Na. Veronica Mwafisi - Arusha
Tarehe 08 Februari, 2024
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. Ridhiwani Kikwete amezielekeza taasisi zote za umma kuweka mipango itakayozisaidia kutatua changamoto
ya urudufu wa mifumo ya TEHAMA ili kukuza na kuimarisha jitihada za serikali mtandao na
kuboresha utendaji kazi katika kutoa huduma bora kwa wananchi kwa lengo la
kufikia azma ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu
Hassan ya kuwa na serikali ya kidijitali.
Mhe. Kikwete ametoa maelekezo hayo jijini Arusha wakati
akifunga Kikao kazi cha nne cha serikali mtandao
kilichowashirikisha wadau zaidi ya 1300 wa serikali mtandao
nchini.
“Changamoto za TEHAMA ili
ziweze kufikia mafanikio katika utekelezaji wa jitihada za serikali mtandao,
hatua madhubuti zichukuliwe ikiwa ni pamoja na kujiwekea mipango katika taasisi
zenu ili changamoto hizo ziweze kutatuliwa,” Mhe. Kikwete
amesisitiza.
Aidha Mhe. Kikwete amewataka wataalam wa TEHAMA
kushirikiana na Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) katika kutekeleza jitihada za
serikali mtandao kupitia msaada na ushauri wa kitaalam unaotolewa na mamlaka
hiyo kwa lengo la kila mtumishi kuweza kuijenga serikali ya kidijitali.
Kwa upande
wake, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi ameipongeza
Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) kwa kutekeleza azma ya Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuijenga Tanzania kuwa ya kidijitali
kwa kuibadilisha nchi na utumishi wa umma kupitia sera na mbinu mbalimbali za
utendaji kazi serikalini ili kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kutumia TEHAMA.
Bw. Xavier ameongeza kuwa, kukutana kwa wadau mbalimbali katika kikao
kazi hicho kutoka katika Wizara, Taasisi na Mashirika iwasaidie kujadili hali
ya utekelezaji wa serikali mtandao katika taasisi za umma zikiwemo changamoto
na mbinu za kukabiliana nazo ili kupunguza gharama za uendeshaji wa serikali.
Naye,
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA), Mhandisi Benedict Ndomba amesema kuwa, miradi ya mifumo ya TEHAMA katika taasisi za umma nchini kupitia
kaulimbiu ya kikao kazi hicho ikizingatia Sera, Sheria, Kanuni na Miongozo ya
Serikali Mtandao katika ujenzi wa miundombinu na mifumo ya TEHAMA itasaidia
kupunguza urudufu wa mifumo, kurahisisha taasisi za umma kubadilishana taarifa
na kuokoa fedha za umma kwa kudhibiti upotevu wa mapato ya serikali.
Kikao kazi hicho kilichoanza tarehe 06 Februari, 2024 na kuhitimishwa leo
tarehe 08 kimebeba kaulimbiu ya “Uzingatiwaji wa Sera, Sheria, Viwango na Miongozo ya Serikali Mtandao
kwa Ubadilishanaji salama wa Taarifa”.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani
Kikwete akizungumza na washiriki wa kikao kazi cha nne cha serikali mtandao wakati akifunga kikao kazi hicho jijini
Arusha kilichoandaliwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA).
Washiriki wa kikao kazi cha nne cha serikali mtandao wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo
pichani) wakati akifunga kikao kazi hicho jijini Arusha kilichoandaliwa na
Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA).
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora Bw. Xavier Daudi akitoa neno la shukrani kwa Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete kwa kufunga kikao kazi cha nne cha serikali mtandao jijini Arusha.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) Mhandisi
Benedict Ndomba akieleza lengo la kikao kazi cha nne cha serikali mtandao kabla ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani
Kikwete kukifunga kikao hicho jijini Arusha.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani
Kikwete akisisitiza jambo kwa washiriki wa kikao kazi cha nne cha serikali mtandao wakati akifunga kikao kazi hicho jijini
Arusha kilichoandaliwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA).
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani
Kikwete akitazama kifaa cha kupima kiasi cha gesi na mafuta alipotembelea
banda la Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) wakati wa kikao kazi cha nne cha serikali
mtandao kilichofanyika jijini Arusha.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani
Kikwete akitazama kipeperushi cha Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) alipotembelea
banda hilo wakati wa kikao kazi cha nne
cha serikali mtandao kilichoandaliwa na Mamlaka ya
Serikali Mtandao (eGA) jijini Arusha.
No comments:
Post a Comment