Monday, February 9, 2026

KIKWETE AWATAKA WAAJIRI NCHINI KUZINGATIA SHERIA NA KANUNI KATIKA USIMAMIZI WA RASILIMALIWATU

 Na. Antonia Mbwambo-Morogoro

Tarehe: 9 Februari, 2026

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete ameziagiza Mamlaka zote za nidhamu nchini ikiwa ni pamoja na Mamlaka za Maji kusimamia na kuzingatia ipasavyo Sheria, Kanuni na Taratibu katika usimamizi na uendeshaji wa masuala ya rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma ili kuiepushia Serikali hasara zisizo za lazima kwa baadhi ya michakato ya mashauri ya nidhamu kurudiwa.

Mhe. Kikwete alisema hayo wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha Tume ya Utumishi wa Umma na Mamlaka za Maji nchini kuhusu utekelezaji wa sheria ya utumishi wa umma sura 298 na matumizi ya mfumo wa kielektroni wa kushughulikia rufaa na malalamiko na uwasilishaji wa taarifa za kiutumishi Tume.

“Nitumie fursa hii kuwakumbusha kuwa haki iliyocheleweshwa ni sawa na haki iliyonyimwa kwa kuwa ukiukwaji wa Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma unachelewesha upatikanaji wa haki za Watumishi kwa wakati kutokana na mashauri hayo kurejeshwa na Tume ili kuanzishwa upya” alisema Mhe. Kikwete.

Katika hotuba yake, Mhe. Kikwete alibainisha kuwa jumla ya rufaa 52 kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2023/2024 na 2024/2025 zilizopokelewa kutoka Mamlaka za Maji na kutolewa uamuzi na Tume, ingawa rufaa 20 sawa na asilimia 38 ya rufaa zote zilizopokelewa katika kipindi hicho zilionekana kuwa na ukiukwaji wa sheria, kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma na kusababisha Tume kuzirudisha ili mchakato wa mashauri ya kinidhamu uanze upya.

Mhe. Kikwete alisisitiza kuwa asilimia hizo ni nyingi na aliipongeza Tume kwa kuandaa kikao kazi hicho chenye lengo la kutoa mafunzo ya namna bora ya kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi katika usimamizi na uendeshaji wa masuala ya rasilimaliwatu ili kuongeza ufanisi katika usimamizi na utoaji wa haki kwenye Utumishi wa Umma.

Tume ya Utumishi wa Umma ni chombo rekebu chini ya Ofisi ya Rais kilichoundwa ili kusimamia utoaji wa haki kwa kushughulikia rufaa na Malalamiko ya Watumishi wa Umma, kufanya ukaguzi, kutoa Miongozo na kutoa elimu kuhusu Sheria ya Utumishi wa Umma kwa Waajiri, Mamlaka za Ajira, Mamlaka za Nidhamu na Watumishi wa Umma ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Tume ya Utumishi wa Umma baada ya Waziri huyo kufungua kikao kazi cha mafunzo ya Tume ya Utumishi wa Umma kwa Mamlaka za Maji Tanzania cha Utekelezaji wa Sheria ya Utumishi wa Umma na Matumizi ya Mfumo wa kielektroniki wa kushughulikia Rufaa na uwasilishwaji wa taarifa za masuala ya kiutumishi leo tarehe 9 Februari, 2026


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika Ofisi za NSSF Mkoani Morogoro katika Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete WTM5

Washiriki wa kikao kazi cha mafunzo ya Tume ya Utumishi wa Umma kwa Mamlaka za Maji Tanzania cha Utekelezaji wa Sheria ya Utumishi wa Umma na Matumizi ya Mfumo wa kielektroniki wa kushughulikia Rufaa na uwasilishwaji wa taarifa za masuala ya kiutumishi wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati Waziri huyo alipokuwa akizungumza nao leo Mkoani Morogoro.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Utawala kutoka Mamlaka za Maji Tanzania baada ya Waziri huyo kufungua kikao kazi cha mafunzo ya Tume ya Utumishi wa Umma kwa Mamlaka za Maji Tanzania cha Utekelezaji wa Sheria ya Utumishi wa Umma na Matumizi ya Mfumo wa kielektroniki wa kushughulikia Rufaa na uwasilishwaji wa taarifa za masuala ya kiutumishi leo tarehe 9 Februari, 2026

