Saturday, March 30, 2024
WAZIRI SIMBACHAWENE AWASISITIZA WATUMISHI WA OFISI YAKE KUTOA HUDUMA ZENYE VIWANGO KWA WANANCHI
Na Lusungu Helela-Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amewataka Watumishi wa Ofisi
yake kutoa huduma bora kwa wananchi kwa haraka na ufanisi, huku akisisitiza
ubora wa huduma hizo uendane na uzuri wa jengo jipya ambalo Ofisi hiyo imehamia
hivi karibuni.
Mhe. Simbachawene ametoa kauli hiyo jana jioni mara baada ya
Iftar iliyoandaliwa na Ofisi hiyo na kuwakutanisha Watumishi wote wa Ofisi hiyo
wakiwemo baadhi ya viongozi kutoka Taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo,
ikiwa ni hatua muhimu ya kujumuika kwa pamoja mara baada ya kuhamia
katika jengo jipya lililopo Mtaa wa Utumishi, Mji wa Serikali Mtumba
Jijini Dodoma.
Amesema anatamani kuona wananchi na watumishi wanaohudumiwa
katika jengo hilo jipya wanafurahia huduma wanazozipata kwani kitendo cha
Watumishi kuhamia katika jengo hilo jipya kwa sasa kuna utulivu wa akili.
“Sasa watumishi wote tupo katika jengo moja, sitegemei kusikia
visingizio vya hapa na pale kuwa jalada fulani halipo Mtumba bali liko
Ofisi za UDOM kule ambako baadhi ya watumishi walikuwa wakifanya kazi, tufanye
kazi,” Mhe. Simbachawene amesisitiza.
Amesema kitendo cha Watumishi kuhamia katika jengo moja tofauti
na ilivyokuwa mwanzo ni muhimu sasa kwa Watumishi wa Ofisi yake kushirikiana
katika kufanya kazi ili kuhakikisha wateja wanaridhika na huduma wanazozipata.
"Serikali imejenga jengo zuri mno, hii kwenu ni motisha kubwa,
hivyo hakikisheni huduma mnazozitoa ziwe za viwango vya hali ya juu ili
kuendana na thamani ya jengo" amesema Mhe. Simbachawene.
Aidha, Mhe. Simbachawene ameiagiza Ofisi hiyo kuweka utaratibu
wa kufanya mazoezi kwa pamoja lengo likiwa ni kulinda afya pamoja na kujikinga
na magonjwa yasiyoambukiza ili kuweza kuwahudumia wananchi kwa ufanisi.
"Kwa sasa tupo jengo moja, naagiza utaratibu uandaliwe wa
kufanya mazoezi kwa pamoja ili kulinda afya zetu na kuwahudumia wananchi
ipasavyo" amesema Mhe.Simbachawene
Awali, Katibu Mkuu UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi alimshukuru Waziri
Simbachawene kwa wazo la kuandaa Iftar hiyo huku akiwataka Watumishi wa Ofisi
yake kushirikiana katika kuwahudumia wananchi.
"Mtaungana nami, leo ni siku muhimu sana ambapo Waislamu
mpo katika mfungo wa Ramadhani huku Wakristo mkiwa katika mfungo wa Kwaresma,
tumekutana hapa ili kufuturu pamoja kuonyesha ishara ya upendo na ushirikiano,"
Bw. Mkomi amesisitiza.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Bw. Xavier Daudi
akitoa neno la shukrani kwa Waziri Simbachawene amemuahidi kuwa maagizo
yote aliyoyatoa yatafanyiwa kazi chini ya uongozi wa Katibu Mkuu ikiwemo
utamaduni wa namna hiyo wa kukutana kwa pamoja.
