Thursday, August 28, 2025

TIMU YA MPIRA WA PETE OFISI YA RAIS - UTUMISHI YAJIAANDA VYEMA KWA AJILI YA MASHINDANO YA SHIMIWI 2025, MWANZA.

 

Na Eric Amani

 

Timu ya Mpira wa Pete ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, imeendelea na mazoezi yake  katika jiji la Dodoma ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kushiriki mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) mwaka 2025 ambayo yanatarajiwa kuanza mwezi Septemba 1.

 

Wachezaji wa timu hiyo wameonyesha ari na mshikamano mkubwa, wakilenga kufanya vizuri katika mashindano hayo yanayotarajiwa kukutanisha timu mbalimbali za watumishi wa umma kutoka wizara, idara na taasisi mbalimbali za serikali katika Jiji la Mwanza.


Mashindano ya SHIMIWI 2025 yamekuwa chachu ya kuimarisha afya za watumishi, kukuza vipaji na kuimarisha mshikamano kazini kupitia  michezo  ikiwemo mpira wa pete, riadha, mpira wa miguu na michezo mingine.

Sehemu ya Wachezaji wa Mpira wa Pete wa Ofisi ya Rais - UTUMISHI wakifanya mazoezi ya viungo ikiwa ni maandalizi ya kushiriki mashindano ya SHIMIWI 2025 jijini Mwanza


Timu ya Mpira wa Pete Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwa katika mechi ya mazoezi kwa ajili ya kujianda na mashindano ya SHIMIWI 2025

Sehemu ya Wachezaji wa mpira wa pete "NETBALL" wakiwania mpira katika muendelezo wa mazoezi yaliyofanyika katika viwanja wa vijana jijini Dodoma


Wednesday, August 27, 2025

WAZIRI SIMBACHAWENE: SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI MCHANGO WA WA KADA YA MENEJIMENTI YA KUMBUKUMBU NYARAKA

 Na. Mwandishi Wetu

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,  Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amesema Serikali inatambua na kuthamini  mchango wa  kada ya Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka katika ustawi wa utumishi wa umma huku akiahidi wakati wote  Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora itaendelea  kutoa ushikiano kwa kada hiyo ili kuendelea kufanikisha masuala mbalimbali ya kiutumishi.

Mhe Simbachawene ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam kwenye Mkutano Mkuu wa 13 wa Chama Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka ( TRAMPA ) kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Kassim Majaliwa kwa ajili ya  kufungua Mkutano huo.

 Amesema mikutano hiyo ya Kitaaluma imekuwa ikileta tija kwa Wanataaluma hao  kwani mbali ya kupata maarifa bali wamekuwa wakibadilishana mawazo ya namna bora  ya kuboresha utendaji kazi wao 

 Ameongeza kuwa " Mikutano hii ni muhimu kwao   kwani imekuwa ikitoa dira kwa Wanataaluma  namna ya kutumia mifumo ya TEHAMA katika kazi zao za kila siku badala ya utaratibu wa ubebaji wa mafaili uliokuwa ukifanyika hapo awali " 

 Aidha, Mhe.Simbachawene amewataka Wanachama hao kufanya kazi kwa bidii na kujiongezea maarifa ili kuendana na mabadiliko ya TEHAMA  yanatokea katika utendaji kazi wao wa kila siku huku akiwataka Waajiri kuhakikisha wanakuwa msaada katika kuwawezesha kutekeleza majukumu yao.

 Wakati huo huo, Waziri Simbachawene amesema kuwa Serikali imeendelea kutoa ajira kwa watumishi wa umma wakiwamo watunza kumbukumbu. Katika mwaka 2024-2025 kada hii tu ajira mpya zilizotolewa ni 965 waliopandishwa cheo ni 1,237, kuwabadilishia kada watumishi 59 (Recategorization) pamoja na kulipa malimbikizo ya mishahara kiasi cha shilingi milioni 204.6

 Katika hatua nyingine,  Ofisi ya Rais, UTUMISHI na Utawala Bora imeahidi kuchangia  kiasi cha Shilingi Mil.10 ikiwa ni mchango wake kwa ajili ya kuwezesha ujenzi wa Kituo cha Maarifa kitakachokuwa na masijala ya mfano, kumbi za mikutano pamoja na ofisi za TRAMPA kinachotarajiwa kujengwa jijini Dodoma.