 

 

Kaimu Katibu, Ofisi ya Rais, Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. John Mbisso akitoa neno la Utangulizi kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete baada ya Waziri huyo kuwasili katika ukumbi wa NSSF Mkoani Morogoro katika kikao kazi cha mafunzo ya Tume ya Utumishi wa Umma kwa Mamlaka za Maji Tanzania cha Utekelezaji wa Sheria ya Utumishi wa Umma na Matumizi ya Mfumo wa kielektroniki wa kushughulikia Rufaa na uwasilishwaji wa taarifa za masuala ya kiutumishi leo tarehe 9 Februari, 2026.

Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu na Utawala Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (AUWSA) Bw. Kazimil Kanyanza akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete baada ya Waziri huyo kufungua kikao kazi cha mafunzo ya Tume ya Utumishi wa Umma kwa Mamlaka za Maji Tanzania cha Utekelezaji wa Sheria ya Utumishi wa Umma na Matumizi ya Mfumo wa kielektroniki wa kushughulikia Rufaa na uwasilishwaji wa taarifa za masuala ya kiutumishi  kilichofanyika katika ukumbi wa NSSF Mkoani Morogoro leo tarehe 9 February, 2026.

SERIKALI KUCHUKUA HATUA ZA KINIDHAMU KWA WAAJIRI WOTE WASIOZINGATIA SHERIA

 Na. Antonia Mbwambo-Morogoro

Tarehe: 9 Februari, 2026

“Ninatoa rai kwa kwa Waajiri wote, Mamlaka za ajira na Mamlaka za nidhamu kuwasilisha vielelezo vya rufaa na malalamiko Tume ya Utumishi wa Umma kwa wakati kama Sheria inavyoelekeza vingenevyo Serikali haitasita kuchukua hatua za kinidhamu dhidi yao.

Rai hiyo imetolelewa leo tarehe 9 Februari, 2026 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha Tume ya Utumishi wa Umma na Mamlaka za Maji nchini kuhusu utekelezaji wa sheria ya utumishi wa umma Sura 298 na matumizi ya mfumo wa kielektroni wa kushughulikia rufaa na malalamiko na uwasilishaji wa taarifa za kiutumishi Tume.

Mhe. Kikwete alisema kuwa Waajiri, Mamlaka za Ajira na Mamlaka za Nidhamu katika Utumishi wa Umma zinaweza kuwasilisha vielelezo vya rufaa na malalamiko ya watumishi wao Tume kupitia Mfumo wa Kielektroni wa Kushughulikia Rufaa na Malalamiko katika Utumishi wa Umma na Uwasilishaji wa Taarifa za Kiutumishi (PSCMIS).

Ninafahamu kuwa wapo Waajiri, Mamlaka za Ajira na Mamlaka za Nidhamu ambazo hazitekelezi wajibu wao ipasavyo hasa Tume inapowaelekeza kuwasilisha vielelezo vya rufaa na malalamiko, jambo hili limekuwa likisababisha watumishi wa Umma kukaa muda mrefu bila kupata haki zao na Serikali Kupata hasara” alisema Mhe. Kikwete.

Aliongeza kuwa, muda wa kuwasilisha vielelezo hivyo unapopita, Tume hulazimika kuamua rufaa hizo kwa kutumia vielelezo vya upande mmoja kwa kuzingatia sheria, jambo hili siyo sawa kwa kuwa Mamlaka haziwatendei haki Warufani na Walalamikaji pamoja na Serikali iliyowaamini na kuwapa dhamana ya kusimamia Utumishi wa Umma.

