Monday, December 5, 2022

MHE. JENISTA AWASISITIZA WATENDAJI WA OFISI YAKE KUWA NA KAULI NZURI NA KUTOA HUDUMA BORA KWA WANANCHI NA WATUMISHI WANAOWAHUDUMIA

Na. James K. Mwanamyoto-Babati

Tarehe 05 Disemba, 2022

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama amewasisitiza  Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhakikisha kauli nzuri na huduma bora zinapewa kipaumbele  kwa watumishi wa umma na wananchi wanaohudumiwa na ofisi yake. 

Mhe. Jenista ametoa maelekezo hayo Mjini Babati, wakati akifungua Mkutano Maalum wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora uliofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara. 

Mhe. Jenista amewataka watendaji wa ofisi yake kuwapokea vizuri na kutoa kauli nzuri kwa watumishi wa umma na wananchi pindi wanapowahudumia, kama ambavyo Mhe. Rais alivyowaamini na kuwapatia dhamana hiyo ya kuwahudumia kwa maslahi na maendeleo ya taifa.  

“Lugha nzuri wakati wa kumuhudumia mteja katika Ofisi ya Rais-UTUMISHI ni nyenzo muhimu katika utoaji wa huduma bora na haki kwa watumishi wa umma na wananchi wanaofuata huduma katika ofisi yetu, hivyo mnapaswa kuzingatia  ili kufikia azma ya Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutoa huduma bora kwa kila mwananchi,” Mhe. Jenista amesisitiza. 

Mhe. Jenista amesema, Ofisi ya Rais-UTUMISHI ndio imepewa dhamana ya kusimamia maadili ya watumishi katika taasisi za umma, hivyo watendaji wa ofisi yake wanapaswa kuwa mfano bora wa kuigwa kwa kuwa na maadili kiutendaji katika Utumishi wa Umma nchini. 

Kwa upande wake, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi hakusita kuwapongeza watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI kwa kufanya kazi kwa bidii maarifa katika kumsaidia Mhe. Jenista Mhagama na yeye mwenyewe kutekeleza jukumu walilopewa na Mhe. Rais la kumsaidia kusimamia vema Utumishi wa Umma ili uwe na tija katika kutoa huduma bora kwa wananchi na maendeleo ya taifa kwa ujumla. 

Naye, Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Cosmas Ngangaji kwa niaba ya wajumbe wa baraza na watumishi wote, amemshukuru Mhe. Jenista kwa kuwataka watumishi kuwa na hofu ya Mungu ili wawe waadilifu katika kuwahudumia wananchi na kumuahidi Mhe. Jenista kuwa wamepokea maelekezo hayo na yatazingatiwa kikamilifu. 

Akizungumzia utekelezaji wa maelekezo ya Mhe. Jenista, mmoja wa Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Mwamvita Shamte amesema, wajumbe watajitahidi kuwaelimisha watumishi wenzao ili watoe huduma nzuri ambayo Serikali imekusudia kuitoa, hivyo amewataka wananchi na watumishi wa umma kutosita kupata huduma ofisi ya Rais-UTUMISHI. 

Mjumbe mwingine, Bw. Romward Rwamarumba amesema kuwa, watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI watajipanga kuzingatia maadili katika utendaji kazi kwa kutambua kuwa ofisi yao ndio inayosimamia maadili Serikalini, na kuahidi kuwa mstari wa mbele katika kuzingatia maadili ili kuwa kioo na mfano wa kuigwa na watumishi wengine walio katika Taasisi za Umma nchini. 

Wajumbe wa Mkutano Maalum wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wamepata fursa ya kupatiwa mafunzo ya Maadili katika Utumishi wa Umma na namna ya kukabiliana na msongo ili waweze kutekeleza majukumu yao kikamilifu.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akifungua Mkutano Maalum wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora uliofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara.


Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano Maalum wa Baraza hilo uliofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara.


Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Bi. Catherine Mthapula akitoa salamu za Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Makongoro Nyerere kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama kabla ya Waziri huyo kufungua Mkutano Maalum wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora uliofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama kufungua Mkutano Maalum wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora uliofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara.


Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi akiongoza Mkutano Maalum wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora uliofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara.


Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Cosmas Ngangaji akitoa neno la shukrani  kwa niaba ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama aliyefungua Mkutano Maalum wa baraza hilo uliofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara.


Mmoja wa Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bi. Mwamvita Shamte akieleza namna Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora walivyojipanga kutekeleza maelekezo ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma ya kutoa huduma bora kwa wananchi.


Mjumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Romward Rwamarumba akitoa ahadi ya kutekeleza maelekezo ya Mhe. Jenista Mhagama ya kutoa huduma bora kwa wananchi aliyoyatoa wakati akifungua Mkutano Maalum wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora uliofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara.

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora mara baada ya kufungua Mkutano Maalumu wa Baraza hilo uliofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akiteta na Naibu Waziri wake Mhe. Deogratius Ndejembi kabla ya kufungua Mkutano Maalum wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora uliofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara.

 


 

No comments:

Post a Comment