 Akizungumza mara baada ya kutoa ahadi hiyo, Mhe.Simbachawene amesema  kimsingi kazi hiyo ya ujenzi wa Kituo Maalum cha Maarifa cha TRAMPA kilipaswa kujengwa  na Serikali hivyo wao kama Ofisi yenye dhamana ya kusimamia Watumishi wa Kada hiyo imeamua kuwa mstari wa mbele kuchangia kiasi hicho 

 Naye, Katibu Mkuu, UTUMISHI, Bw .Juma Mkomi ameahidi kutoa Sh.milioni 10 kwa niaba ya timu Menejimenti ya Ofisi hiyo ili kuhakikisha maono ya kujenga Kituo hicho cha Maarifa yanatimia.

 Awali, Mwenyekiti wa TRAMPA, Devota Mrope amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya katika sekta mbalimbali iliwemo katika kada ya Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka.

 Rais Dkt. Samia amekuwa mwana TRAMPA namba moja, amepigania maslahi ya watumishi wa umma ikiwemo sisi  mwana TRAMPA, ametoa ajira nyingi katika kipindi kifupi ikiwemo kwa  wanataaluma wa kada hii ya Menejimenti ya kumbukumbu na nyaraka, amefanyia kazi changamoto zetu kwa kiasi kikubwa. 

 

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Kassim Majaliwa akikabidhiwa mfano wa funguo ya gari la wagonjwa kutoka kwa  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene  lililotolewa na Chama Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka ( TRAMPA ) kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe. Samia Suluhu Hassan ikiwa ni zawadi ya kutambua mchango wake kwa wanachama wa TRAMPA mara baada ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akifungua  Mkutano Mkuu wa 13 wa Chama Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka ( TRAMPA ) uliofanyika leo jijini Dar es Salaam

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Kassim Majaliwa akizungumza wakati akifungua  Mkutano Mkuu wa 13 wa Chama Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka ( TRAMPA ) uliofanyika leo jijini Dar es Salaam

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa 13 wa Chama Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka ( TRAMPA ) kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Kassim Majaliwa kufungua Mkutano huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam



Sehemu ya Wanachama wa Chama Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka ( TRAMPA ) Wwakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa 13 wa Chama Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka ( TRAMPA ) kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Kassim Majaliwa kufungua Mkutano huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam



Mwenyekiti wa Chama Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka (TRAMPA) Bi. Devotha Mrope  akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa 13 wa Chama Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka ( TRAMPA ) kabla ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Kassim Majaliwa kufungua Mkutano huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam







 

 


KITUO CHA HUDUMA KWA MTEJA, OFISI YA RAIS-UTUMISHI

Maafisa kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakitoa huduma kwa Watumishi na Wananchi wanaopiga simu kwenye Kituo cha Huduma kwa Mteja (Call Centre) cha Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali kutoka katika ofisi hiyo iliyopo katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma leo.





 






Tuesday, August 26, 2025

WATUMISHI WA UMMA NCHINI WAASWA KUACHA KUKOPA KUPITA KIASI

Na.Lusungu Helela- Dar es Salaam

 Mkurugenzi wa Usimamizi wa Maadili, Ofisi Rais, UTUMISHI,  Bi.Felister Shuli amewaasa Watumishi wa Umma nchini kuacha tabia ya kukopa kupita kiasi huku akisisitiza kuwa kitendo hicho ni kinyume na maadili katika  Utumishi wa Umma nchini.

 Mkurugenzi Shuli ametoa kauli hiyo  leo Jumanne Agosti 26, 2025 jijini Dar es Salaam wakati akiwasilisha mada ya Maadili katika Utumishi wa Umma katika Mkutano wa 13 wa Chama Cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka ( TRAMPA) unaotarajiwa kufunguliwa rasmi kesho na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Kassim Majaliwa.

 Amesema kitendo hicho cha Mtumishi kukopa kupita kiasi humpelekea  kupata msongo wa mawazo na kusababisha kuwahudumia wateja kwa ukali au kwa kukosa  staha kutokana msongo wa mawazo alionao unaosababishwa na  madeni 

 Ameongeza kuwa baadhi ya Watumishi waliokopa kupita kiasi hujikuta ni watu wa kuhangaika hangaika na muda mwingine huwa na  mahudhurio  hafifu kazini " huwa ni watu wa  kujificha na kukimbia kimbia  ili  wadai wake wasiweze kuwaona kwani baadhi ya wadai wao huwafuata ofisini" amesema 

 Kufuatia hatua hiyo, Bi.Shuli amewataka Watumishi kuishi kulingana na kipato chao ili wasiweze kujiingiza kwenye madeni yasiyolipika na hivyo  kusababisha kushindwa kutoa huduma bora kwa wananchi. 

