Thursday, August 31, 2023
MSITUME NYARAKA ‘WHATSAPP’ Ni MARUFUKU
Tuesday, August 29, 2023
MHE. RIDHIWANI KIKWETE; MAADILI NI MSINGI WA MAGEUZI YA MAENDELEO ENDELEVU
Naibu Waziri wa
Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete amewasisitiza watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi
kuendelea kufanya kazi kwa bidii, weledi na ubunifu ili tija ya kazi zao iweze
kuonekana kupitia huduma bora wanazozitoa kwa wananchi.
“Ninatamani kuona utendaji kazi wenu unazingitia misingi ya maadili ya utendaji katika utumishi wa Umma kwani ndiyo msingi wa mageuzi kuelekea maendeleo endelevu vinginevyo watumishi wazembe na wenye mienendo isiyofaa kimaadili mwisho wao umefika.” alisisitiza Mhe. Ridhiwani.
Aidha,
amewakumbusha watumishi hao kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Dkt. Samia Suluhu Hassan anasisitiza uadilifu kazini na ametoa haki na stahiki
mbalimbali kwa watumishi, hivyo, Serikali kupitia Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora imekamilisha mapitio, kusanifu na kuanza
kujenga mifumo ya utendaji kazi Serikalini ili dhana ya wajibu pia iweze
kutekelezeka kwa ufanisi.
Pia, Naibu Waziri
huyo amezitaka Mamlaka za Ajira na Nidhamu kuendelea kusimamia haki na stahiki
zote za watumishi na kuachana na kasumba ya utendaji wa mazoea. Pia, amesema
Mamlaka za Ajira na Nidhamu zirejee Sheria ya Utumishi wa Umma, Sura ya 298
ambayo inaonesha kuwa madaraka kuhusu ajira, kuthibitishwa kazini, mafunzo,
kupandishwa cheo, nidhamu hadi hitimisho la kazi kwa mtumishi wa umma
yalishagatuliwa na hivyo kushindwa kutekeleza wajibu huo ni kielelezo cha
kushindwa kutekeleza majukumu waliyopewa.
Katika hatua
nyingine Mhe. Ridhiwani amezitaka Halmashauri nchini kuhakikisha zinaendeleza
miradi ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii- TASAF kwa kuwa ni chaguo na imeridhiwa
na wananchi wenyewe katika maeneo yao. Iwapo Halmashauri na TASAF zitaunganisha
nguvu ni rahisi kuwakomboa wananchi katika umaskini.
“Ninaelekeza
walengwa wote wenye sifa za kunufaika na TASAF wasilipwe fedha nusu
nusu kwa kuwa lengo ni kuwatoa katika wimbi la umaskini” alisema Mhe.
Ridhiwani.
Naye, Mkuu wa
Wilaya ya Manyoni Mhe. Kemilembe Lwotta ameomba pongezi zifike kwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta
watumishi wapya wa kada mbalimbali 228 na wote wameripoti kazini na watumishi
289 walimu na wasio walimu wamepandishwa vyeo na 15 wamebadilishiwa vyeo.
Vilevile,
ameongeza kuwa wananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Itigi katika vijiji
vyote 39 wananufaika vyema na uwepo wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii- TASAF kwa
kiwango kikubwa kwa kuwa kaya masikini zimefikiwa na zinawezeshwa kujikwamua
kiuchumi.
Kwa upande wake
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi Bw. John Mgalula pamoja
na shukurani alizotoa kwa Serikali, ameomba Serikali kuendelea kutoa vibali vya
ajira ili watumishi waongezeke na utoaji huduma kwa umma uimarike.
Mhe. Ridhiwani
amehitimisha ziara yake ya siku moja tarehe 25 Agosti, 2023 katika Halmashauri
ya Wilaya ya Itigi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi na kukagua
utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri hiyo.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi mkoani Singida kwenye kikao kazi ambapo amewataka kufanya kazi kwa weledi na ubunifu katika kuwahudumia wananchi.
Sehemu ya Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi mkoani Singida wakimsiliza Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati alipofanya ziara mkoani humo kwa lengo la kuwataka Watumishi hao kufanya kazi kwa weledi na ubunifu katika kuwahudumia wananchi.
Mkuu
wa wilaya ya Manyoni Mhe.Kemilembe Lwotta akizungumza na Watumishi wa Halmashauri
ya Wilaya ya Itigi mkoani Singida kwenye kikao kazi kabla ya
kumkaribisha Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete na Watumishi
hao ambapo amewataka kufanya kazi kwa weledi na ubunifu katika
kuwahudumia wananchi.
Naibu Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani
Kikwete akisalimia na Katibu Tawala wa wilaya
ya Manyoni ,Bw. James Mchembe mara baada ya kuwasili katika Halmashauri
hiyo kwa lengo la kuzungumza na watumishi ambapo amewataka kufanya kazi kwa
weledi na ubunifu katika kuwahudumia wananchi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashuri ya Wilaya ya Itigi,Bw. John Mgalula akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.
Ridhiwani Kikwete kuzungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Itigi mkoani Singida kwenye kikao kazi ambapo amewataka Watumishi kufanya
kazi kwa weledi na ubunifu katika kuwahudumia wananchi.
Naibu Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani
Kikwete akiandika changamoto zinazowakabili Watumishi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi mkoani Singida kwenye kikao kazi
alichokifanya leo mkoani humo ambapo amewataka kufanya kazi kwa weledi na
ubunifu katika kuwahudumia wananchi.
MHE. KIKWETE; MASLAHI KWA WATUMISHI NI KIPAUMBELE KWA AWAMU YA SITA
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete
amesisitiza kuwa maslahi ya watumishi ni kipaumbele katika awamu hii ya Sita
ili kuongeza motisha na kuchochea zaidi utendaji kazi na utoaji wa huduma bora
kwa umma.
“Kila mara tunaona Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akitangaza kutoa haki na stahiki
mbalimbali kwa watumishi wa umma, hivyo, kila mmoja wetu kwa nafasi yake
anatakiwa pia kuwajibika ipasavyo ili kuleta ufanisi zaidi” ameongeza Mhe.
Ridhiwani.
Mhe. Ridhiwani amesema na kusisitiza hayo tarehe 26
Agosti, 2023 alipokuwa akizungumza na viongozi wa Sekretarieti ya Mkoa wa
Singida katika ofisi hizo. Aidha,
amewakumbusha watumishi hao kutoka ofisini na kwenda kuwahudumia wananchi na
kutatua changamoto zilizo ndani ya uwezo wao.
Katika hatua nyingine Mhe. Ridhiwani ametembelea na
kukagua ujenzi wa majengo ya Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Singida
awamu ya pili inayohusu majengo ya madarasa na vyoo vya nje na kuelekeza
viongozi kuhakikisha miundombinu ya watu wenye ulemavu inazingatiwa katika ujenzi huo.
“Chuo cha Utumishi wa Umma ni muhimu sana kwa kuwa
kinaandaa watumishi wa umma bora na ambao ni msingi wa maendeleo ya nchi katika
nyanja zote” ameongeza Mhe. Ridhiwani.
Vilevile, akiwa katika ziara ya kutembelea wanufaika
wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii- TASAF katika Kijiji cha Ughaugha Kata ya
Unyamikumbi, Manispaa ya Singida amesema Serikali imetoa zaidi ya bilioni 51
kwa ajili ya kunusuru kaya maskini nchini ili ziweze kuboresha maisha yao
mathalani kwa kupata chakula milo 3 kwa siku, kusomesha watoto na kupata huduma
za matibabu kwenye vituo vya afya na zahanati.
Naye, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Bw.
Stanislaus Choaji amesema wamepokea maelekezo na
watahakikisha wanatazama kwa jicho pevu maeneo ya pembezoni katika Mkoa wa
Singida kwa kutoa na kupanga watumishi ili kuboresha utoaji wa huduma kwa umma.
Aidha, Bw. Choaji ameongeza kuwa wananchi wa Mkoa wa
Singida wananufaika na uwepo wa TASAF kwa kuwa kaya maskini ambazo ni wanufaika
wamepata fedha na wanafanya shughuli za kiuchumi ikiwemo kufuga
Mbuzi, Kuku na Kondoo kwa ajili ya kujikwamua katika wimbi la umaskini, hivyo
salamu za shukurani zimfikie Mhe. Dkt.
Samia Suluhu Hassan kwa ukombozi huo.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu,
Chuo cha Utumishi wa Umma Dkt. Ernest Mabonesho amesema ujenzi umefikia
asilimia 21 na kazi inayoendelea ni ujenzi wa kuta ambapo hadi sasa mradi huo
umetoa ajira za vibarua kwa wananchi 96 wanaozunguka eneo la mradi ikiwa
wanaume ni 62 na wanawake ni 34.
Mhe. Ridhiwani amehitimisha ziara yake ya siku mbili
katika Mkoa wa Singida kwa tarehe 25-26 Agosti, 2023 ambapo alianzia
Halmashauri ya Wilaya ya Itigi na kumalizia katika Manispaa ya Singida. Ziara
hiyo ililenga kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi na kukagua utekelezaji wa
miradi ya TASAF katika Mkoa huo.
Naibu Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani
Kikwete akizungumza na viongozi wa
Sekretarieti ya Mkoa wa Singida ambapo amesema
kuwa maslahi ya watumishi ni kipaumbele katika awamu hii ya Sita ili
kuongeza motisha na kuchochea zaidi utendaji kazi na utoaji wa huduma bora kwa
umma.
Sehemu ya wanufaika wa
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii- TASAF katika Kijiji cha Ughaugha Kata ya Unyamikumbi,
Manispaa ya Singida wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete ambapo amewaeleza kuwa Serikali
imetoa zaidi ya bilioni 51 kwa ajili ya kunusuru kaya hizo
.
Baadhi ya
Wakurugenzi wa Taasisi mbalimbali za mkoa wa Singida pamoja na Wajumbe wa Kamati
ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo wakimsiliza
Naibu Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani
Kikwete wakati alipotembelea na kukagua ujenzi
wa majengo ya Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Singida awamu ya pili
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akioneshwa ramani ya majengo ya Chuo cha Utumishi wa
Umma, Kampasi ya Singida awamu ya pili mara baada ya kufika katika eneo hilo kwa ajili kukagua ujenzi wa chuo hicho
unavyoendelea
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza mara baada ya
kutembelea na kukagua ujenzi wa majengo ya Chuo cha Utumishi wa
Umma, Kampasi ya Singida awamu ya pili mara baada ya kufika katika eneo
hilo
Muonekano wa
baadhi ya majengo ya Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Singida ambayo
tayari yameshakamilika
Mnufaika wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii- TASAF
katika Kijiji cha Ughaugha Kata ya Unyamikumbi, Manispaa ya Singida, Mariamu
Luguti ambaye amewezeshwa kufuga mbuzi akizungumza mbele ya Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete ambapo ameishukuru Serikali kwa
kumsaidia kuondokana kwenye lindi la umasikini
Kaimu Mkuu wa
Chuo na Mtendaji Mkuu, Chuo cha Utumishi wa Umma Dkt. Ernest Mabonesho
akizungumza mbele ya Naibu Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani
Kikwete
ambapo amesema ujenzi umefikia asilimia
21wa Chuo cha Utumisi wa Umma Kampasi ya Singida
Friday, August 25, 2023
MHE. SIMBACHAWENE AWATAKA WANANCHI KUPUUZA TAARIFA ZA UZUSHI KUHUSIANA NA NDEGE YA RAIS Gulf Stream (G550)
Na. Veronica Mwafisi-Dar es Salaam
Tarehe 25 Agosti, 2023
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amewataka wananchi kupuuza taarifa za uzushi zinazosambazwa na watu wasio wema kuhusiana na ndege ya Rais Gulf Stream (G550) kushikiliwa nchini Dubai.
Mhe.
Simbachawene ameyasema hayo leo wakati akizindua Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ndege za Serikali katika Kituo cha
Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
“Mtu anaweza kuzusha jambo na likawapotezea muda mwingi wananchi badala ya kufanya mambo ya maendeleo, kwa mfano uzushi kuhusiana na ndege ya Rais Gulf Stream (G550) kuzuiliwa Dubai, nataka niwahakikishie Watanzania kuwa ndege hiyo ipo sehemu husika kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 1 VIP, jijini Dar es Salaam kwenye eneo ambalo Wakala wa Ndege za Serikali wanalitumia na yeyote anayepita barabarani ataiona,” Mhe. Simbachawene amesisitiza.
