Monday, July 29, 2024

MHE. SIMBACHAWENE AKUTANA NA WENZA WA VIONGOZI WA KITAIFA

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene leo kwa nyakati tofauti amewatembelea na kufanya mazungumzo mama Anna Mkapa na Janeth Magufuli nyumbani kwao Osterbay Jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo yake na wenza wa viongozi hao, Mhe. Simbachawene ameahidi kuwaelekeza watendaji katika ofisi yake, kushughulikia changamoto zinazojitokeza na kuwafanya wenza wa viongozi hao kuendelee kuishi kwa amani na usalama.

Aidha, Mama Mkapa amemshukuru Mhe. Simbachawene kwa kupata nafasi ya kumtembelea, kumjulia hali na kusikiliza changamoto alizonazo na kuzitafutia ufumbuzi.

Vilevile Mama Janeth Magufuli amempongeza Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuijali familia yake na kuwatunza wakati wote bila kuchoka na amemuombea kwa Mungu aendelee kuiongoza vyema Tanzania.







 

 

No comments:

Post a Comment