Wednesday, September 27, 2017

JICA YAPONGEZWA KWA KUDUMISHA USHIRIKIANO NA TANZANIA

Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya Ushiririkiano wa Kimataifa kutoka Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Naibu Balozi Msafiri Marwa akimkabidhi zawadi kijana wa Kijapani aliyemaliza muda wa kujitolea hapa nchini, Bw. Yusuke Sakakibara katika hafla fupi ya kuwaaga wataalam wa kujitolea kutoka Japan iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa vijana wa kujitolea kutoka Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) nchini Tanzania, Bw. Ichiro Owa (kushoto) akielezea jambo wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wataalam wa kujitolea waliomaliza muda wao wa kujitolea hapa nchini kutoka Japan iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni mmoja wa waliokuwa wakijitolea Kyoko Tada.

Baadhi ya wataalam wa kijapani waliomaliza muda wa kujitolea nchini wakiwa katika hafla ya kuwaaga baada ya kumaliza muda wao.

No comments:

Post a Comment