Mhe. Simbachawene amesema yeye akiwa ndiye Waziri mwenye dhamana ya Utawala Bora ameona aliweke wazi jambo hilo, lililoleta taharuki ili kuwaondoa hofu Watanzania na uvumi huo ulioenea, hivyo lisiwapotezee muda wao na kuwahakikishia wanaovumisha hayo kwa nia ovu wanaweza kwenda kupata uhakika wa uwepo wa ndege hiyo ambapo ameongeza kuwa Viongozi wanasafiri kama kawaida kwa kutumia ndege hiyo.
Aidha, Mhe. Simbachawene ametoa wito kwa Wajumbe wa Bodi hiyo kushirikiana na Menejimenti ya Wakala wa Ndege za Serikali ili kuiwezesha Wakala hiyo kutekeleza majukumu yake ipasavyo.
“Ni matarajio yangu kuwa Bodi hii itasimamia vema utendaji wa Wakala hii ili kuleta tija kwa maendeleo ya taifa kama inavyosisitizwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan,” Mhe. Simbachawene amesisitiza.
Akitoa neno la shukrani, Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ndege za Serikali, Prof. Mhandisi, Idrissa Mshoro amemuahidi Mhe. Simbachawene kuwa, yeye pamoja na Wajumbe wa Bodi hiyo kwa kushirikiana na Menejimenti ya TGFA watatekeleza yote ambayo ameyaelekeza kwani wanafahamu kwa kina maono makubwa ya Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika katika kuharakisha maendeleo ya nchi katika kuhakikisha uwepo wa usafiri madhubuti.
Kwa upande wake, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za
Serikali (TGFA) Capt. Budodi Budodi amesema Menejimenti ya
Wakala inamhakikishia Mhe. Simbachawene kuwa wataendelea kutekeleza majukumu
yao kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu pamoja na maelekezo ya Bodi
ya Ushauri ya Wakala wa Ndege za Serikali ili kufikia malengo ya uanzishwaji wa Wakala hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene
akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ndege za Serikali kabla
ya kuzindua bodi hiyo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene
akisisitiza jambo kwa Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ndege za Serikali
wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa bodi hiyo jijini Dar es Salaam.
Sehemu
ya Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ndege za Serikali wakimsikiliza Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George
Simbachawene alipokuwa akizungumza nao wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa bodi
hiyo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais
Ikulu, Bw. Mululi Mahendeka akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
George Simbachawene kuzindua Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ndege za Serikali
jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ndege za Serikali, Prof. Mhandisi, Idrissa Mshoro akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George
Simbachawene mara baada ya Waziri Simbachawene kuzindua Bodi hiyo jijini Dar es
Salaam.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa
Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) Capt.
Budodi Budodi akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi yake kwa
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. George Simbachawene kabla ya Waziri huyo kuzindua Bodi ya Ushauri ya
Wakala wa Ndege za Serikali jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene
akikabidhi vitendea kazi kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya
Wakala wa Ndege za Serikali, Prof. Mhandisi,
Idrissa Mshoro, mara baada ya Waziri huyo kuzindua Bodi ya Ushauri ya Wakala hiyo jijini
Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene
akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi
ya Ushauri ya Wakala wa Ndege za Serikali mara baada ya kuzindua Bodi hiyo jijini
Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene
akiagana na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) Capt. Budodi Budodi mara baada ya Waziri
huyo kuwasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere
(JNICC) jijini Dar es Salaam kuzindua Bodi ya Ushauri ya Wakala hiyo jijini Dar
es Salaam. Wanaoshuhudia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu, Bw. Mululi
Mahendeka na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ndege za
Serikali, Prof. Mhandisi, Idrissa
Mshoro.
Thursday, August 24, 2023
MHE. SIMBACHAWENE AIPONGEZA WHI KWA KUENDELEA KUJENGA MAKAZI BORA YA WATUMISHI , ASISITIZA KUJENGA ZAIDI KARIBU NA MAENEO YA KAZI
Na. Veronica Mwafisi-Dodoma
Tarehe 24 Agosti, 2023
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ameipongeza Taasisi ya Watumishi Housing Investments (WHI) kwa kuendelea kujenga makazi bora ya watumishi wa umma nchini na kuwasisitiza kuelekeza nguvu zaidi ya ujenzi jirani na maeneo ambayo watumishi wanafanya kazi ili kuwaondolea changamoto ya makazi kwa lengo la kuboresha utendaji kazi.
