Na.
James K. Mwanamyoto-Mtwara
Tarehe 29 Aprili, 2021
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amesema Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) ni taasisi muhimu ya kitaaluma yenye jukumu kubwa la kujenga maadili na uwezo wa kiutendaji kwa Watumishi wa Umma waliopo, wanaotarajiwa kuajiriwa na viongozi wateule wajao, hivyo watumishi wake wanapaswa kulinda hadhi ya chuo hicho kwa kufanya kazi kwa bidii, weledi na uadilifu ili kukiwezesha chuo hicho kufikia malengo yake.
Mhe. Ndejembi amesema
hayo, wakati wa ziara yake ya kikazi katika Chuo cha Utumishi wa Umma Kampasi
ya Mtwara yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa kampasi hiyo.
Mhe. Ndejembi
amefafanua kuwa, TPSC ndio chuo pekee kinachojitofautisha na vyuo vingine kwa
kutoa mafunzo yanayolenga kujenga maadili bora kwa Watumishi wa Umma waliopo,
wanaotarajiwa kuajiriwa ili kuutumikia umma, ikiwa ni pamoja na viongozi wa
umma wajao watakaoteuliwa na mamlaka.
Ameongeza kuwa,
Serikali ina dhamira ya kuhakikisha mhitimu kutoka chuo chochote cha ndani au
nje ya nchi pindi anapotaka kuingia katika Utumishi wa Umma itamlazimu kupitia TPSC
ili kufundishwa maadili na miiko ya Utumishi wa Umma kabla ya kuanza kutekeleza
majukumu yake.
Kwa upande wake,
Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Emmanuel
Shindika amesema Kampasi ya Mtwara inatoa mafunzo ya muda mfupi na mrefu, kutoa
shauri za kitaalam na kufanya tafiti zenye tija ambazo zinatumiwa kutatua
changamoto mbalimbali zinazolikabili taifa, hivyo ametoa wito kwa taasisi za
umma kuitumia kampasi hiyo kuwajengea uwezo kiutendaji watumishi wao.
Chuo cha Utumishi wa
Umma Kampasi ya Mtwara kilizinduliwa mwaka 2009 na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe.
Mizengo Pinda, ambaye alielekeza TPSC iongeze kampasi mikoani ili kutoa huduma
za mafunzo kwa Watumishi wa Umma waliopo na wanaotarajiwa kuajiriwa.
Naibu Waziri, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius
Ndejembi akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Kampasi ya Mtwara
wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi
wa kampasi hiyo.
Watumishi wa Chuo cha
Utumishi wa Umma Kampasi ya Mtwara wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo
pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo yenye lengo la kuhimiza
uwajibikaji kwa watumishi hao.
Mtendaji Mkuu na Mkuu
wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Emmanuel Shindika akitoa taarifa ya
utekelezaji ya TPSC Kampasi ya Mtwara kwa Mhe. Ndejembi wakati wa ziara ya
kikazi ya Naibu Waziri huyo yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa
Kampasi ya Mtwara.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Deogratius Ndejembi akiwasili katika Chuo cha Utumishi wa Umma Kampasi ya
Mtwara wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa
watumishi wa kampasi hiyo.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Deogratius Ndejembi akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Chuo cha
Utumishi wa Umma Kampasi ya Mtwara mara baada ya kuzungumza nao wakati wa ziara
yake ya kikazi yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa kampasi
hiyo.
No comments:
Post a Comment