 Katika hatua nyingine, Bi.Shuli amewataka watumishi wa umma kujiepusha  na  michezo ya bahati nasibu na kubashiri ( betting ) kwani ni ukiukwaji wa Maadili katika  Utumishi wa Umma nchini

 " Jiepusheni na "betting" kwani watumishi wanaocheza michezo hiyo hujikuta wakitumia muda mwingi na fedha nyingi kucheza michezo hiyo na hivyo kusababisha kukopa kupita kiasi.

 

Mkurugenzi wa Usimamizi wa Maadili, Ofisi Rais, UTUMISHI,  Bi.Felister Shuli akizungumza leo  jijini Dar es Salaam wakati akiwasilisha mada ya Maadili katika Utumishi wa Umma katika Mkutano wa 13 wa Chama Cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka ( TRAMPA) unaotarajiwa kufunguliwa rasmi kesho na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Kassim Majaliwa.    








Baadhi ya Wanachama wa Chama cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka (TRAMPA)  wakimsikiliza  Mkurugenzi wa Usimamizi wa Maadili, Ofisi Rais, UTUMISHI,  Bi.Felister Shuli  wakati akiwasilisha mada ya Maadili katika Utumishi wa Umma katika Mkutano wa 13 wa  TRAMPA unaotarajiwa kufunguliwa rasmi kesho na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Kassim Majaliwa.





  Rais wa  Chama cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka (TRAMPA) Bi. Devotha Mrope  akizungumza na Wanachama wa TRAMPA kwenye  Mkutano wa 13 wa  TRAMPA ulioanza jana na  unaotarajiwa kufunguliwa rasmi kesho na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Kassim Majaliwa.

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utawala na Utumishi wa Umma  kutoka  Ofisi Rais, UTUMISHI,  Bw. Andrew Ponda  akizungumza leo  jijini Dar es Salaam wakati akiwasilisha mada ya masuala ya Uhamisho kwa njia ya mfumo  katika Mkutano wa 13 wa Chama Cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka ( TRAMPA) unaotarajiwa kufunguliwa rasmi kesho na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Kassim Majaliwa

 

Monday, August 25, 2025

MAFUNZO ELEKEZI KWA WATUMISHI OFISI YA RAIS-UTUMISHI KUONGEZA TIJA YA UTENDAJI KAZI


Mtaalam wa Saikolojia, Dkt. Chris Mauki akisisitiza jambo kwa watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi  watumishi wa ofisi hiyo yaliyofanyika katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI (wa kwanza kushoto) Bw. Xavier Daudi akifuatilia mafunzo ya kujengewa uwezo na kuimarisha utendaji kazi watumishi wa ofisi hiyo yaliyofanyika katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma. Wengine ni Wakurugenzi na Watumishi wa ofisi hiyo.

Sehemu ya Wakurugenzi na Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakifuatilia mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.


Sehemu ya Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakifurahia jambo wakati wa mafunzo yaliyolenga kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi yaliyofanyika katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakifuatilia mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.


Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakifuatilia mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.


Sehemu ya Wakurugenzi na Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakifuatilia mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.


Sehemu ya Wakurugenzi, Wakurugenzi wasaidizi na Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakifuatilia mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.


Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakifuatilia mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

 




Saturday, August 23, 2025

UTEKELEZAJI MRADI WA UJENZI WA MAKAZI KWA WATUMISHI WA UMMA KUONGEZA CHACHU YA UTENDAJIKAZI KWA MAENDELEO YA TAIFA

 






UTEKELEZAJI MRADI WA UJENZI WA MAKAZI KWA WATUMISHI WA UMMA KUONGEZA CHACHU YA UTENDAJIKAZI KWA MAENDELEO YA TAIFA

Na. Veronica Mwafisi-Dodoma

Timu ya wataalam kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Wizara ya Fedha na Watumishi Housing Investments (WHI) imehitimisha ziara ya kikazi katika Mikoa ya Singida, Ruvuma, Lindi, Pwani na Dodoma iliyolenga kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa makazi kwa Watumishi wa Umma.

