Na Lusungu Helela - SINGIDA
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene amemshukia aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Freeman Mbowe kuhusiana na hoja yake aliyoitoa ya kubeza juhudi ya Serikali ya kutaka kuondoa umaskini wa watu kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa kuwagawia fedha.
Mhe.
Simbachawene ameyasema hayo leo mara baada ya
kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa kupitia TASAF
Mkoani Singida ambapo amesema TASAF ni mpango mmojawapo wa uwezeshaji
wananchi kiuchumi lakini Serikali ina mipango lukuki.
"Jana (juzi)
nilikuwa nasikiliza ule Mkutano wa Uchaguzi wa Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) nilimsikia Mhe. Mbowe wakati akitoa taarifa ya Chama
hicho kuwa "Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inataka
kuondoa umaskini wa watu kupitia TASAF kwa kuwagawia fedha"
"Ni kweli Serikali ya
CCM inataka kuondoa umaskini wa watu wake hasa wale wasiojiweza kabisa kwa
kuwasaidia kifedha lakini pia Serikali hii inatumia mfuko wa TASAF kuondoa
changamoto zinazogusa maisha ya wananchi moja kwa moja kwa kwenda kurekebisha
miundombinu pamoja na vikwazo katika maisha yao ikiwemo ujenzi wa vivuko
ili waweze kwenda mashambani kwa urahisi hususan wakati wa msimu wa
mvua" amesisitiza Mhe. Simbachawene
Pia, Mhe. Simbachawene
amesema Serikali kupitia TASAF imekuwa ikijenga vituo vya afya mahali
ambako kuna zahanati zisizokidhi mahitaji ya wananchi ili kuhakikisha wananchi
wanapata huduma bora za afya lengo likiwa ni kupambana na umaskini
"Nataka nimwambie Kaka yangu
Mbowe kwamba TASAF ni mpango mmojawapo wa kuwezesha wananchi wetu
kiuchumi lakini Serikali yetu ina mipango mingi sana na tunayo Sera ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi"
amesisitiza Mhe. Simbachawene
Amesema Serikali ina Mfuko wa
uwezeshaji wa wananchi kiuchumi ambapo kuna njia mbalimbali za kuwagusa
kiuchumi ikiwemo vijana na makundi mbalimbali lengo likiwa ni kupambana
na umasikini na kuwapa ahueni katika hali zao za maisha
Ameongeza kuwa "Tuna mpango wa
kuwawezesha kiuchumi kwa kutoa mikopo kwa Vijana, Wanawake na Watu wenye
Ulemavu ambapo asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri hupelekwa kwa
ajili ya kukopesha makundi hayo.
Mbali na mipango hiyo Mhe. Simbachawene
ameitaja mipango mingine ya uwezeshaji wananchi kiuchumi kuwa ni utoaji ruzuku kwenye pembejeo za
kilimo, utoaji wa mikopo ya elimu ya juu, ujenzi wa Shule za Sekondari
kila Kata pamoja na Shule za Msingi kila Kijiji, utoaji wa mikopo ya
Elimu ya juu pamoja na matibabu bure kwa wazee
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na wanufaika wa TASAF katika Kijiji cha Kinyakaya kilichopo katika Mkoa wa Singida
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene akikagua Mradi wa upandaji miti kupitia TASAF uliotekelezwa katika Kijiji cha Kinyakaya kilichopo katika Mkoa wa Singida
Baadhi ya Wanufaika wa TASAF
wakimsikiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene wakati akizungumza nao katika Kijiji cha Kinyakaya
kilichopo katika Mkoa wa Singida
Mkuu wa Wilaya ya Singida
Mhe. Godwin Gondwe akizungumza na walengwa wa TASAF katika
Kijiji cha Kinyakaya kabla ya
kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kuzungumza na walengwa hao Mkoani
Singida
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene akiwa
ameongoza na Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe. Godwin Gondwe mara baada ya kuwasili
Mkoani Singida kwa ajili ya ziara ya kikazi
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George
Simbachawene akiagana na wanufaika wa mpango wa kuondoa umasikini mara baada ya
kuzungumza nao katika Kijiji cha Kinyakaya kilichopo katika Mkoa wa Singida
No comments:
Post a Comment