Baadhi ya Wakurugenzi na Maafisa wa Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora wakiwa
katika mstari wakichukua futari jana jioni wakati wa Iftar iliyoandaliwa na
Ofisi hiyo ambapo Watumishi wote
walikutanishwa wakiwemo baadhi ya
viongozi kutoka Taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo, ikiwa ni hatua muhimu
ya kujumuika kwa pamoja mara baada ya kuhamia katika jengo jipya lililopo
Mtaa wa Utumishi, Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu, UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi akizungumza jana jioni na
Watumishi wa Ofisi yake kabla ya Iftar
iliyoandaliwa na Ofisi hiyo ambapo Watumishi
wote walikutanishwa wakiwemo baadhi ya
viongozi kutoka Taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo, ikiwa ni hatua muhimu
ya kujumuika kwa pamoja mara baada ya kuhamia katika jengo jipya lililopo
Mtaa wa Utumishi, Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu, UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi akitoa neneo la shukrani kwa jana jioni kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene mbele ya Watumishi
wa Ofisi hiyo baada ya Iftar iliyoandaliwa na Ofisi hiyo ambapo Watumishi wote walikutanishwa wakiwemo baadhi ya viongozi kutoka Taasisi
zilizo chini ya Ofisi hiyo, ikiwa ni hatua muhimu ya kujumuika kwa pamoja
mara baada ya kuhamia katika jengo jipya lililopo Mtaa wa Utumishi, Mji
wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma
Sehemu ya Watumishi wakimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene
wakati wa Iftar iliyoandaliwa na Ofisi
hiyo ambapo Watumishi wote
walikutanishwa wakiwemo baadhi ya
viongozi kutoka Taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo, ikiwa ni hatua muhimu
ya kujumuika kwa pamoja mara baada ya kuhamia katika jengo jipya lililopo
Mtaa wa Utumishi, Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene
(katikati) akiwa na Katibu Mkuu, UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi (kulia) pamoja na Naibu Katibu Mkuu, UTUMISHI, Bw. Xavier
Daudi ( kushoto) wakati wa Iftar iliyoandaliwa na Ofisi hiyo ambapo Watumishi wote walikutanishwa wakiwemo baadhi ya viongozi kutoka Taasisi
zilizo chini ya Ofisi hiyo, ikiwa ni hatua muhimu ya kujumuika kwa pamoja
mara baada ya kuhamia katika jengo jipya lililopo Mtaa wa Utumishi, Mji
wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma
Baadhi ya Maafisa wa Ofisi
ya Rais, Utumishi na Utawala Bora wakiwa katika mstari wakichukua futari jana
jioni wakati wa Iftar iliyoandaliwa na Ofisi hiyo ambapo Watumishi wote walikutanishwa wakiwemo baadhi ya viongozi kutoka Taasisi
zilizo chini ya Ofisi hiyo, ikiwa ni hatua muhimu ya kujumuika kwa pamoja
mara baada ya kuhamia katika jengo jipya lililopo Mtaa wa Utumishi, Mji
wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma
Sehemu ya Watumishi wakiwa katika Iftar
iliyoandaliwa na Ofisi hiyo ambapo Watumishi
wote walikutanishwa wakiwemo baadhi ya
viongozi kutoka Taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo, ikiwa ni hatua muhimu
ya kujumuika kwa pamoja mara baada ya kuhamia katika jengo jipya lililopo
Mtaa wa Utumishi, Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.
Baadhi ya Wakurugenzi na Maafisa wa Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora wakiwa
na nyuso za furaha jana jioni mara baada
ya Iftar iliyoandaliwa na Ofisi hiyo ambapo Watumishi wote walikutanishwa wakiwemo baadhi ya viongozi kutoka Taasisi
zilizo chini ya Ofisi hiyo, ikiwa ni hatua muhimu ya kujumuika kwa pamoja
mara baada ya kuhamia katika jengo jipya lililopo Mtaa wa Utumishi, Mji
wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.
