Tuesday, January 5, 2016

MHE. KAIRUKI AKUTANA WATUMISHI WA OFISI YAKE,AMKARIBISHA KATIBU MKUU MTEULE

Watumishi wa Ofisi ya Rais – Utumishi wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angella Kairuki (Mb) (hayupo pichani) wakati wa kikao cha Mhe. Waziri na watumishi wa ofisi hiyo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angella Kairuki (Mb) akizungumza na watumishi wa Ofisi yake (hawapo pichani) wakati wa kikao chake na watumishi hao.

Aliyekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Utumishi, Bw. HAB Mkwizu akizungumza na Watumishi wa Ofisi ya Rais – Utumishi (hawapo pichani) wakati wa kikao cha Mhe. Waziri na watumishi wa ofisi hiyo.

Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Utumishi, Bw. Tixon Nzunda akizungumza na Watumishi wa Ofisi ya Rais – Utumishi (hawapo pichani) wakati wa kikao cha Mhe. Waziri na watumishi wa ofisi hiyo

 Katibu Mkuu mteule Ofisi ya Rais-Utumishi Dkt. Laurian Ndumbaro (kushoto) akipokea Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma (Standing Order) kutoka kwa aliyekuwa akishika nafasi hiyo Katibu Mkuu, Bw. HAB Mkwizu (kulia). Anayeshuhudia ni aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Tixon Nzunda.

Katibu Mkuu mteule Ofisi ya Rais-Utumishi Dkt. Laurian Ndumbaro (kushoto) akipokea Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma (Standing Order) kutoka kwa aliyekuwa akishika nafasi hiyo Katibu Mkuu, Bw. HAB Mkwizu (kulia). Anayeshuhudia ni aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Tixon Nzunda.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi akila kiapo cha utii kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt.Laurian Ndumbaro akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Joseph Magufuli na Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue wakati wa hafla ya kuwaapisha Makatibu Wakuu na Manaibu wao iliyofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.

Monday, January 4, 2016

WAZIRI KAIRUKI AFANYA ZIARA YA KIKAZI TAKUKURU

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akisalimiana na watumishi wa TAKUKURU alipotembelea ofisi hiyo. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akimsikiliza Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bw. Valentino Mlowola alipotembelea ofisi za TAKUKURU.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akizungumza na watumishi wa TAKUKURU (hawapo pichani) alipotembelea ofisi hiyo.

Mtumishi wa TAKUKURU akiuliza swali kwa Mhe. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Angella Kairuki (Mb) (hayupo pichani) wakati Waziri alipokuwa akizungumza na watumishi wa TAKUKURU. 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) (kushoto) akipokea Nyaraka kutoka kwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bw. Valentino Mlowola alipotembelea ofisi za TAKUKURU.