Saturday, March 21, 2020

WATUMISHI HOUSING COMPANY IMESHAURIWA KUTENGA NYUMBA ZA KUWAUZIA NA KUPANGISHA WADAU WA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII






Naibu Waziri ,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa akikagua nyumba zilizojengwa na Watumishi Housing Company eneo la Gezaulole jijini Dar es Salaam.Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Company Dkt. Fred Msemwa.

Mkurugenzi wa Watumishi Housing Company, Dkt. Fred Msemwa akitoa maelezo kuhusu mradi wa nyumba za kampuni hiyo kwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi ujenzi wa nyumba eneo la Gezaulole jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary akitoa ushauri juu ya upangishaji na uuzaji wa nyumba kwa watendaji wa Watumishi Housing Company katika mojawapo ya nyumba alizozikagua eneo la Gezaulole  - Kigamboni jijini Dar Es salaam.

Baadhi ya Nyumba za ghorofa za Mradi wa Watumishi Housing Company zilizojengwa kwa madhumuni ya kuuzwa kwa Watumishi wa Umma na kupangishwa zilizopo katika eneo la  Gezaulole Kigamboni nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.

Wednesday, March 18, 2020

UTUMISHI YAPOKEA VITENDEA KAZI TOKA UNDP KUBORESHA UTENDAJI


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (kulia) akimpongeza Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimaliwatu, Mkoa wa Shinyanga, Bw. James Bwana kwa kuwezesha kupatikana kwa vitendea kazi vya kielektroniki toka Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Umoja wa Mataifa (UNDP) mara baada ya Katibu Tawala huyo kukabidhi vitendea kazi hivyo katika ukumbi wa Ofisi ya Rais, Utumishi, Mtumba jijini Dodoma. 


Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimaliwatu, Mkoa wa Shinyanga, Bw. James Bwana akitoa maelezo ya vitendea kazi vilivyotolewa na UNDP kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (kulia) katika ukumbi wa Ofisi ya Rais, Utumishi, Mtumba jijini Dodoma.

Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimaliwatu, Mkoa wa Shinyanga, Bw. James Bwana, akionyesha nyaraka zenye orodha ya vitendea kazi vilivyotolewa na UNDP kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (kulia).

Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi, Ofisi ya Rais, Utumishi, Bw. Victor Ngole, akipokea nyaraka leo toka kwa Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimaliwatu, Mkoa wa Shinyanga, Bw. James Bwana zinazoonyesha orodha ya vitendea kazi vilivyotolewa na UNDP. Anayeshuhudia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro. 

Vitendea kazi vya kielektroniki vilivyotolewa na UNDP kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi wa watumishi wa watumishi wa Ofisi ya Rais, Utumishi vikishushwa leo kwa ajili ya makabidhiano rasmi katika ofisi hiyo, Mtumba jijini Dodoma. 

Sunday, March 15, 2020

UTUMISHI YAFANYA KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI KUJADILI TAARIFA YA MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA BAJETI WA MWAKA 2019/20 NA MPANGO WA BAJETI KWA MWAKA 2020/21

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (katikati) akiongoza kikao cha Baraza la Wafanyakazi kujadili taarifa ya Mapitio ya Utekelezaji wa Mpango wa Bajeti wa Mwaka 2019/20 na Mpango wa Bajeti kwa Mwaka 2020/21 kilichofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma.

Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) wakati akiongoza kikao hicho kujadili taarifa ya Mapitio ya Utekelezaji wa Mpango wa Bajeti wa Mwaka 2019/20 na Mpango wa Bajeti kwa Mwaka 2020/21 kilichofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Cosmas Ngangaji (aliyesimama) akiwasilisha taarifa ya Mapitio ya Utekelezaji wa Mpango wa Bajeti wa Mwaka 2019/20 na Mpango wa Bajeti kwa Mwaka 2020/21 kwenye Kikao cha Baraza la Wafanyakazi la ofisi hiyo kilichofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (katikati) akitoa ufafanuzi wa masuala ya kiutumishi katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi cha kujadili taarifa ya Mapitio ya Utekelezaji wa Mpango wa Bajeti wa Mwaka 2019/20 na Mpango wa Bajeti kwa Mwaka 2020/21 kilichofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma.

