Tuesday, January 14, 2020

WAZIRI MKUU AITAKA JAMII KUSHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA VITA DHIDI YA RUSHWA NCHINI



Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akimkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) kuzindua ofisi mpya za TAKUKURU zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Mkoani Lindi jana.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akimkaribisha, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) kuzungumza na wananchi mara baada ya kuzindua jengo jipya la TAKUKURU katika Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Mkoani Lindi jana.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) akizungumza na wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Mkoani Lindi baada ya kuzindua jengo jipya la TAKUKURU jana.

Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) alipokuwa akizungumza nao jana baada ya kuzindua jengo jipya la TAKUKURU katika Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Mkoani Lindi.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo jipya la TAKUKURU katika Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Mkoani Lindi jana. Kushoto kwake ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi na wa kwanza kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brigedia Jenerali, John Mbungo.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) akipanda mti baada ya kuzindua jengo jipya la TAKUKURU lililopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Mkoani Lindi jana. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na  Usalama ya Mkoa wa Lindi baada ya kuzindua jengo jipya la TAKUKURU lililopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Mkoani Lindi jana.


No comments:

Post a Comment