Monday, February 17, 2020

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AZINDUA KIPINDI CHA PILI CHA AWAMU YA TATU YA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika akitoa maelezo ya awali kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kabla ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kuzindua Kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu ya Mpango huo jijini Dar es Salaam leo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimwangalia Msanii wa Muziki, Mrisho Mpoto alipokuwa akitumbuiza kwenye sherehe za uzinduzi wa Kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini jijini Dar es Salaam leo. Wengine katika picha ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Mohammed Aboud Mohammed na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Ikulu na Mwenyekiti wa TASAF Dkt. Moses Kusiluka

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa na Marais Wastaafu wa Awamu ya Pili, Tatu na Nne wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania wakionyesha Mpango wa Utekelezaji wa TASAF baada ya Rais Magufuli kuzindua Kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini jijini Dar es Salaam leo. Wengine katika picha ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Mohammed Aboud Mohammed na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Ikulu na Mwenyekiti wa TASAF Dkt. Moses Kusiluka.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika wakiwa kwenye sherehe za uzinduzi wa Kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini jijini Dar es Salaam leo.  

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwa Mhe. Kikwete ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi na waliosimama ni Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment