Wednesday, July 31, 2024

MHE. SIMBACHAWENE AITAKA OFISI YAKE KUTOA USHIRIKIANO WA KIUTENDAJI KWA NAIBU WAZIRI SANGU ILI KUBORESHA UTUMISHI WA UMMA NCHINI

 Na. Veronica Mwafisi-Dodoma

Tarehe 31 Julai, 2024

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ametoa wito kwa watumishi  pamoja na wakurugenzi wa Idara na Vitengo wa ofisi yake kutoa ushirikiano wa kiutendaji kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu aliyeteuliwa na kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kutumikia ofisi hiyo.

Mhe. Simbachawene ametoa wito huo leo jijini Dodoma, wakati wa hafla fupi ya kumpokea kiongozi huyo.

Mhe. Simbachawene amesema, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, imepata kiongozi mwingine kwa ajili ya kuongeza nguvu ya kiutendaji, hivyo ametoa rai kwa menejimenti ya ofisi hiyo kumpa ushirikiano wa kutosha ili aweze kutekeleza majukumu yake kikamilifu ili kufikia maono ya Rais wa Awamu ya Sita ya kuuboresha Utumishi wa Umma nchini.

“Tumepata kiongozi mwingine kwa ajili ya kuongeza nguvu ya kiutendaji, niwatake mtoe ushirikiano kwa Naibu Waziri Sangu ili kumuwezesha kutekeleza majukumu yake kikamilifu na kutoa mchango katika Utumishi wa Umma kama ilivyokusudiwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan” amesema Mhe. Simbachawene.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa ofisi hiyo Mhe. Deus Sangu ameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa watumishi wote na kuongeza kuwa, atahakikisha anasimamia haki katika kufanya kazi.

Mhe. Sangu ameongeza kuwa, ataendeleza pale alipoishia mtangulizi wake katika kuujenga utumishi wa umma wenye uadilifu na unaowajibika kwa wananchi katika kutoa huduma bora ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa malengo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kuujenga utumishi wa umma unaowajibika kwa wananchi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (wa pili kulia) akimkaribisha Naibu Waziri wa ofisi yake, Mhe. Deus Sangu (wa kwanza kulia) mara baada ya kuripoti rasmi katika ofisi hizo zilizopo Mtumba jijini Dodoma baada ya kuteuliwa na kuapishwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa ofisi hiyo Bw. Juma Mkomi. 

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu akipokea maua ya ukaribisho mara baada ya kuripoti rasmi katika ofisi ya Rais-UTUMISHI iliyopo Mtumba jijini Dodoma baada ya kuteuliwa na kuapishwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Naibu Waziri wa ofisi hiyo.


Sehemu ya watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakisubiri kumpokea Naibu Waziri wa ofisi hiyo Mhe. Deus Sangu (hayupo pichani) kabla ya kuwasili katika ofisi hiyo zilizopo Mtumba jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (wa pili kulia) akifurahia jambo na Naibu Waziri wa ofisi yake Mhe. Deus Sangu (wa kwanza kulia) pamopja na Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Juma Mkomi na Naibu Katibu Mkuu Bw. Xavier Daudi mara baada ya baada ya Naibu Waziri Sangu kuripoti rasmi katika ofisi hizo zilizopo Mtumba jijini Dodoma baada ya kuteuliwa na kuapishwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Cosmas Ngangaji mara baada ya Naibu Waziri huyo kuripoti rasmi katika ofisi hizo zilizopo Mtumba jijini Dodoma. 

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu akisalimiana na sehemu ya watumishi wa ofisi hiyo mara baada ya kuripoti rasmi katika ofisi hizo zilizopo Mtumba jijini Dodoma baada ya kuteuliwa na kuapishwa na Mhe. Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Wengine ni viongozi wa ofisi hiyo.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu akizungumza jambo na mmoja wa watumishi wa ofisi hiyo mara baada ya kuripoti rasmi katika ofisi hizo zilizopo Mtumba jijini Dodoma baada ya kuteuliwa na kuapishwa na Mhe. Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Wa kwanza kushoto ni Waziri wa ofisi hiyo Mhe. George Simbachawene.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (wa tatu kushoto) akimsikiliza Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi (wa pili kushoto) kabla ya kuwasili Naibu Waziri wa ofisi hiyo Mhe. Deus Sangu aliyeteuliwa na kuapishwa kuwa Naibu Waziri wa ofisi hiyo. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Musa Magufuli.












No comments:

Post a Comment