Kwa kuzingatia utawala bora unaoshamilishwa na uwepo wa mifumo ya TEHAMA, Warufani wataweza kufuatilia, kufahamu hali ya rufaa na malalamiko yao yamefikia hatua gani kwa urahisi.

Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala tumepewa dhamana ya kuhakikisha dhamira ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kujenga Utumishi wa Umma wenye uadilifu na unaowajibika kwa wananchi kwa kutoa huduma bora inatimia kupitia Tume ya Utumishi wa Umma" Mhe. Kikwete alisisitiza.

Vile vile, aliwashukuru Wanahabari kwa kuhabarisha umma kuhusu jitihada zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuijenga Tanzania hasa katika kuboresha haki za Watumishi wa Umma na kuimarisha Utawala Bora.

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete, akizungumza na Maafisa Utawala na Maafisa Sheria (hawapo pichani) wakati akifungua kikao kazi cha mafunzo ya Tume ya Utumishi wa Umma kwa Mamlaka za Maji Tanzania cha Utekelezaji wa Sheria ya Utumishi wa Umma na Matumizi ya Mfumo wa kielektroniki wa kushughulikia Rufaa na uwasilishwaji wa taarifa za masuala ya kiutumishi kilichofanyika katika ukumbi wa NSSF Mkoani Morogoro leo tarehe 9 February, 2026.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika Ofisi za NSSF Mkoani Morogoro katika Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete WTM5


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete (kushoto) akiteta jambo na Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma Mhe. Hamisa Kalombola, wakati wa kikao kazi cha mafunzo ya Tume ya Utumishi wa Umma  kwa Mamlaka za Maji Tanzania cha Utekelezaji wa Sheria ya Utumishi wa Umma na Matumizi ya Mfumo wa kielektroniki wa kushughulikia Rufaa na uwasilishwaji wa taarifa za masuala ya kiutumishi leo tarehe 9 Februari, 2026


Viongozi wa Tume ya Utumishi wa Umma wakimsubiri Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete kuwasili katika katika kikao kazi cha mafunzo ya Tume ya Utumishi wa Umma  kwa Mamlaka za Maji Tanzania cha Utekelezaji wa Sheria ya Utumishi wa Umma na Matumizi ya Mfumo wa kielektroniki wa kushughulikia Rufaa na uwasilishwaji wa taarifa za masuala ya kiutumishi leo tarehe 9 Februari, 2026

     

Washiriki wa kikao kazi cha mafunzo ya Tume ya Utumishi wa Umma kwa Mamlaka za Maji Tanzania cha Utekelezaji wa Sheria ya Utumishi wa Umma na Matumizi ya Mfumo wa kielektroniki wa kushughulikia Rufaa na uwasilishwaji wa taarifa za masuala ya kiutumishi wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati Waziri huyo alipokuwa akizungumza nao leo Mkoani Morogoro.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Tume ya Utumishi wa Umma baada ya Waziri huyo kufungua kikao kazi cha mafunzo ya Tume ya Utumishi wa Umma kwa Mamlaka za Maji Tanzania cha Utekelezaji wa Sheria ya Utumishi wa Umma na Matumizi ya Mfumo wa kielektroniki wa kushughulikia Rufaa na uwasilishwaji wa taarifa za masuala ya kiutumishi leo tarehe 9 Februari, 2026


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Sekretarieti ya Tume ya Utumishi wa Umma baada ya Waziri huyo kufungua kikao kazi cha mafunzo ya Tume ya Utumishi wa Umma kwa Mamlaka za Maji Tanzania cha Utekelezaji wa Sheria ya Utumishi wa Umma na Matumizi ya Mfumo wa kielektroniki wa kushughulikia Rufaa na uwasilishwaji wa taarifa za masuala ya kiutumishi leo tarehe 9 Februari, 2026