Tuesday, March 26, 2024
MARUFUKU HUJUMA BAINA YA WATUMISHI MAHALI PA KAZI
Na.Lusungu Helela- Dodoma
Tarehe 26 Machi, 2024
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – UTUMISHI na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Bw. Juma Mkomi amewataka Watumishi katika ofisi yake kupendana na kuthaminiana mahali pa kazi huku akiwasihi kuacha tabia ya kuhujumiana.
Ametoa kauli hiyo leo Machi 26, 2024 Jijini Dodoma wakati akifungua Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kilichowakutanisha Watumishi hao pamoja na baadhi ya Wajumbe wa TUGHE Taifa.
"Sisi ni jicho katika Utumishi wa Umma tujitahidi kufanya kazi kwa kushirikiana na kuheshimiana ili kutimiza malengo tuliyojiwekea ikiwa ni pamoja na kutoa huduma kwa watumishi na wananchi kwa jumla kwa haraka na kwa ufanisi " amesisitiza Mkomi.
Bw. Mkomi amewataka watumishi hao kupendana kwa kuwa sehemu kubwa ya muda wao unatumika kazini. Hivyo, mazingira ya kazi yanatakiwa kuwa na amani na utulivu ili ufanisi uongezeke na mwananchi aweze kupata huduma bora.
Vilevile, ametoa wito kwa Wakurugenzi wote kuwaandaa watumishi walio chini yao kwa ajili ya kurithishana madaraka na kuwapa majukumu watumishi hao ili kuwajengea uwezo kiutendaji na kuwafanya waoneshe uwezo wao kazini.
Aidha, Katibu Mkuu Mkomi amewanyooshea vidole baadhi ya watumishi wenye tabia ya kuvujisha siri ambapo amewatahadharisha kuwa yeyote atakayebainika hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake.
Naye, Mwakilishi wa Katibu Mkuu, TUGHE Bw.
Nsubisi Mwasandende ametumia fursa ya mkutano huo kuwaomba Wakurugenzi wa Idara
na Vitengo kuwasikiliza watumishi walio chini yao kwa kuwa wanaweza kuwa na mawazo
mazuri yenye kujenga taasisi na Serikali kwa jumla.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi akifungua mkutano maalum wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi yake uliolenga kuwasilisha mapendekezo ya bajeti na mpango kazi wa mwaka wa fedha 2024/2025 uliofanyika Jijini Dodoma.
Wajumbe
wa Mkutano
Maalum wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Mwenyekiti wa Baraza hilo Bw.
Juma Mkomi (aliyekaa meza kuu) wakati akifungua mkutano wa Baraza hilo uliolenga
kuwasilisha mapendekezo ya bajeti na mpango kazi wa mwaka wa fedha 2024/2025
uliofanyika Jijini Dodoma.
Mkurugenzi
Msaidizi Sehemu ya Mipango na Bajeti, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Julieth
Magambo akiwasilisha mapendekezo ya bajeti na mpango kazi wa mwaka wa fedha
2024/2025 kwa Wajumbe wa Mkutano Maalum wa Baraza la
Wafanyakazi wa Ofisi hiyo (hawapo pichani) uliofanyika jijini Dodoma. Kulia ni
Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Ufuatiliaji na Tathmini, Bw. Patrick Allute.
Mkurugenzi
wa Idara ya Mipango, Bw. Cosmas Ngangaji akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi Bw. Juma Mkomi (hayupo pichani) wakati
wa Mkutano Maalum wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi
hiyo uliofanyika jijini Dodoma. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala
na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Ofisi hiyo Bw. Mussa Magufuli.
Sehemu ya Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakifuatilia wasilisho la taarifa ya
mapendekezo ya bajeti na mpango kazi wa mwaka wa fedha 2024/2025 wakati wa
Mkutano Maalum wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo uliofanyika jijini
Dodoma.
Mwakilishi
wa Katibu Mkuu-TUGHE, Bw. Nsubisi Mwasandende akiwasilisha hoja kwa Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (hayupo
pichani) wakati wa Mkutano Maalum wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo
uliofanyika jijini Dodoma.
