Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amesema Serikali imeendelea kutoa vibali vya ajira ili kuondokana na adha ya uhaba wa watumishi kufuatia kasi ya ujenzi wa miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali nchini ikiwemo ya afya na elimu.
Mhe. Simbachawene amesema hayo leo wakati
wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo na
kusikiliza changamoto za wananchi katika Mkoa wa Mara ikiwa ni utekelezaji wa
Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
“Katika
sekta ya afya, mchakato wa ajira umefanyika kwenye mikoa yote, waombaji
wameomba na katika Mkoa wa Mara kama ilivyo katika mikoa mingine, Katibu Tawala
wa Mkoa na wasaidizi wake wamesimamia zoezi hilo na watumishi hao wamepatikana
hivyo, wanakuja wa kutosha, Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amemaliza kazi
yake,” Mhe. Simbachawene ameongeza.
Ameongeza
kuwa, katika sekta ya elimu kama ilivyokuwa kwenye afya, mchakato wa ajira utaanza
tena ambapo waombaji wataomba tena kupitia kwenye mikoa na huko ndiko watawapangia
wenyewe sehemu yenye upungufu na sio tena Ofisi ya Rais-UTUMISHI au Ofisi ya
Rais-TAMISEMI kama ilivyokuwa awali.
Mhe.
Simbachawene amewasisitiza Viongozi wa mkoa huo kutoa taarifa za upungufu wa
watumishi kwa kuwa mahitaji ya watumishi yanapangwa kutokana na maombi ya mkoa
husika.
“Katibu
Tawala wa Mkoa, kwenye upungufu wa watumishi tusaidiane kupeana taarifa na kwa
wale ambao hawatapatikana kupitia mchakato wa ajira mpya katika mkoa wenu, basi
tutafanya uhamisho kwasababu kasi ya maendeleo ni kubwa sana hivyo suala la upungufu
wa watumishi ni lazima lipewe kipaumbele.
Aidha,
Mhe. Simbachawene ametoa wito kwa watumishi wa umma kuhakikisha utoaji wa
huduma bora kwa wananchi unakuwa ndio kipaumbele.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene
akizungumza na wananchi wa Halmashauri
ya Wilaya Musoma mara baada ya kutoka kuweka jiwe la msingi katika Hospitali
ya Halmashauri ya Wilaya Musoma wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga
kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Mara.
Baadhi ya Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya Musoma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) wakati akizungumza nao mara baada ya kutoka kuweka jiwe la msingi katika Hospitali ya Wilaya ya Musoma wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Mara.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akifurahia jambo mara baada ya
kuzindua Hospitali
ya Halmashauri ya Wilaya Musoma ambayo imewekwa jiwe la
msingi na Waziri huyo wakati wa ziara yake
ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya
maendeleo mkoani Mara.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akielekea kukagua majengo ya
Hospitali ya Halmashauri
ya Wilaya Musoma wakati wa ziara ya
kikazi ya Waziri huyo iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali
ya maendeleo mkoani Mara.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa
Mkoa wa Mara, Kanali Evance Mtambi wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo iliyolenga kukagua
na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Mara.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene
akisisitiza jambo baada ya kukagua mashine ya x-ray wakati wa ziara yake
ya kikazi katika mkoa wa Mara iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa
miradi mbalimbali ya maendeleo.
Mwonekano wa mashine ya x-ray iliyopo katika Hospitali
ya Halmashauri ya Wilaya Musoma mkoani Mara.
Mwonekano wa kitanda
cha mgonjwa na mashine za kupima afya zilizopo katika Hospitali
ya Halmashauri ya Wilaya Musoma mkoani Mara.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akisalimiana na Viongozi wa Mkoa wa
Mara baada ya kuwasili mkoani humo kwa lengo la kufanya ziara ya kikazi ya kukagua
na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na kuzungumza na
wananchi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akitazama nyaraka za mwananchi wa Halmashauri ya Wilaya
Musoma aliyewasilisha
changamoto yake wakati wa ziara ya
kikazi ya kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na kuzungumza
na wananchi.