Thursday, December 8, 2016

MHE. KAIRUKI NA BALOZI WA JAPANI NCHINI WAFANYA MAZUNGUMZO KUHUSU USHIRIKIANO KATI YA TANZANIA NA JAPANI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo na Balozi wa Japani nchini Tanzania, Mhe. Masaharu Yoshida (hayupo pichani) alipomtembelea ofisini kwake leo kuzungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Japani hususan suala la wataalamu wa kujitolea wanaokuja kufanya kazi nchini katika sekta mbalimbali.

Balozi wa Japani nchini Tanzania, Mhe. Masaharu Yoshida (kushoto) akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (hayupo pichani) alipomtembelea ofisini kwake leo kuzungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Japani hususan suala la wataalamu wa kujitolea wanaokuja kufanya kazi nchini. Kulia kwake ni Afisa wa Ubalozi wa Japani nchini, Bi. Yoko Kamiyana.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (wa pili kulia) akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Masaharu Yoshida (wa pili kushoto) alipomtembelea ofisini kwake leo kuzungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Japani hususan suala la wataalam wa kujitolea wanaokuja kufanya kazi nchini katika sekta mbalimbali.

Tuesday, December 6, 2016

UFUNGUZI WA MAFUNZO YA UFUATILIAJI NA TATHMINI

KAYA 55,692 ZAONDOLEWA KWENYE MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASIKINI KATIKA AWAMU YA TATU YA TASAF. WATENDAJI MBALIMBALI WASIMAMISHWA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na Vyombo vya Habari jijini Dar es Salaam kuhusu Kaya zilizoondolewa kwenye Mpango wa kunusuru Kaya Masikini (TASAF), Awamu ya Tatu kwa kukosa sifa. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu, Ikulu, Bw. Peter Ilomo na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Susan Mlawi.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akisisitiza jambo kwa Waandishi wa Habari kuhusu Kaya zilizoondolewa kwenye Mpango wa kunusuru Kaya Masikini katika Awamu ya Tatu ya TASAF Tatu kwa kukosa sifa.