Mjumbe wa Mkutano
Maalum wa Baraza la Wafanyakazi, Bw. Shaha Nampeha akichangia moja ya hoja
wakati wa mkutano huo uliolenga kuwasilisha taarifa ya mapendekezo ya bajeti na
mpango kazi wa mwaka wa fedha 2024/2025 uliofanyika jijini Dodoma
Sehemu ya Wajumbe wa Mkutano Maalum wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakifuatilia wasilisho la taarifa ya mapendekezo ya bajeti na mpango kazi wa mwaka wa fedha 2024/2025 uliofanyika jijini Dodoma.
Katibu Mkuu,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (katikati) akiwa
katika picha ya Pamoja na Wajumbe wa Mkutano Maalum wa Baraza la Wafanyakazi wa
Ofisi yake mara baada ya kufungua mkutano huo uliolenga kuwasilisha mapendekezo
ya bajeti na mpango kazi wa mwaka wa fedha 2024/2025 uliofanyika Jijini Dodoma.
Sunday, March 24, 2024
KAMATI YA BUNGE YAPITISHA MAKADIRIO YA BAJETI YA MWAKA 2024/25 YA TAASISI ZILIZO CHINI YA OFISI YA RAIS, UTUMISHI NA UTAWALA BORA
KAMATI YA BUNGE YAPITISHA MAKADIRIO YA BAJETI YA MWAKA 2024/25
YA TAASISI ZILIZO CHINI YA OFISI YA RAIS, UTUMISHI NA UTAWALA BORA
Na Lusungu Helela-Dodoma
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imepitisha Makadirio ya
Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2024/25 ya Taasisi zilizo chini ya Ofisi
ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Hayo yamesemwa na Makamu
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Florent Laurent Kyombo akikaimu nafasi ya
Mwenyekiti wa Kamati hiyo leo Machi 23, 2024 katika Ukumbi wa Mikutano wa Bunge
Jijini Dodoma mara baada ya wajumbe wa Kamati kujadili na kuridhia bajeti
katika kikao kilichohusisha Kamati hiyo na Watendaji wa Taasisi zilizo chini ya
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Amesema baada ya majadiliano
mazuri na maelezo ya ziada kutolewa kuhusiana na bajeti iliyotengwa, Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Utawala Katiba na Sheria imeridhia.
“Tunawatakia matumizi mema ya
fedha hizi pale zitakapokubaliwa kupitishwa katika vikao vya Bunge la Bajeti na
tunahitaji kuona bajeti ya fedha hizi inaakisi matarajio ya msingi ya nchi
yetu,” amebainisha Mhe. Kyombo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora,
Mhe. George Simbachawene ameishukuru Kamati hiyo kwa ushauri na kupitia bajeti
hiyo kifungu kwa kifungu na kutoa maelekezo ya kuboresha kabla ya kuiwasilisha
kwenye vikao vya Bunge la Bajeti.
“Mimi pamoja na timu yangu, tunatoa
shukrani za dhati kwa jinsi mnavyotoa michango yenu yenye muelekeo wa kuboresha
Utumishi wa Umma nchini ili kukidhi matakwa na maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Samia Suluhu Hassan” amesema Mhe. Simbachawene.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakiwa
katika kikao cha kamati hiyo na
Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora kilicholenga
kuwasilisha tarifa kuhusu utekelezaji wa mpango wa Bajeti
ya mwaka 2023/24 na makadirio ya mapato na matumizi ya Taasisi zote zilizo chini ya
Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/25
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akitoa ufafanuzi wa moja ya hoja iliyowasilishwa
na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala,
Katiba na Sheria wakati wa kikao cha kamati hiyo kuhusu utekelezaji wa mpango wa Bajeti ya mwaka
2023/24 na makadirio ya mapato na matumizi
ya Taasisi
zote zilizo chini ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa
fedha 2024/25
Katibu Mkuu-UTUMISHI, Juma Mkomi akitoa ufafanuzi wa hoja iliyowasilishwa
na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati
wa kikao cha kamati hiyo na Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhusu utekelezaji wa mpango wa Bajeti ya mwaka
2023/24 na makadirio ya mapato na matumizi
ya Taasisi
zilizo zote chini ya Ofisi hiyo kwa
mwaka wa fedha 2024/25
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka, Bw.
