Na.Lusungu Helela — DODOMA
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imeipongeza Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa kutekeleza majukumu yake kikamilifu na kuhakikisha michakato ya ajira inafanyika kwa ufanisi na kwa uwazi wa hali ya juu.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo , Mhe. Dkt.
Joseph Mhagama ametoa pongezi hizo leo jijini Dodoma kwa niaba ya Kamati yake
wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kilicholenga kupokea
na kujadili taarifa ya utendaji kazi ya mwezi Septemba 2024 hadi Januari 2025.
Mhe. Dkt. Mhagama mesema kitendo cha
usaili kufanyika katika ngazi za mikoa badala ya kuwalazimu waombaji kazi wote
kufika jijini Dodoma kumeleta ahueni
kubwa kwa waombaji kazi hao hususani wale waliotoka kwenye familia maskini.
Hapo awali wazazi walilazimika kuuza ardhi au
ngombe ili kijana wao aweze kusafiri kuja jijini Dodoma kwa ajili ya kufanya
usaili ila ubunifu wa kufanya usaili kimkoa umerahisishia. Amesema Mhe. Dkt. Mhagama amesema
Amesisitiza kuwa utaratibu huo umeondoa usumbufu pamoja na
kumfanya Muombaji kazi kutokutumia gharama ya usafiri kwa ajili ya
kufika jijini Dodoma kufanya usaili
Akizungumzia
matumizi ya mfumo wa Ajira Portal kwa waombaji kazi Mhe.Dkt. Mhagama amesema mfumo juo umeondoa dhana ya upendeleo
wa kupata ajira katika Utumishi wa Umma na kuchagiza ushindani miongoni mwa
waombaji kwani hutoi fursa ya kuonana ana kwa ana na wahusika
Nimekuwa nikipokea simu nyingi kutoka
kwa Watoto wa familia masikini wa kutoka
vijijini wakiwa wamepata ajira serikalini pasipo kumjua yeyote aliyepo
serikalini amesisitiza Mhe.Dkt. Mhagama
Kwa Upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene
amesema ajira katika Utumishi wa Umma zinapatikana kwa ushindani kutokana na
idadi kubwa ya wasomi iliyopo lakini nafasi ni chache
Ametumia fursa hiyo kuwaomba Wajumbe wa
Kamati hiyo kuwa Mabalozi wa Sekretariet ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa
kuwaeleza wananchi kuwa ajira katika Utumishi wa Umma hazihitaji kumjua yeyote
na cha msingi ni kufuata taratibu zilizowekwa na Sekretarieti hiyo wakati wa kuomba kazi.
Mwenyekiti wa Kamati ya ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria , Mhe. Dkt. Joseph Mhagama akizungumza na Wajumbe mara baada ya Naibu Waziri Mhe. Deus Sangu kuwasilisha taarifa ya utendaji kazi wa Ofisi ya Rais, UTUMISHI na Utawala Bora kwa niaba ya Waziri Mhe. George Simbachawene
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene
akijibu hoja zilizotolewa na Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya ya Kudumu ya Bunge
ya Utawala, Katiba na Sheria mara baada ya Wajumbe hao kupokea na kujadili
taarifa ya utendaji kazi wa Ofisi ya Rais, UTUMISHI na Utawala
Bora
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya ya
Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakimsikiliza
Naibu Waziri Mhe. Deus Sangu mara baada ya kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi wa
Ofisi ya Rais, UTUMISHI na Utawala Bora kwa niaba ya Waziri Mhe. George
Simbachawene
Naibu Waziri , Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi wa
Ofisi ya Rais, UTUMISHI na Utawala Bora kwa niaba ya Waziri Mhe. George
Simbachawene mbele ya Wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria
Baadhi ya Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwa katika kikao kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi ya Ofisi hiyo kilichofanyika leo Jijini Dodoma
No comments:
Post a Comment