Na. Veronica Mwafisi-Manyara
Tarehe 23 Julai, 2024
Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw. Cyprus
Kapinga amezitaka Wizara na Taasisi za Umma kufanya uhakiki wa takwimu za
watumishi wa umma wenye VVU, Ukimwi na Magonjwa Sugu
Yasiyoambukiza (MSY) ili kulinda afya za watumishi hao.
Bw. Kapinga ametoa wito huo leo wakati akifungua kikao
kazi cha Robo ya Nne ya Mwaka 2023/2024 kilichoshirikisha
Kamati ya Kifaifa, Waratibu wa Wizara wa Kudhibiti VVU, Ukimwi na Magonjwa Yasiyoambukiza (MSY)
pamoja na Wajumbe, Wenyeviti, Makatibu wa Mkoa wa Manyara wanaosimamia
magonjwa hayo.
“Tunatakiwa kuwa na takwimu sahihi ya watumishi hao
ili kurahisisha zoezi la kupanga bajeti ya kuwahudumia na kuimarisha afya ya
akili na kudhibiti msongo wa mawazo. Watumishi hao ni sehemu ya nguvu kazi ya
Taifa inayohudumia wananchi” alisisitiza Bw. Kapinga.
Aidha, Bw. Kapinga ametoa rai kwa Maafisa Masuuli wote
katika taasisi za umma kuunda na kuimarisha Kamati za VVU, Ukimwi na Magonjwa
Sugu Yasiyoambukiza (MSY) zilizopo kwa kutoa nafasi kwa wanakamati hao kupata
mafunzo na elimu itakayowafanya wawe na uwezo wa kushawishi watumishi kupima
afya na hivyo kuwa na takwimu sahihi kwa
mipango bora na endelevu.
Awali akitoa neno la utangulizi, Katibu Tawala Mkoa wa
Manyara, Bi. Maryam Muhaji aliwataka washiriki wa kikao kazi hicho kusikiliza
na kufuatilila kwa makini mada zote zitakazowasilishwa ili wapate uwezo na
ujuzi Madhubuti wa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, kupitia Idara ya Uendelezaji Sera ipo mkoani Manyara kwa lengo la
kujadili utekelezaji wa mapambano dhidi ya VVU, Ukimwi na Magonjwa
yasiyoambukiza (MSY) ili kuwalinda watumishi wa umma na kuhakikisha taifa
linaondokana na vifo vitokanavyo na magonjwa hayo ifikapo mwaka 2030.
Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Cyprus
Kapinga akizungumza na Kamati ya Kifaifa,
Waratibu wa Wizara wa Kudhibiti VVU,
Ukimwi na Magonjwa Yasiyoambukiza (MSY)
pamoja na Wajumbe, Wenyeviti, Makatibu wa mkoa wa Manyara wanaosimamia
magonjwa hayo wakati wa kikao kazi cha robo ya nne ya Mwaka 2023/2024.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Rasilimaliwatu wa Kamati ya
Kitaifa ya Kudhibiti VVU, Ukimwi na Magonjwa Sugu Yasiyoambukiza (MSY) na
Waratibu wa magonjwa hayo wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais-UTUMISHI, Bw. Cyprus Kapinga (hayupo pichani) wakati akifungua kikao kazi
cha robo ya nne ya Mwaka 2023/2024 kinachofanyika mkoani Manyara.
Katibu Tawala Mkoa wa Manyara, Bi. Maryam Muhaji
akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais-UTUMISHI, Bw. Cyprus Kapinga kufungua kikao
kazi cha robo ya nne ya Mwaka 2023/2024 cha Kamati ya
Kifaifa, Waratibu wa Wizara wa Kudhibiti VVU, Ukimwi na Magonjwa Yasiyoambukiza
(MSY) kinachofanyika mkoani Manyara.
Mkurugenzi Msaidizi Anuai za Jamii na Mratibu wa VVU, Ukimwi na Magonjwa Yasiyoambukiza, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Mwanaamani Mtoo akitoa utambulisho wa Kamati ya Kifaifa, Waratibu wa Wizara wa Kudhibiti VVU, Ukimwi na Magonjwa Yasiyoambukiza (MSY) pamoja na Wajumbe, Wenyeviti, Makatibu wa mkoa wa Manyara wanaosimamia magonjwa hayo kwenye kikao kazi kilichofanyika mkoani Manyara.
Afisa Maendeleo ya Jamii, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi.
Neema Range akiwasilisha mada kuhusu Ujumuishwaji wa Sehemu za Anuai za Jamii
wakati wa kikao kazi cha robo ya nne ya Mwaka 2023/2024
kilichoshirikisha Kamati ya Kifaifa, Waratibu wa Wizara wa Kudhibiti VVU,
Ukimwi na Magonjwa Yasiyoambukiza (MSY) pamoja na Wajumbe, Wenyeviti, Makatibu
wa mkoa wa Manyara.
Afisa Ustawi wa Jamii Mwandamizi na Mratibu wa Kitaifa
wa Kudhibiti VVU, Ukimwi na Magonjwa Sugu Yasiyoambukiza, Ofisi ya
Rais-UTUMISHI, Bi. Juliana Ntukey akiwasilisha mada kuhusu Mwongozo wa Waraka
wa kudhibiti VVU, Ukimwi na Magonjwa Sugu Yasiyoambukiza mahali pa kazi katika Utumishi
wa Umma (2014) wakati wa kikao kazi cha robo ya nne ya
Mwaka 2023/2024.
Mratibu wa VVU, Ukimwi na Magonjwa Sugu Yasiyoambukiza
(MSY), Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara, Bi. Marietha Kyomo akiwasilisha taarifa
ya Mkoa wa Manyara kuhusu hali ya utekelezaji wa Afua za VVU, Ukimwi na MSY
wakati wa kikao kazi cha robo ya nne ya Mwaka 2023/2024 kilichofanyika katika
mkoa huo.
Mratibu wa Kinga na Mwitikio wa Kitaifa dhidi ya VVU,
Ukimwi na Magonjwa Yasiyoambukiza, Dkt. Haffidh Ameir akitoa taarifa kuhusu
hali halisi ya VVU na Ukimwi Nchini wakati wa kikao kazi cha robo ya nne
ya Mwaka 2023/2024 kilichoshirikisha Kamati ya Kifaifa, Waratibu wa Wizara wa
Kudhibiti VVU, Ukimwi na Magonjwa Yasiyoambukiza (MSY) pamoja na Wajumbe,
Wenyeviti, Makatibu wa mkoa wa Manyara.
Daktari Bingwa wa Afya na Magonjwa ya Akili, Dkt.
Sadiki Mandari akiwasilisha mada kuhusu kuimarisha afya ya akili kwa Kamati ya
Kifaifa, Waratibu wa Wizara wa Kudhibiti VVU, Ukimwi na Magonjwa Yasiyoambukiza
(MSY) pamoja na Wajumbe, Wenyeviti, Makatibu wa mkoa wa Manyara wanaosimamia
magonjwa hayo wakati wa kikao kazi cha robo ya nne ya Mwaka 2023/2024
kinachofanyika mkoani Manyara.
Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Cyprus
Kapinga akiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya Waratibu wa Wizara wa
Kudhibiti VVU, Ukimwi na Magonjwa Sugu Yasiyoambukiza (MSY) wakati wa kikao
kazi cha robo ya nne ya Mwaka 2023/2024 kinachofanyika mkoani Manyara.
No comments:
Post a Comment