Tuesday, July 24, 2018

WATUMISHI WAASWA KUFANYA KAZI KWA BIDII NA UADILIFU



Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bi. Dorothy Mwaluko akizungumza wakati wa hafla fupi ya kumuaga aliyekuwa Mkurugenzi wa Sera, Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mathias Kabunduguru ambaye kwa sasa ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. 

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. Mathias Kabunduguru, ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Sera, Ofisi ya Rais-Utumishi  akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Utumishi.

Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. Mathias Kabunduguru, (hayupo pichani) ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Sera, Ofisi ya Rais-Utumishi wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Utumishi.

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. Mathias Kabunduguru, ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Sera, Ofisi ya Rais-Utumishi  akimkabidhi nyaraka za kiutendaji Kaimu Mkurugenzi wa Sera, Bi Agnes Meena wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Utumishi.

Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bi. Dorothy Mwaluko pamoja na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. Mathias Kabunduguru wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi baada ya hafla fupi ya kumuaga Bw. Mathias Kabunduguru ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Sera Ofisi ya Rais-Utumishi.

No comments:

Post a Comment