RUZUKU YA TASAF YAMUWEZESHA ALBINA KUENDESHA MRADI WA KOKOTO NA KUBORESHA MAISHA YAKE MJINI BABATI

Mnufaika wa Ruzuku inayotolewa na Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF), Bibi Albina Matayo, mkazi wa Halmashauri ya Mji wa Babati, Mtaa wa Mrara, akitoa ushuhuda jana kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wa namna TASAF ilivyomuwezesha kuboresha maisha yake.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Dkt. Jasson Rweikiza (Mb), akieleza kuridhishwa na maendeleo ya Mnufaika wa (TASAF), Bibi Albina Matayo, mkazi wa Halmashauri ya Mji wa Babati.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe. George Mkuchika (Mb) akishuhudia kokoto zilizopondwa kwa ajili ya kuuzwa na Bibi Albina Matayo ambaye ni Mnufaika wa Ruzuku inayotolewa na Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF), Halmashauri ya Mji wa Babati.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe. George Mkuchika (Mb) akiwa katika picha na mnufaika wa TASAF, Halmashauri ya Mji wa Babati, Bibi Albina Matayo mbele ya nyumba iliyojengwa na mnufaika huyo kupitia Ruzuku inayotolewa na Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF).

Mbuzi wanaofugwa na Bibi Albina Matayo, mkazi wa Halmashauri ya Mji wa Babati, Mtaa wa Mrara ambaye ni mnufaika wa Ruzuku inayotolewa na Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF), ambayo imemuwezesha kuwanunua mbuzi hao.


Saturday, March 14, 2020

KAMATI YA BUNGE YAIPONGEZA MKURABITA KWA KURAHISISHA MCHAKATO WA URASIMISHAJI WA BIASHARA KATIKA MANISPAA YA SINGIDA



Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Dkt. Jasson Rweikiza (Mb), akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Biashara wa Manispaa ya Singida, Bw. Erick Simkwembe ya namna Kituo cha Pamoja cha Urasimishaji na Uendelezaji Biashara, Manispaa ya Singida kinavyofanya kazi.

Baadhi ya Wafanyabiashara wanaofaidika na uwepo wa Kituo cha Pamoja cha Urasimishaji na Uendelezaji Biashara, Manispaa ya Singida, wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Dkt. Jasson Rweikiza (Mb) (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao leo wakati wa ziara ya kamati yake mkoani humo yenye lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya Serikali mkoani Singida.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe. George Mkuchika (Mb) akitoa maelezo kuhusu utekelezaji wa MKURABITA kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakati wa ziara ya kamati hiyo mkoani Singida yenye lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya Serikali mkoani Singida.

Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Biashara na Rasilimali za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), Dkt. Seraphia Mgembe akitoa ufafanuzi kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wa namna MKURABITA ilivyoshiki katika uanzishwaji wa Kituo cha Pamoja cha Urasimishaji na Uendelezaji Biashara, Manispaa ya Singida wakati wa ziara ya kamati hiyo mkoani Singida yenye lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya Serikali mkoani humo.

Mfanyabiashara wa Manispaa ya Singida, Bi. Happy Francis akitoa maelezo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhusiana na bidhaa anazozalisha wakati wa ziara ya kamati hiyo mkoani Singida yenye lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya Serikali mkoani humo.

SERIKALI YAKANUSHA UVUMI WA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA KAMPASI YA SINGIDA KUHAMISHIWA DODOMA


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Dkt. Jasson Rweikiza (Mb), akitazama ramani ya kiwanja cha Mungumaji ambacho Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Singida kinatarajiwa kujengwa wakati wa ziara ya kamati hiyo ya kukagua kiwanja hicho iliyofanyika jana.

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, wakisikiliza maelezo ya mpango wa ujenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Singida kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma na Mtendaji Mkuu wa Taasisi, Dkt. Selemani Shindika,  wakati wa ziara ya kamati hiyo ya kukagua kiwanja hicho iliyofanyika jana.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe. George Mkuchika (Mb) akifafanua kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, uvumi ulioenea wa Serikali kukihamishia Dodoma Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Singida wakati wa ziara ya kamati hiyo iliyofanyika jana ya kukagua kiwanja cha Mungumaji ambacho Kampasi ya Singida inatarajiwa kujengwa.

Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Emmanuel Selemani Shindika akitoa ufafanuzi kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, kuhusu kiwanja kilichonunuliwa kwa ajili ya Ujenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Singida wakati wa ziara ya kamati hiyo iliyofanyika jana.

