Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora, SACP. Ibrahim Mahumi (Wa kwanza kulia) akizungumza na Timu
ya Utekelezaji wa Mchakato wa Matumizi ya Mfumo wa Tathmini ya Utendaji Kazi wa
Watendaji wa Jeshi la Polisi katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI,
Mtumba Jijini Dodoma tarehe 11 Julai, 2024.
Kamishna wa Utawala na
Rasilimaliwatu wa Jeshi la Polisi DCP. Gabriel Semiono (Wa Pili Kushoto) akifafanua
jambo baada ya kuwasilishwa kwa taarifa fupi ya namna ya upimaji wa utendaji
kazi wa watendaji wa Jeshi la Polisi kwa sasa ili waweze kutumia Mfumo wa
Tathmini ya Utendaji Kazi (e-Utendaji). Kikao kazi kimefanyika katika Ukumbi wa
Mikutano wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Mtumba Jijini Dodoma tarehe 11 Julai, 2024.
Mkurugenzi wa Huduma za
TEHAMA Serikalini, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora, Bw. Priscus Kiwango akifafanua jambo kwa Timu ya Utekelezaji wa Mchakato
wa Matumizi ya Mfumo wa Tathmini ya Utendaji Kazi wa Watendaji wa Jeshi la
Polisi (hawapo pichani) katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI,
Mtumba Jijini Dodoma tarehe 11 Julai, 2024.
Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, SACP. Ibrahim Mahumi (Wa kwanza kulia) akifuatilia
wasilisho la namna Mfumo wa e-Utendaji kazi unavyofanya kazi wakati akiongoza
kikao kazi cha mafunzo na majadiliano ya namna ya kutumia mfumo huo. Wa Pili
Kulia ni Kamishna wa Utawala na Rasilimaliwatu wa Jeshi la Polisi DCP. Gabriel
Semiono aliyeongoza Timu ya Utekelezaji wa Mchakato wa Matumizi ya Mfumo wa
Tathmini ya Utendaji Kazi wa Watendaji wa Jeshi la Polisi katika Ukumbi wa
Mikutano wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Mtumba Jijini Dodoma tarehe 11 Julai, 2024.
No comments:
Post a Comment