Monday, March 2, 2020

TANZANIA BILA RUSHWA INAWEZEKANA


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mkakati wa Kitaifa wa Kushirikisha Vijana wa Scout katika mapambano dhidi ya rushwa nchini iliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Sayansi ya Kompyuta, Habari na Mawasiliano uliopo Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) jijini Dodoma.
Baadhi ya vijana wa Skauti Taifa wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst.), Mhe. George H. Mkuchika (Mb)(hayupo pichani) alipokuwa akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mkakati wa Kitaifa wa Kushirikisha Vijana wa Skauti katika mapambano dhidi ya rushwa nchini iliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Sayansi ya Kompyuta, Habari na Mawasiliano uliopo Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)  jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst.), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akizindua Mkakati wa Kitaifa wa Kushirikisha Vijana wa Skauti katika mapambano dhidi ya rushwa nchini katika ukumbi wa Chuo cha Sayansi ya Kompyuta, Habari na Mawasiliano uliopo Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)  jijini Dodoma. Wanaoshuhudia ni Rais Mstaafu na Mdhamini wa Chama cha Skauti Tanzania, Mhe. Ali Hassan Mwinyi (kulia), Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia na Rais wa Chama cha Skauti Tanzania, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (Mb) (wa pili kutoka kushoto) na Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Justine Mahiga (MB)(kushoto).

Monday, February 17, 2020

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AZINDUA KIPINDI CHA PILI CHA AWAMU YA TATU YA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika akitoa maelezo ya awali kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kabla ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kuzindua Kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu ya Mpango huo jijini Dar es Salaam leo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimwangalia Msanii wa Muziki, Mrisho Mpoto alipokuwa akitumbuiza kwenye sherehe za uzinduzi wa Kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini jijini Dar es Salaam leo. Wengine katika picha ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Mohammed Aboud Mohammed na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Ikulu na Mwenyekiti wa TASAF Dkt. Moses Kusiluka

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa na Marais Wastaafu wa Awamu ya Pili, Tatu na Nne wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania wakionyesha Mpango wa Utekelezaji wa TASAF baada ya Rais Magufuli kuzindua Kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini jijini Dar es Salaam leo. Wengine katika picha ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Mohammed Aboud Mohammed na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Ikulu na Mwenyekiti wa TASAF Dkt. Moses Kusiluka.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika wakiwa kwenye sherehe za uzinduzi wa Kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini jijini Dar es Salaam leo.  

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwa Mhe. Kikwete ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi na waliosimama ni Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam.