Wednesday, August 3, 2016

MHE. KAIRUKI AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA BENKI YA DUNIA KUZUNGUMZIA MABORESHO KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kushoto) akifafanua jambo kuhusu maboresho katika Utumishi wa Umma alipokutana na ujumbe kutoka Benki ya Dunia (WB) kwenye ukumbi wa Ofisi ya Rais Utumishi leo mchana. Wa kwanza kulia ni Meneja Mtendaji wa Sekta ya Umma kutoka Benki hiyo, Bw. George Larhi na katikati ni Mkurugenzi wa Utumishi wa Umma na Taasisi wa WB.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (katikati) akizungumza na Ujumbe kutoka Benki ya Dunia kuhusu maboresho katika Utumishi wa Umma kwenye ukumbi wa Ofisi ya Rais Utumishi leo mchana.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kushoto) akimsikiliza Meneja Mtendaji wa Sekta ya Umma kutoka Benki ya Dunia (WB), Bw. George Larhi (wa kwanza kulia) wakati wa mazungumzo na ujumbe wa Benki hiyo kuhusu maboresho katika Utumishi wa Umma kwenye ukumbi wa Ofisi ya Rais Utumishi leo mchana. Katikati ni Mkurugenzi wa Utumishi wa Umma na Taasisi wa WB.

SERIKALI YAPOKEA WATAALAM WA KUJITOLEA KUTOKA JAPANI


Naibu Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais-Utumishi  na Utawala Bora Bi. Susan Mlawi akimkaribisha Mwakilishi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) nchini Tanzania Bw. Toshio Nagase baada ya kuwapokea Wataalam  sita wa kujitolea mapema leo kutoka shirika hilo ambao watafanya kazi katika maeneo mbalimbali nchini kwenye sekta za Elimu na Maendeleo ya Jamii.

Naibu Katibu Mkuu- Ofisi ya Rais - Utumishi na Utawala Bora Bi. Susan Mlawi, akizungumza na Wataalam wa kujitolea kutoka Japan mapema leo  ambao watafanya kazi  katika sekta za Elimu na Maendeleo ya Jamii, katika mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Pwani na Mtwara.

Mwakilishi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) nchini Tanzania Bw. Toshio Nagase (kulia) akimueleza jambo Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Utumishi na Utawala Bora Bi. Susan Mlawi,mapema leo  kuhusu Wataalam  wa kujitolea kutoka shirika hilo waliokuja nchini kutoa huduma katika sekta za Elimu na Maendeleo ya Jamii .

Tuesday, August 2, 2016

KIKAO KAZI KUHUSU UTOAJI HUDUMA NA MATUMIZI YA TEHAMA SERIKALINI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kulia) akimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro (aliyeinua mkono) alipokuwa akifafanua jambo wakati wa kikao kazi na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais- Utumishi kuhusu utoaji huduma na matumizi ya TEHAMA katika Utumishi wa Umma  kilichofanyika katika ukumbi wa utumishi leo, wa tatu kulia (mstari wa mbele) ni Naibu Katibu Mkuu Utumishi na Utawala Bora, Bi. Susan Mlawi.



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akielekeza jambo kwa baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais Utumishi wakati wa kikao kazi kuhusu utoaji huduma na matumizi ya TEHAMA kilichofanyika katika ukumbi wa utumishi leo. 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) na baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi wakijadili kuhusu matumizi ya TEHAMA katika utoaji huduma Serikalini wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa utumishi leo. 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akimsikiliza Mkurugenzi wa TEHAMA katika Utumishi wa Umma, Bw. Priscus Kiwango wakati wa kikao kazi kuhusu utoaji huduma na matumizi ya TEHAMA katika Utumishi wa Umma kilichofanyika katika ukumbi wa utumishi leo.