Me. Simbachawene amezungumza hayo jijini Dodoma wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua mradi wa ujenzi wa nyumba zilizojengwa na taasisi hiyo eneo la Njedengwa na Kisasa Relini kwa lengo la kuwauzia na kuwapangisha watumishi wa umma na wanachama wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
Mhe. Simbachawene amesema kitendo cha watumishi wa umma kutokuwa na makazi bora na kuwa mbali na maeneo yao wanayofanyia kazi ni changamoto kubwa inayoathiri utendaji kazi, hivyo ameisisitiza taasisi hiyo kuona umuhimu wa kufanya hivyo kwani licha ya kuwasaidia watumishi kupata makazi bora watakuwa wametekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi na maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hasssan ya kuhimiza uwepo wa makazi bora kwa watumishi ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Mhe. Simbachawene ameongeza kuwa, umuhimu wa kuwa na makazi bora karibu na maeneo ya kazi, kutawasaidia watumishi hasa wanaoajiriwa kwa mara ya kwanza maeneo ambayo yana changamoto ya nyumba, kutohangaika.
“Mkijenga nyumba maeneo ya jirani na vituo vya kazi, kutawasaidia sana watumishi hasa wa ajira mpya kutopata changamoto na kuchukia kazi kwa sababu ya kuhangaika kutafuta sehemu nzuri ya kuishi,” Mhe. Simbachawene amesisitiza.
Kwa upande wake Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete ameungana na Mhe. Simbachawene kuipongeza taasisi hiyo kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kujenga nyumba bora kwa ajili ya kuwauzia na kuwapangisha watumishi wa umma na wanachama wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
Naye, Mtendaji Mkuu wa Watumishi Housing Investments (WHI) Dkt. Fredy Msemwa, amewashukuru viongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kutembelea mradi wa ujenzi wa nyumba zinazojegwa na taasisi hiyo katika eneo la Kisasa Relini na Njedengwa na kuhimiza uwajibikaji na ubunifu.
Dkt. Msemwa
amewaahidi viongozi hao kuwa, watayafanyia kazi maelekezo yote ambayo wameyatoa
kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na
Waandishi wa Habari mara baada ya kukagua mradi wa nyumba zilizojengwa na Watumishi
Housing Investments (WHI) eneo la Njedengwa na Kisasa Relini jijini Dodoma wakati wa ziara yake ya kikazi
iliyolenga kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa WHI.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza kabla ya
kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kuzungumza na Waandishi wa Habari mara
baada ya kukagua mradi wa nyumba zilizojengwa na Watumishi
Housing Investments (WHI) eneo la Njedengwa na Kisasa Relini jijini Dodoma wakati wa ziara yake ya kikazi
iliyolenga kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa WHI.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akimsikiliza Mkurugenzi
Mtendaji wa Watumishi Housing Investments (WHI), Dkt. Fred Msemwa alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi
wa nyumba zilizojengwa na WHI eneo la Njedengwa na Kisasa
Relini jijini Dodoma. Kulia kwake ni Naibu
Katibu Mkuu wa Ofisi yake, Bw. Xavier Daudi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiambatana na Naibu Waziri
wake, Mhe. Ridhiwani Kikwete na Naibu Katibu Mkuu
wa Ofisi yake, Bw. Xavier Daudi wakielekea kukagua mradi wa nyumba zilizojengwa na Watumishi
Housing Investments (WHI) eneo la Njedengwa jijini Dodoma wakati wa ziara yake ya kikazi
iliyolenga kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa WHI.
Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi
akimuonyesha Mtendaji wa Watumishi Housing Investments (WHI), Dkt.
Fred Msemwa namna alivyovutiwa na mojawapo ya nyumba zilizojengwa
na Watumishi Housing Investments (WHI) walipokuwa
wakimsubiri Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kukagua
mradi wa nyumba hizo
eneo la Kisasa Relini jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akifurahia jambo na
Menejimenti ya Watumishi Housing Investments (WHI) wakati wa ziara yake ya
kikazi iliyolenga kukagua nyumba zilizojengwa na Watumishi
Housing Investments (WHI) eneo la Njedengwa na Kisasa Relini jijini Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza jambo na
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi
wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene iliyolenga kukagua mradi
wa nyumba zilizojengwa na Watumishi Housing Investments
(WHI) eneo la Njedengwa na Kisasa Relini jijini Dodoma.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Watumishi Housing Investments (WHI), Dkt. Fred Msemwa akitoa ufafanuzi
kwa Waandishi wa Habari kuhusu mradi wa nyumba zilizojengwa na WHI eneo la
Njedengwa na Kisasa Relini jijini Dodoma.
