KOMBANI AITISHA KIKAO NA WATENDAJI WA OFISI YAKE MJINI DODOMA
Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh. Celina O. Kombani (Mb) akiongea na
watendaji kutoka Ofisi ya Rais katika ukumbi wa Kituo cha Taifa cha
Kumbukumbu-Dodoma kabla ya kuwasilisha bajeti Bungeni siku ya Jumatatu, Mei
18/2015
Watendaji kutoka
Taasisi zilizo Ofisi ya Rais wakipitia maelezo ya Bajeti ya mwaka 2015/2016.
Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais-Ikulu Bw.Peter Alanambula Ilomo (wa kwanza kushoto), pamoja na watendaji
wengine wakiwa katika kikao cha matayarisho ya kuwasilisha bajeti Bungeni
wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh.
Celina O. Kombani (Mb) hayupo pichani.
Kaimu Katibu Mkuu,
Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. HAB Mkwizu akitoa maelekezo
katika kikao cha kujiandaa kuwasilisha Bajeti ya Ofisi ya Rais kilichofanyika
katika ukumbi wa Kituo cha Taifa cha Kumbukumbu - Dodoma.
No comments:
Post a Comment