Na. Veronica Mwafisi- Kilosa, Mikumi na Dumila
Tarehe 19 Desemba, 2023
Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA Serikalini, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora
ambaye pia ni Msimamizi Mkuu wa Mafunzo ya PEPMIS, PIPMIS na HR Assesment kwa
Mkoa wa Morogoro, Bw. Priscus
Kiwango amewataka watumishi wa umma katika mkoa wa Morogoro kuzingatia
mafunzo wanayopewa ili kuboresha utendaji kazi wao na taasisi kwa jumla.
Bw. Kiwango amesema mifumo hii itawawezesha viongozi kusimamia utendaji kazi wa watumishi wao bila upendeleo ikiwemo kupanda vyeo kwa haki, kupima utendaji kazi wa Taasisi za Umma na kufanya Tathmini ya hali ya Rasilimaliwatu Serikalini kwa lengo la kuimarisha utoaji wa huduma kwa umma.
Amesema hayo katika nyakati tofauti wakati wa mafunzo ya namna ya kutumia mifumo mipya ya PEPMIS, PIPMIS na HR Assesment kwa Watumishi wa Umma na taasisi zilizopo mkoani Morogoro katika Kanda tatu ikiwemo Mikumi, Kilosa Mjini na Dumila.
Mkurugenzi
Kiwango ameongeza kuwa mafunzo hayo yanaendelea kutolewa kwenye Halmashauri ya
Wilaya Kilosa, Gairo, Morogoro mjini na kwa baadhi ya taasisi na kwa watendaji
wa kata na vijiji, walimu wa sekondari na msingi, watumishi wa kilimo, mifugo
na ustawi wa jamii.
“Mpaka sasa kwa mkoa wa
Morogoro tumetoa mafunzo kwa taasisi 21 ikiwemo Ofisi ya RAS, Halmashauri ya
Morogoro DC, Manispaa ya Morogoro, Mvomero, Malinyi, Mlimba, Ifakara Ulanga,
Kilosa, Mikumi na Dumila na kwa mwenendo huu tutakamilisha mafunzo kwa wakati
uliopangwa”. Alisema Bw. Kiwango.
Kwa upande wake, Mkufunzi wa mafunzo hayo ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi
anayesimamia huduma za Uuguzi na Ukunga nchini, Wizara ya Afya, Bw. Paul
Mashauri amesema watumishi wa umma mkoa wa Morogoro wanaonesha utayari wa
kutumia mifumo hii katika utendaji kazi wao kutokana na uwazi uliopo katika
mifumo.
Naye, Mkurugenzi Msaidizi Mipango na Bajeti, Wizara ya Mifugo na
Uvuvi, Bi. Matilda Mtenga ambaye pia ni mkufunzi ameongeza kuwa, mwitikio
wa watumishi wa umma katika mkoa wa Morogoro ni mkubwa na wanafurahi kuona ujio
wa mifumo inayonesha uwezo wa kila
mtumishi wa umma.
Ofisi ya Rais-UTUMISHI inaendelea
kutoa Mafunzo ya PEPMIS, PIPMIS na HR Assesment katika Mikoa yote Tanzania Bara
na yanatarajiwa kuhitimishwa Desemba 31,2023.
Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA Serikalini, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambaye pia ni Msimamizi Mkuu wa Mafunzo ya Mifumo ya
PEPMIS, PIPMIS na HR Assesment kwa Mkoa wa Morogoro Bw. Priscus Kiwango akizungumza
na baadhi
ya Viongozi na Watumishi wa Halmashauri Wilaya ya
Kilosa Kanda ya Mikumi wakati akifungua
Mafunzo
ya Mifumo hiyo katika Ukumbi wa Veta mkoani humo.
Baadhi ya Viongozi na Watumishi wa Halmashauri
Wilaya ya Kilosa Kanda ya Mikumi wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA Serikalini, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora ambaye pia ni Msimamizi Mkuu wa Mafunzo ya Mifumo ya PEPMIS, PIPMIS na
HR Assesment kwa Mkoa wa Morogoro Bw. Priscus Kiwango (hayupo
pichani) wakati akifungua
Mafunzo
ya Mifumo hiyo.
Baadhi ya Viongozi na Watumishi wa Halmashauri
Wilaya ya Kilosa wakifuatilia Mafunzo ya Mifumo ya PEPMIS, PIPMIS na HR Assesment
yanayotolewa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
mkoani Morogoro.
Mkurugenzi Msaidizi
anayesimamia huduma za Uuguzi na Ukunga nchini, Wizara ya Afya, ambaye pia ni Mkufunzi
wa mafunzo ya PEPMIS, PIPMIS na HR Assessment, Bw. Paul Mashauri akiwaelekeza watumishi
wa Halmashauri Wilaya ya Kilosa, Kanda ya Mikumi mkoani
Morogoro
namna ya kuingia na kutumia Mifumo hiyo wakati wa mafunzo.
Mkurugenzi
Msaidizi Mipango na Bajeti, Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mkufunzi wa
mafunzo ya PEPMIS, PIPMIS na HR Assessment, Bi. Matilda Mtenga akiwaelekeza
watumishi Halmashauri Wilaya ya Kilosa, Kanda ya Mikumi mkoani Morogoro
namna ya kuingia na kutumia Mifumo hiyo wakati wa mafunzo.
No comments:
Post a Comment