Na Mwandishi Wetu
Tarehe 06 Mei, 2024
Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Mhandisi Zena Ahmed Said amesisitiza Mameneja Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma Barani Afrika, Tawi la Tanzania kuwaheshimu watumishi wote wa umma hata kama ni wa kada ya chini kwa kuwa kila mmoja anamchango wake kwa ustawi wa taasisi na Taifa kwa jumla.
Mhandisi Zena ametoa kauli hiyo leo Mei 6, 2024 wakati wa kufungua Mkutano wa Mameneja Rasilimaliwatu
katika Utumishi wa Umma Barani Afrika, Tawi la Tanzania unaofanyika katika
Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).
“Tunahitaji kutoa heshima kwa kila mtu kwa kuwa kila
binadamu anastahili heshma, iwapo tutawadharau wahudumu wetu kwa kuona kuwa ni
kada ya chini tutajikuta tutakosa watu wa kutuhudumia, hivyo tutashindwa
kufanya kazi zetu za msingi”ameongeza Mhandisi Zena.
Aidha, Mhandisi Zena amewakumbusha Mameneja hao kutambua
kuwa, vyeo vya watumishi wa umma kwa kada zote ni muhimu sana na viliwekwa kwa
sababu maalum. Kwa mantiki hiyo, kila mtumishi kwa nafasi yake anatakiwa
kuheshimiwa kwa kuwa anamchango katika kuhakikisha dira ya taifa inafikiwa kwa
haraka na kwa ufanisi.
Vilevile, amewataka Mameneja hao kuwa wazalendo,
kutamani kuona maendeleo ya Taifa, kutotaja majina ya viongozi wakuu bila
sababu ya msingi kuwa wamepewa maelekezo kutoka juu, kuacha tabia ya kubeza kwa
namna yoyote ile siku na sherehe za kitaifa, isipokuwa wanatakiwa kuziheshimu
na kuzienzi kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
Awali, Rais wa Mtandao wa Mameneja Rasilimaliwatu
Barani Afrika ambaye pia ni Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Xavier Daudi, amesema kuwa mtandao huo unatumika
kama njia ya kuweka pamoja Mameneja Rasilimaliwatu Barani Afrika na kubadilishana
uzoefu wa namna ya kuboresha utendaji kazi katika nchi zao kwa lengo la kuleta
maendeleo ya haraka.
“Sasa hivi tunashuhudia matumizi makubwa ya Teknolojia
ya Habari na Mawasiliano -TEHAMA katika utendaji kazi, hivyo uwepo na ukuaji
huu wa teknolojia mathalani matumizi ya Akili Bandia (Artificial
Intelligence-AI) hatuna budi kama Bara la Afrika kuongeza jitihada za ukuaji wa
Mtandao huu ili nchi zote Barani Afrika ziweze kutumia teknolojia hizi kwa
maendeleo” amebainisha Bw. Daudi.
Aidha, ameongeza kuwa Mtandao utasaidia Bara la Afrika
kuwa na wataalamu wa rasilimaliwatu wenye sifa na ubora ili waweze kuzisaidia
nchi zao kujikwamua kiuchumi na kuleta maendeleo.
Pia, Bw. Daudi ametumia fursa ya mkutano huo
kuhamasisha watu kushiriki kwa wingi kwenye mkutano wa mwaka wa Bara la Afrika
ambao utafanyika mwezi Novemba, 2024 nchini Tanzania. Mkutano huo utatumika
kubadilisha uzoefu na zaidi kukuza na kuongeza uchumi wa Taifa.
Mkutano huo ulifanyika kwa siku moja umetumika kuzindua
rasmi Mtandao wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma Barani Afrika,
Tawi la Tanzania (TPS-HRMnet).
Mhe. Xavier Daudi, Rais wa APS HRMnet-Africa akiwa na
Viongozi mbalimbali kabla ya kumpokea Mgeni Rasmi ambaye ni Katibu
Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Eng. Zena
Ahmed Said kwa ajili ya kufungua
Mkutano wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma Barani Afrika, Tawi
la Tanzania-TPS HRMnet katika Kituo cha Mikutano cha
Kimataifa Arusha (AICC)AICC
leo tarehe 6
Mei, 2024.
Mhe. Xavier Daudi, Rais wa APS HRMnet-Africa akimpokea
Mgeni Rasmi ambaye ni Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu
wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar
Eng. Zena Ahmed Said katika Kituo cha Mikutano cha
Kimataifa Arusha kwa ajili ya
kufungua Mkutano wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma Barani
Afrika, Tawi la Tanzania-TPS HRMnet leo tarehe 6 Mei, 2024.
Katibu
Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Eng. Zena
Ahmed Said akiteta jambo na Mhe.
Xavier Daudi, Rais wa APS HRMnet-Africa ambaye pia ni Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi
ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora wakati wa kufungua Mkutano wa Mameneja
Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma Barani Afrika, Tawi la Tanzania leo
tarehe 6
Mei, 2024.
Mhe. Xavier Daudi, Rais wa APS HRMnet-Africa ambaye
pia ni Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora akitoa salaamu
za APSHRMnet -Afrika kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua Mkutano wa
Mameneja Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma Barani Afrika, Tawi la Tanzania
leo tarehe 6 Mei, 2024.
Katibu
Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Eng. Zena
Ahmed Said akihutubia washiriki
wa Mkutano wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma Barani Afrika,
Tawi la Tanzania unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha
Kimataifa Arusha (AICC) leo
tarehe 6
Mei, 2024.
No comments:
Post a Comment