Na. James Mwanamyoto-Dodoma
Tarehe 5 Oktoba, 2020.
Gazeti la Serikali lilianzishwa kwa lengo la kuchapisha na kuhifadhi taarifa muhimu zinazotumika kama marejeo katika kutatua migogoro mbalimbali na kufanya maamuzi muhimu yakiwemo ya kisheria.
Msaidizi wa Maktaba
Mwandamizi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Bi. Beatrice Mganga ameainisha baadhi ya migogoro inayotatuliwa kupitia Gazeti
la Serikali kuwa, ni ya umiliki wa ardhi, mirathi na mali isiyo na mwenyewe.
Akizungumzia lengo la uanzishwaji
wa gazeti hilo, amesema, matangazo ya Gazeti la Serikali huwa rasmi kiutendaji
na kwa utekelezaji wa majukumu mbalimbali hapa nchini.
Naye, Mkutubi wa Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Halima Rauna
amefafanua kuwa, Gazeti la Serikali ni kielelezo muhimu cha taarifa za
Serikali, taasisi binafsi, wananchi na wadau mbalimbali zinazotumika katika utendaji
wa kila siku.
Gazeti la Serikali lilianzishwa
kwa mujibu wa “General Orders”
kifungu C.56- C.62 ya mwaka 1957, pamoja na marekebisho yake kwenye Kanuni za
Kudumu katika Utumishi wa Umma Kifungu C.28-C.30 toleo la mwaka 1971, kifungu
C.28-C.31 toleo la mwaka 1994 na Kifungu C.27-C.30 toleo la mwaka 2009.
Kutokana na umuhimu wa
Gazeti hili, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na utawala Bora,
inazihimiza Taasisi za Umma na wananchi kuwasilisha taarifa zinazopaswa
kuchapishwa katika Gazeti la Serikali ili ziweze kutumika kutatua migogoro
katika jamii na kuiwezesha Mahakama kufanya maamuzi ya kisheria.
Muonekano wa mbele wa Gazeti la Serikali la tarehe 24
Januari, 2020 Toleo Namba 4.
No comments:
Post a Comment