Firmin Msiangi akitoa ufafanuzi wa hoja iliyowasilishwa
na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati
wa kikao kazi cha kamati hiyo na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora kuhusu
utekelezaji wa mpango wa Bajeti ya mwaka 2023/24 na makadirio ya mapato na
matumizi ya Taasisi zote zilizo chini ya Ofisi kwa mwaka wa fedha 2024/25
Naibu Katibu
Mkuu, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Xavier Daudi akitoa ufafanuzi wa hoja iliyowasilishwa na Wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Utawala Katiba na Sheria wakati wa kikao kazi cha Kamati
hiyo na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ya
kuwasilisha taarifa kuhusu utekelezaji wa mpango wa Bajeti
ya mwaka 2023/24 na makadirio ya mapato na matumizi ya Taasisi zote zilizo chini ya
Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/25
Sehemu ya Watendaji wa
Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwa katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala,
Katiba na Sheria na Watendaji wa ofisi hiyo wakati wa uwasilishaji wa tarifa kuhusu utekelezaji wa mpango wa Bajeti ya mwaka 2023/24 na makadirio ya
mapato na matumizi ya Taasisi zilizo zote chini ya Ofisi kwa mwaka wa fedha 2024/25
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba
na Sheria, Mhe. Mashimba Ndaki akichangia hoja
kuhusu masuala ya utumishi wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala,
Katiba na Sheria na viongozi pamoja na watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhusu utekelezaji wa mpango wa Bajeti ya mwaka
2023/24 na makadirio ya mapato na matumizi
ya Taasisi
zote zilizo chini ya Ofisi hiyo kwa
mwaka wa fedha 2024/25
Tuesday, March 19, 2024
MAAFISA MASUULI WATAKIWA KUZINGATIA USHAURI WA WATAALAMU KATIKA TAASISI ZAO
Na. Veronica Mwafisi-Dodoma
Tarehe 19 Machi, 2024
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George
Simbachawene amewataka Maafisa Rasilimaliwatu na Maafisa Sheria kutoka katika
Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri za Wilaya kutoa ushauri mahususi kwa
Maafisa Masuuli wao ili kuepuka kuipa hasara Serikali.
“Ninajua
kusimamia rasilimaliwatu sio jambo jepesi kwani linahitaji hekima na busara. Wapo baadhi ya Maafisa Masuuli
ambao hawasikilizi na hawapendi kupokea ushauri wa kitaalamu kutoka kwa maofisa wao na hivyo kutoa uamuzi
kinyume na matakwa ya sheria na kanuni za Utumishi wa Umma, hivyo kuipa hasara Serikali”
amesema Mhe. Simbachawene.
Mhe.
Simbachawene ameongeza kuwa, iwapo sheria
na kanuni za usimamizi wa rasilimaliwatu katika utumishi wa umma hautazingatiwa, utaondoa
adhima ya Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwa na utumishi wa umma unaotenda
haki na wenye kuwajibika kwa
umma.
Aidha, amebainisha kuwa, taasisi za
umma zinapokuwa na malalamiko
mengi ya watumishi ni ishara kuwa watendaji wa ofisi hizo hawafanyi kazi
ipasavyo hata kama lalamiko liko
ndani ya uwezo wao. Hivyo, kitendo cha kupeleka malalamiko
hayo katika ngazi za juu kwa utatuzi ni dhihaka kwa utawala.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi Bw. Juma Mkomi
amesema Maofisa hao ni washauri wakuu wa Maafisa Masuuli katika taasisi zao,
hivyo wanatakiwa kutoa ushauri kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu ili
kuepuka kuumiza watumishi.