Akizungumza mara baada ya kuhitimisha ziara hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Patrick Allute, amesema watumishi wa umma wanafurahia utekelezaji wa mradi huo ambao wanaamini utaleta motisha ya utendajikazi kwa kuwa karibu na eneo la kazi lenye makazi bora.

Kwa niaba ya timu hiyo Mkurugenzi Allute ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kutekeleza kwa vitendo azma yake ya kuwathamini watumishi wa umma kwa kuboresha mazingira ya utendaji kazi.

Kwa upande wake, Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka Wizara ya fedha, Bw. Ezekiel Odipo ameeleza kuwa, Serikali inawajali watumishi wa umma hivyo imetoa fedha za kutosha ili kuboresha mazingira ya kazi ikiwemo utekelezaji wa mradi wa makazi ya watumishi ili waweze kutoa huduma bora kwa jamii.

Naye, Mhandisi Salum Chanzi kutoka Watumishi Housing Investments, amesema WHI ndiyo kandarasi inayojenga makazi katika mradi huo ambao kwa sasa umefikia 85%.

Aidha, Mhandisi Chanzi amesema makazi hayo yatakuwa na ubora wa hali ya juu utakaoongeza ufanisi wa kazi kutokana na mazingira bora watakayokuwa nayo watumishi wa umma. 

Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Patrick Allute (watatu kutoka kulia) akizungumza jambo na Afisa kutoka ofisi hiyo Bw. Rashid Shedafa (wakwanza kushoto) wakati wa kuhitimisha ziara ya kikazi iliyolenga kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi kwa makazi ya watumishi wa umma katika Shule ya Msingi Mlezi, mkoani Dodoma.



Mwonekano wa jengo la mradi wa makazi ya watumishi wa umma lililopo katika Shule ya Msingi Mlezi, mkoani Dodoma.

Timu ya wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Wizara ya Fedha na Watumishi Housing Investments ikijadili jambo wakati wa kuhitimisha ziara ya kikazi iliyolenga kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi kwa makazi ya watumishi wa umma katika Shule ya Msingi Mlezi, mkoani Dodoma.


Timu ya wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Wizara ya Fedha na Watumishi Housing Investments ikikagua maendeleo ya mradi wa ujenzi kwa makazi ya watumishi wa umma katika Shule ya Msingi Mlezi, mkoani Dodoma.



Thursday, August 21, 2025

UTEKELEZAJI WA MRADI WA UJENZI WA MAKAZI YA WATUMISHI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MPWAPWA

 HABARI KATIKA PICHA

Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Patrick Allute (aliyenyoosha mkono) akizungumza jambo na Afisa Usimamizi wa Fedha Mwandamizi kutoka Wizara ya fedha, Bw. Ezekiel Odipo (wakwanza kushoto) wakati wa ziara ya kikazi iliyolenga kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa makazi ya watumishi wa umma katika Shule ya Sekondari Lumuma Green, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.


Mwonekano wa jengo la mradi wa makazi ya watumishi wa umma lililopo katika Shule ya Sekondari Lumuma Green, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.


Fundi mkuu anayejenga makazi ya watumishi wa umma, katika Shule ya Msingi Chaludewa, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, Bw. Fadhili Kabainda (wapili kutoka kulia) akifafanua jambo kwa Mhandisi Salum Chanzi kutoka Watumishi Housing Investments (wakwanza kulia) wakati wa ziara ya timu ya wataalam kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Wizara ya Fedha na Watumishi Housing Investments iliyolenga kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa makazi ya watumishi wa umma katika Halmashauri hiyo mkoani Dodoma.


Timu ya wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Wizara ya Fedha na Watumishi Housing Investments ikijadili jambo wakati wa ziara ya kikazi iliyolenga kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa makazi ya watumishi wa umma katika Shule ya Sekondari Lumuma Green, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.


Mwonekano wa jengo la mradi wa makazi ya watumishi wa umma lililopo katika Shule ya Msingi Chaludewa, kijiji cha Mlunduzi, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.


Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Patrick Allute (wakwanza kulia) akisisitiza jambo kwa Mtakwimu Mwandamizi Bw. Ombeni Kasayo (wapili kutoka kushoto) na Mchumi Mwandamizi kutoka Watumishi Housing Investments, Bw. Damian Mnenwa (wakwanza kushoto) mara baada ya timu ya wataalam kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Wizara ya Fedha na WHI kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa makazi ya watumishi wa umma katika Kijiji cha Ludewa, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.