Wednesday, August 23, 2023
Tuesday, August 15, 2023
OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAPONGEZWA NA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA KWA KUIPA USHIRIKIANO KAMATI HIYO WAKATI WA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YAKE
Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama akiongoza kikao kazi
cha kamati yake na Watendaji wa Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhusu Utekelezaji wa Mpango na
Bajeti wa Taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo (TGFA, eGA na Taasisi ya UONGOZI) kwa mwaka
2022/23.
Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na
Sheria wakiwa katika kikao kazi cha kamati hiyo na Watendaji wa Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kilicholenga
kuwasilisha Utekelezaji wa Mpango na Bajeti wa taasisi zilizo chini ya Ofisi
hiyo (TGFA,
eGA na Taasisi ya UONGOZI) kwa mwaka
2022/23.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwasilisha taarifa ya Utelezaji wa Mpango na Bajeti wa taasisi zilizo chini ya Ofisi yake (TGFA, eGA na Taasisi ya UONGOZI) kwa mwaka 2022/23 kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao cha kamati hiyo kilichofanyika jijini Dodoma.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.
Ridhiwani Kikwete akitoa neno la shukrani kwa Wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria mara baada ya kumalizika kwa kikao
kazi cha kamati hiyo kuhusu Utekelezaji wa Mpango na Bajeti wa
taasisi
zilizo chini ya ofisi hiyo (TGFA, eGA na Taasisi ya UONGOZI) kwa mwaka
2022/23
kilichofanyika jijini Dodoma.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA), Cpt. Budodi
Budodi akijibu moja ya hoja ya
taasisi yake kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na
Sheria wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na Watendaji wa Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhusu
Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa taasisi zilizo chini ya ofisi hiyo (TGFA, eGA
na Taasisi ya UONGOZI) kwa Mwaka 2022/23.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali
Mtandao (eGA), Mhandisi Benedict Ndomba akitoa ufafanuzi wa hoja za masuala ya
serikali mtandao zilizowasilishwa na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na
Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhusu
Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa taasisi zilizo chini ya ofisi hiyo (TGFA, eGA
na Taasisi ya UONGOZI) Kwa Mwaka
2022/23.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI,
Bw. Deogratias Usangira akijibu moja ya hoja ya Taasisi ya UONGOZI kwa
wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati
wa kikao kazi cha kamati hiyo na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhusu Utekelezaji wa Mpango na
Bajeti kwa taasisi zilizo chini ya ofisi hiyo (TGFA, eGA na Taasisi ya
UONGOZI) kwa Mwaka 2022/23.
Mjumbe wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Mashimba Ndaki akichangia hoja kuhusu serikali mtandao wakati
wa kikao kazi cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria
na viongozi pamoja na watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora kuhusu Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa
taasisi zilizo chini ya ofisi hiyo (TGFA, eGA na Taasisi ya UONGOZI) kwa Mwaka
2022/23.
Katibu Mkuu-IKULU, Bw.
Mululi Majula Mahendeka akitoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja
iliyowasilishwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na
Sheria wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhusu Utekelezaji wa Mpango na
Bajeti kwa taasisi zilizo chini ya ofisi hiyo (TGFA, eGA na Taasisi ya
UONGOZI) kwa Mwaka 2022/23.
Naibu Katibu Mkuu,
Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi akitoa
ufafanuzi wa moja ya hoja iliyowasilishwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Utawala Katiba na Sheria wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhusu
Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa taasisi zilizo chini ya ofisi hiyo (TGFA, eGA
na Taasisi ya UONGOZI) kwa Mwaka 2022/23.
Sehemu ya Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwa katika kikao kazi
cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria na Watendaji wa
ofisi hiyo kuhusu Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa taasisi zilizo chini ya ofisi
hiyo (TGFA,
eGA na Taasisi ya UONGOZI) kwa Mwaka 2022/23.