Monday, July 29, 2024

MHE. SIMBACHAWENE ATETA NA RAIS MWINYI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene leo amemtembelea na kufanya mazungumzo na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi nyumbani kwake Osterbay Jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo Mhe. Simbachawene amemueleza Mhe. Dkt. Mwinyi kuwa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amemuelekeza kumfikishia salaam kwa familia ya Hayati Ali Hassan Mwinyi na kuahidi kuendelea kuwa pamoja na familia hiyo kwa kuwa ni wajibu wa Ofisi yake kutunza wenza wa Viongozi wa Kitaifa na yeye yuko tayari kuendelea kutekeleza wajibu huo.

Mhe. Simbacahwene aliongeza kuwa anafanya ziara ya kuwajulia hali Wenza wa Viongozi hao ili kufahamu changamoto zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi.

Aidha, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameshukuru kwa ujio huo na kupongeza utaratibu uliopo wa kuwatembelea wanafamilia na kuwapa faraja.

 







No comments:

Post a Comment