Na. James K. Mwanamyoto-Kilosa
Tarehe 20 Disemba, 2022
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama amesema Serikali ya Awamu ya Sita haitosita kumchukulia hatua za kinidhamu na kisheria kiongozi yeyote atakayeshindwa kusimamia vizuri rasilimaliwatu kwa ajili ya ustawi wa taifa.
Mhe. Jenista amesema hayo, wakati wa kikao kazi chake na watumishi wa umma katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro kilicholenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi katika halmashauri hiyo.
Mhe. Jenista amesema, hatomuonea aibu wala huruma kiongozi yeyote aliyepewa dhamana ya kusimamia rasilimaliwatu ambaye atabainika kukiuka sheria na taratibu za usimamizi wa rasilimaliwatu.
Mhe. Jenista ameongeza kuwa, viongozi wenye dhamana ya kusimamia rasilimaliwatu wanapaswa kuiheshimu, kuithamini na kuhakikisha inakuwa kwenye mikono salama kwasababu inategemewa na Serikali kwa kiasi kikubwa katika ustawi na maendeleo ya taifa.
“Rasilimaliwatu ambayo ndio watumishi wa umma ikisimamiwa vizuri itaisaidia Serikali kutimiza lengo la kutoa huduma bora kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kutekeleza mipango na mikakati ya maendeleo katika taifa,” Mhe. Jenista amefafanua.
Mhe. Jenista amesisitiza kuwa, watumishi wa umma ndio wanategemewa kutoa huduma bora za afya, kuboresha huduma za maji, kuboresha huduma za elimu, kuboresha huduma za miundombinu pamoja na kilimo.
Akizungumza kwa niaba ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Kilosa, Mwalimu Richard Shagungu ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayoongozwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kulipa kila mwezi madai ya malimbikizo ya mishahara ya watumishi katika Halmashauri hiyo na kuomba waajiri wasizalishe madai mapya ili Serikali iyamalize madai yaliyopo sasa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama amefanya
ziara ya kikazi ya siku moja katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa ili
kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma, kutatua changamoto zinazowakabili
watumishi wa umma pamoja na kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya
Maskini katika Halmashauri hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza
na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro, wakati
wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto
zinazowakabili watumishi katika halmashauri hiyo.
Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya
Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama alipokuwa
akizungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji
na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi hao.
Mbunge wa Jimbo la Kilosa, Mhe. Prof.
Palamagamba Kabudi akitoa salaam za wananchi wa jimbo lake kwa Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista
Mhagama wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo iliyolenga kuhimiza
uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma katika
Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa.
Mbunge wa Jimbo la Mikumi, Mhe.
Dennis Londo akitoa salaam za wananchi wa jimbo lake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama
wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na
kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma katika Halmashauri ya
Wilaya ya Kilosa.
Mwenyekiti wa Chama cha Walimu
Kilosa, Mwalimu Richard Shagungu akitoa shukrani kwa niaba ya Watumishi wa
Kilosa kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa Mhe. Dkt.
Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kulipa madai ya malimbikizo ya mishahara ya watumishi
katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akiimba
Wimbo wa Taifa na viongozi wengine walio meza kuu kabla ya kuzungumza na
watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro, wakati
ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto
zinazowakabili watumishi katika halmashauri hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana
baadhi ya viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, mara baada ya kuwasili
Wilayani humo ili kuzungumza na watumishi wa umma wa Halmashauri hiyo, wakati
ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto
zinazowakabili watumishi walio katika halmashauri hiyo.
No comments:
Post a Comment