Tuesday, October 20, 2020

SERIKALI YAMKABIDHI NYUMBA RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA PILI, MHE. ALHAJ ALI HASSAN MWINYI IKIWA NI UTEKELEZAJI WA MATAKWA YA KISHERIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akikata utepe kufungua nyumba ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Mhe. Alhaj Ali Hassan Mwinyi aliyojengewa na Serikali eneo la Masaki jijini Dar es Salaam ikiwa ni utekelezaji wa matakwa ya kisheria.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipokea mfano wa funguo kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais. Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro ili kumkabidhi rasmi nyumba Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Mhe. Alhaj Ali Hassan Mwinyi aliyojengewa na Serikali eneo la Masaki jijini Dar es Salaam ikiwa ni utekelezaji wa matakwa ya kisheria.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimkabidhi mfano wa funguo Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Mhe. Alhaj Ali Hassan Mwinyi na mkewe Mama Sitti Mwinyi katika hafla ndogo ya kumkabidhi nyumba hiyo eneo la Masaki jijini Dar es Salaam, nyumba hiyo imejengwa na Serikali ikiwa ni utekelezaji wa matakwa ya kisheria. Kulia ni Mama Janet Magufuli.



 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimsikiliza Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Mhe. Alhaj Ali Hassan Mwinyi wakati akitoa shukurani kwa Serikali baada ya kumkabidhi nyumba ambayo serikali imemjengea Rais huyo Mstaafu eneo la Masaki jijini Dar es Salaam ikiwa ni utekelezaji wa matakwa ya kisheria.

 

No comments:

Post a Comment