Wednesday, June 19, 2019

SERIKALI HAITOSITA KUMCHUKULIA HATUA MTU YEYOTE ATAKAYEJIHUSISHA NA MASUALA YA RUSHWA



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe. George Mkuchika (Mb), akifungua mjadala kuhusu Kuelekea Msimamo wa Pamoja wa Afrika kuhusu Urejeshwaji Mali wakati wa Kongamano la Siku Maalum ya Mapambano Dhidi ya Rushwa Barani Afrika iliyoadhimishwa kitaifa jijini Dodoma.

Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Siku Maalum ya Mapambano Dhidi ya Rushwa Barani Afrika, wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe. George Mkuchika (Mb), alipokuwa akifungua mjadala kuhusu Kuelekea Msimamo wa Pamoja wa Afrika kuhusu Urejeshwaji Mali wakati wa kongamano hilo jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Kamishna wa Polisi, Diwani Athumani akitoa maelezo ya awali kuhusu Siku Maalumu ya Mapambano Dhidi ya Rushwa Barani Afrika wakati wa Kongamano la siku hiyo iliyoadhimishwa kitaifa jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe. George Mkuchika (Mb) akimkabidhi mwongozo wa utendaji kazi mmoja wa wajumbe wa kamati ya uadilifu ya Chuo Kikuu cha Dodoma wakati wa Kongamano la Siku Maalum ya Mapambano Dhidi ya Rushwa Barani Afrika iliyoadhimishwa kitaifa jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe. George Mkuchika (Mb) akipokea hati ya utambuzi wa mchango wake katika mapambano dhidi ya rushwa toka kwa viongozi wa Klabu ya Wapinga Rushwa ya Chuo Kikuu cha Dodoma, wakati wa Kongamano la Siku Maalum ya Mapambano Dhidi ya Rushwa Barani Afrika iliyoadhimishwa kitaifa jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment