Friday, June 21, 2019

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA KWA KUFANYA USAFI WA MAZINGIRA


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza na watumishi wa ofisi yake mara baada ya watumishi hao kukamilisha zoezi la usafi wa mazingira eneo la Mtumba jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2019. 

Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Maadili,  Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Fabian Pokela akimwagilia maji moja ya mti uliopandwa  katika Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora eneo la Mtumba jijini Dodoma  ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2019. 

Baadhi ya watumishi  wa  Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakifanya usafi katika ofisi yao iliyopo Mji wa Serikali, eneo la Mtumba jijini Dodoma  ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2019.

No comments:

Post a Comment