Bw.
Mkomi amewasihi maofisa hao kuhakikisha wanatatua matatizo ya watumishi wa umma
kwa kuwasikiliza na wakati mwingine kuwaonya kwanza kuliko kuwafukuza katika
utumishi wa umma jambo.
Awali, Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria
katika Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bi. Hilda Kabissa amesema kikao kazi hiki
kimelenga kuwajengea uwezo Maafisa Rasilimaliwatu na Maafisa Sheria katika
kutekeleza Sheria, Kanuni na Miongozo ya Utumishi wa Umma.
Amesema, anaamini mada zilizowasilishwa zimeeleka kwa
vizuri na washiriki wameahidi kuzifanyia kazi mafunzo haya kwa umahiri mkubwa
sana na kuhakikisha wanahimiza haki na wajibu kwa watumishi wa umma.
Ameongeza kuwa maofisa hao pamoja na mambo mengine
wamepitishwa katika masuala ya maslahi ya watumishi, uzingatiaji wa maadili
mahala pa kazi, mifumo ya TEHAMA Serikalini, kutambua mifumo ya upimaji wa
utendaji kazi Serikalini, utaratibu wa kuendesha mashauri ya kinidhamu katika
utumishi wa umma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na Maafisa Sheria na Maafisa Rasilimaliwatu wakati akifunga kikao kazi cha kujadili changamoto za utekelezaji wa Sheria, Kanuni na Miongozo ya Utumishi wa Umma kilichofanyika Jijini Dodoma.
Maafisa Sheria na
Maafisa Rasilimaliwatu wakimsikiliza Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
George Simbachawene alipokuwa akizungumza nao wakati wa kufunga
kikao
kazi cha kujadili changamoto za utekelezaji wa Sheria, Kanuni na Miongozo ya Utumishi wa Umma.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Mhe. George Simbachawene wakati wa kufunga kikao kazi cha kujadili changamoto za utekelezaji wa Sheria, Kanuni na Miongozo ya Utumishi wa Umma.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria, Bi.
Hilda Kabissa (katikati) akijibu hoja zilizowasilishwa na Maafisa Sheria na
Maafisa Rasilimaliwatu wakati wa kikao kazi cha
kujadili changamoto za utekelezaji wa Sheria, Kanuni na Miongozo ya Utumishi wa Umma kilichofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA Serikalini, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Priscus Kiwango akiwasilisha mada kwa Maafisa Sheria na Maafisa Rasilimaliwatu kuhusu Mifumo ya TEHAMA Serikalini wakati wa kikao kazi cha kujadili changamoto za utekelezaji wa Sheria, Kanuni na Miongozo ya Utumishi wa Umma.
Mkurugenzi wa Idara ya
Uendelezaji Taasisi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Bw. Nolasco Kipanda akiwasilisha mada kwa Maafisa Sheria na Maafisa Rasilimaliwatu kuhusu Muundo na mgawanyiko
wa majukumu wakati wa
kikao
kazi cha kujadili changamoto za utekelezaji wa Sheria, Kanuni na Miongozo ya Utumishi wa Umma
Afisa Sheria, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Edwin Bilikundi akiwasilisha mada kwa Maafisa Sheria na Maafisa Rasilimaliwatu kuhusu utaratibu wa kuendesha mashauri ya nidhamu katika utumishi wa umma wakati wa kikao kazi cha kujadili changamoto za utekelezaji wa Sheria, Kanuni na Miongozo ya Utumishi wa Umma.
Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George
Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wa Ofisi yake mara
baada kufunga kikao
kazi cha Maafisa Sheria na Maafisa Rasilimaliwatu kilichofanyika jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na
Maafisa Sheria na Maafisa Rasilimaliwatu mara baada ya kufunga kikao
kazi kilichofanyika jijini Dodoma.