa Ofisi hiyo kilichofanyika
mkoani Manyara.
Mratibu wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo Maafisa Bajeti
wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Rashid
Shedafa (aliyesimama) akielezea malengo ya kikao kazi cha kuwajengea uwezo
maafisa hao kilichofanyika mkoani Manyara.
Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Cosmas Ngangaji (katikati) akiwa katika
picha ya pamoja na Maafisa Bajeti wa Ofisi hiyo baada ya kufungua kikao kazi
cha maafisa hao kilichofanyika mkoani Manyara.
No comments:
Post a Comment