Friday, January 29, 2016

Katibu Mkuu-Utumishi atembela Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA)

Katibu Mkuu-Utumishi Bw. Laurean Ndumbaro, wa pili kulia, akijiandaa kushiriki kikao kwa njia ya video na wajumbe kutoka Chuo cha Utumishi Kenya. Kushoto kabisa ni Mtendaji Mkuu wa TaGLA Bw. Charles Senkondo. 
Mkutano kwa njia ya video ukiendelea kati ya Katibu Mkuu Utumishi Bw. Laurean Ndumbaro na washiriki kutoka Chuo cha Utumishi Kenya (katika video).

Sehemu ya Maafisa Rasilimaliwatu wanaoshiriki mafunzo kuhusu Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara wakimsikiliza Katibu Mkuu Utumishi -Bw. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani)

Katibu Mkuu-Utumishi Bw. Laurean Ndumbaro (kulia) akiangalia moja ya chumba cha mafunzo

Monday, January 25, 2016

Serikali yafungua rasmi mafunzo ya ukusanyaji Taarifa za Tathmini ya Kazi

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma, Bibi Tamika Mwakahesya (kulia) akimkaribisha Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro (katikati) kufungua mafunzo kwa timu ya ukusanyaji taarifa za tathmini ya kazi kwenye ukumbi wa jengo la Maendeleo ya Jamii Dar es Salaam. 
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro (katikati) akifungua mafunzo kwa timu ya ukusanyaji taarifa za tathmini ya kazi (hawapo pichani) kwenye ukumbi wa jengo la Maendeleo ya Jamii Dar es Salaam. Kulia kwake ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma Bibi Tamika Mwakahesya na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu wa Maendeleo ya Jamii, Bwana James Kibamba. 

Timu ya washiriki wa ukusanyaji taarifa za tathmini ya kazi wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) alipokuwa akifungua mafunzo ya ukusanyaji taarifa za tathmini ya kazi kwenye ukumbi wa jengo la Maendeleo ya Jamii Dar es Salaam. 
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa ukusanyaji taarifa za tathmini ya kazi baada ya kufungua mafunzo kwa timu hiyo kwenye ukumbi wa jengo la Maendeleo ya Jamii Dar es Salaam mapema leo. Waliokaa kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma Bibi Tamika Mwakahesya na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu wa Maendeleo ya Jamii, Bwana James Kibamba. 

Thursday, January 21, 2016

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAZUNGUMZA NA MINIBUZZ TV KUHUSIANA NA MASUALA YA KIUTUMISHI

Mkurugenzi Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. Mick Kiliba (kulia) akisikiliza swali la Mwandishi wa Habari kutoka MiniBuzz Tv Bi. Hadija Mzee wakati wa mahojiano kuhusiana na masuala ya kiutumishi yaliyofanyika ofisini kwake 

Mkurugenzi Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. Mick Kiliba (kulia) akitoa ufafanuzi wa masuala ya kiutumishi kwa Mwandishi wa Habari kutoka MiniBuzz Tv Bi. Hadija Mzee wakati wa mahojiano yaliyofanyika ofisini kwake 

Mkurugenzi Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. Mick Kiliba (kushoto) akitoa ufafanuzi wa Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma kwa Mwandishi wa Habari kutoka MiniBuzz Tv Bi. Hadija Mzee wakati wa mahojiano yaliyofanyika ofisini kwake