Thursday, February 13, 2020

RAIS MAGUFULI KUZINDUA KIPINDI CHA PILI CHA AWAMU YA TATU YA TASAF



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe. George Mkuchika (Mb) akisisitiza jambo kwa Waandishi wa Habari leo alipokuwa akizungumza nao kuhusu uzinduzi wa Kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) utakaofanyika siku ya Jumatatu tarehe 17 Februari, 2020 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere , Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu IKULU na Mwenyekiti wa Bodi ya TASAF Dkt. Moses Kusiluka na kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Ladislaus Mwamanga.

Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe. George Mkuchika (Mb) (Hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao leo kuhusu uzinduzi wa Kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) utakaofanyika siku ya Jumatatu tarehe 17 Februari, 2020 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere , Dar es Salaam. 

No comments:

Post a Comment