Friday, March 13, 2020

KAULI MBIU YA “HAPA KAZI TU” YAWA CHACHU YA MAENDELEO KWA MNUFAIKA WA TASAF MKOANI SINGIDA


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Dkt. Jasson Rweikiza (Mb), akizungumza na mnufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF), Bibi Edith Brayson Makala jana ambaye anafanya shughuli za ushonaji wakati wa ziara ya kamati hiyo yenye lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya Serikali mkoani Singida.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Dkt. Jasson Rweikiza (Mb), akishuhudia moja na bidhaa iliyotengenezwa na mnufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF), Bibi Edith Brayson Makala wakati wa ziara ya kamati hiyo jana yenye lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya Serikali mkoani Singida.



Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Dkt. Jasson Rweikiza (Mb), akizungumza na baadhi ya wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF), Mtaa wa Sokoine, Kata ya Misuna, Manispaa ya Singida wakati wa ziara ya kamati hiyo jana yenye lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya Serikali mkoani Singida.

Baadhi ya wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF), Mtaa wa Sokoine, Kata ya Misuna, Manispaa ya Singida wakimsikilza Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Dkt. Jasson Rweikiza (Mb), (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao jana wakati wa ziara ya kamati hiyo yenye lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya Serikali mkoani Singida.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe. George Mkuchika (Mb) akizungumza na baadhi ya wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF), Mtaa wa Sokoine, Kata ya Misuna, Manispaa ya Singida (hawapo pichani) wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa jana yenye lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya Serikali mkoani Singida.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF), Bw. Ladislaus Mwamanga akiwasalimia wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF), Mtaa wa Sokoine, Kata ya Misuna, Manispaa ya Singida (hawapo pichani) wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa jana yenye lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya Serikali mkoani Singida.


Tuesday, March 10, 2020

SERIKALI YAFANYA MAPITIO YA RASIMU YA MUONGOZO WA KUANDAA MPANGO WA RASILIMALIWATU KATIKA UTUMISHI WA UMMA


Mkurugenzi wa Uendelezaji Sera Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Agnes Meena akifungua kikao kazi cha wadau cha kupitia Rasimu ya Mwongozo wa kuandaa Mpango wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro katika ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa Dodoma.

Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango ya Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Edith Rwiza akitoa maelezo ya awali kwa wadau juu ya umuhimu na faida za kupitia Rasimu ya Mwongozo wa kuandaa Mpango wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma katika ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa Dodoma.
Mkurugenzi wa Sera Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Agnes Meena (wa tatu kushoto mstari wa mbele) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa kikao kazi cha kupitia Rasimu ya Mwongozo wa kuandaa Mpango wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma.

Baadhi ya wadau walioshiriki kikao kazi cha kupitia rasimu ya Mwongozo wa kuandaa mpango wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma wakimsilikiza Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango ya Rasilimaliwatu, Dkt, Edith Rwiza (hayupo pichani).



Thursday, March 5, 2020

TASAF YABORESHA MAISHA YA BIBI WA MIAKA 90 CHUNYA


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na Mnufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Bibi Rozena Bilia Mwambogo alipomtembelea mnufaika huyo kijiji cha Mapogoro wilayani Chunya wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo yenye lengo la kukagua utekelezaji wa mpango wa TASAF mkoani Mbeya.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Mnufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, Bibi Rozena Bilia Mwambogo wakielekea kushuhudia banda la nguruwe wanaofugwa na mnufaika huyo kutokana na ruzuku ya TASAF.

Banda la Nguruwe wanaofugwa na Bibi Rozena Mwambogo ambao amewanunua kupia ruzuku ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF).

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na mgonjwa, Mzee Gidison Mwayiyi ambae anauguzwa na mnufaika wa TASAF Bibi Rozena Mwambogo alipomtembelea mnufaika huyo katika kijiji cha Mapogoro wilayani Chunya wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo yenye lengo la kukagua utekelezaji wa mpango wa TASAF mkoani Mbeya.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akimfariji mgonjwa, Mzee Gidison Mwayiyi ambae anauguzwa na mnufaika wa TASAF Bibi Rozena Mwambogo alipomtembelea mnufaika huyo katika kijiji cha Mapogoro wilayani Chunya.