Monday, September 10, 2018

SERIKALI YATOA VIBALI VYA KUAJIRI WATUMISHI WAPYA 15,000 KUZIBA PENGO LILILOACHWA NA WATUMISHI WALIOONDOLEWA KWA KUGHUSHI VYETI




Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akijibu swali Bungeni kuhusu kuziba nafasi wazi zilizoachwa na watumishi walioondolewa kazini kwa kosa la kughushi vyeti.

KATIBU MKUU-UTUMISHI AMWAGIZA MKUU WA CHUO CHA HOMBOLO KUWACHUKULIA HATUA ZA KINIDHAMU WATUMISHI WALIOSHIRIKI KULIPA MISHAHARA HEWA KWA ALIYEKUWA MTUMISHI WA CHUO HICHO



 Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dkt. Mpamila Madale alipofanya ziara ya kushtukiza katika chuo hicho jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Ibrahim Mahumi akitoa ufafanuzi kuhusu taratibu za kiutumishi kwa Mkuu wa Chuo na baadhi ya watumishi wa Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo (hawapo pichani) wakati wa ziara ya kikazi chuoni hapo.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akifuatilia maelezo ya Mkuu wa Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dkt. Mpamila Madale alipofanya ziara ya kushtukiza katika chuo hicho jijini Dodoma.




Saturday, September 1, 2018

WANASHERIA WALIO KATIKA UTUMISHI WA UMMA NCHINI WAASWA KUHAKIKISHA WANAANDAA MIKATABA YENYE MANUFAA KWA SERIKALI




Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Prof. Sifuni Mchome, akitoa neno la utangulizi na kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) kufunga mkutano wa siku mbili wa Wanasheria walio katika utumishi wa umma, uliofanyika katika Chuo cha Mipango jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akizungumza na Wanasheria walio katika Utumishi wa Umma (hawapo pichani) wakati akifunga mkutano wa siku mbili wa Wanasheria hao uliofanyika Chuo cha Mipango, jijini Dodoma.
Baadhi ya Wanasheria walio katika utumishi wa umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) (hayupo pichani) wakati akifunga mkutano wa siku mbili wa Wanasheria hao, uliofanyika katika Chuo cha Mipango jijini Dodoma.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Adelardus Kilangi, akitoa neno la shukrani baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) kufunga mkutano wa siku mbili wa Wanasheria walio katika utumishi wa umma, uliofanyika katika Chuo cha Mipango jijini Dodoma.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Adelardus Kilangi, akizungumza na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Dorothy Mwaluko mara baada ya kufungwa kwa mkutano wa siku mbili wa Wanasheria walio katika utumishi wa umma, uliofanyika katika Chuo cha Mipango jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akifafanua jambo kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Adelardus Kilangi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Prof. Sifuni Mchome mara baada ya kufunga mkutano wa siku mbili wa Wanasheria walio katika utumishi wa umma, uliofanyika katika Chuo cha Mipango jijini Dodoma.