Saturday, December 30, 2023
Saturday, December 23, 2023
Friday, December 22, 2023
MHE. KIKWETE AWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUTUMIA MIFUMO YA TEHAMA KUBORESHA UTENDAJI KAZI
Na. Rainer Budodi - Dodoma
Tarehe 20 Desemba, 2023
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete amewataka watumishi wa Ofisi ya Rais, Mipango na
Uwekezaji, Wizara ya Mambo ya Nje na Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini-GPSA
kuzingatia mafunzo wanayopewa ili kuboresha utendaji kazi wa watumishi na
taasisi kwa jumla.
Mhe. Kikwete amesema hayo jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo ya
matumizi ya mifumo ya kupima utendaji kazi wa watumishi na taasisi (PEPMIS, PIPMIS)
na HR Assesment kwa nyakati tofauti.
Mhe. Kikwete ameongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na
Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inalenga kutoa huduma bora zaidi kwa
wananchi, hivyo Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
imebuni mifumo hiyo kwa lengo la kutatua changamoto za upimaji wa utendaji kazi
wa watumishi na taasisi na zaidi kutambua hali halisi ya uwiano wa
rasilimaliwatu katika utumishi wa umma.
Aidha, Mhe. Kikwete amesema kuwa mfumo wa zamani wa upimaji utendaji
kazi wa watumishi kwa kujazaji fomu za OPRAS ulionekana kushindwa kupima
uhalisia wa kiutendaji kwa watumishi wa umma. Hivyo mifumo hii ya PEPMIS na PIPMIS
itatatua changamoto iliyokuwapo hapo awali na kuleta ufanisi zaidi.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,
Mipango na Uwekezaji Dkt. Tausi Kida ameishukuru na kuipongeza Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kubuni na kusanifu mifumo
hii muhimu itakayoleta ufanisi wa kiutendaji na kuzingatia haki na wajibu kwa
watumishi wa umma na Serikali kwa jumla.
“Tumefurahia ujio wa mifumo hii ambayo
italeta chachu kwa watumishi wa umma katika kuwahudumia wananchi na kuifanya
Serikali kuboresha maeneo yenye changamoto kwa watumishi na taasisi” Amesema
Dkt. Kida.
Dkt. Kida ameongeza kuwa ofisi yake iko tayari kuunganisha mifumo hii ya
PEPMIS, PIPMIS na HR Assessment kwenye Dira ya taifa ya mwaka 2050 ambayo
itaenda kuonesha mwelekeo wa nchi kwa miaka 25 ijayo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akifungua mafunzo ya matumizi ya mfumo wa kupima
utendaji kazi wa mtumishi na taasisi (PEPMIS na PIPMIS) kwa watumishi wa Ofisi
ya Rais, Mipango na Uwekezaji katika ukumbi mdogo uliopo katika jengo
Mkandarasi House Jijini Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akiongea na watumishi wa Ofisi ya Rais, Mipango na
Uwekezaji wakati akifungua mafunzo ya matumizi ya mfumo wa kupima utendaji kazi
wa mtumishi na taasisi katika ukumbi uliopo Mkandarasi House Jijini Dodoma
tarehe 19 Desemba, 2023. Kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Mipango na
Uwekezaji Dkt. Tausi Kida na Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa
Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais- UTUMISHI Bi. Felista Shuli.
Baadhi ya watumishi kutoka Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati akifungua mafunzo ya matumizi ya mfumo wa kupima utendaji kazi wa mtumishi na taasisi katika ukumbi uliopo Mkandarasi House Jijini Dodoma.
Baadhi ya watumishi kutoka Ofisi ya Rais, Mipango na
Uwekezaji wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete (Hayupo Pichani) wakati
akifungua mafunzo ya matumizi ya mfumo wa kupima utendaji kazi wa mtumishi na taasisi
katika ukumbi uliopo Mkandarasi House Jijini Dodoma.
Thursday, December 21, 2023
WATUMISHI WA UMMA SASA KUJIPIMA UTENDAJI KAZI KWA KUTUMIA MIFUMO YA TEHAMA
Na. Veronica Mwafisi- Dumila
Tarehe 20 Desemba, 2023
Naibu Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi amewaasa watumishi wa umma wa
Halmashauri Wilaya ya
Kilosa Kanda ya Dumila kujipima kupitia Mifumo Mipya ya PEPMIS, PIPMIS na HR
Assessment kwa kujaza kazi wanazotekeleza kila siku ili mfumo uweze kutoa alama
sahihi.
Amesema hayo wakati alipotembelea kanda ya
kimafunzo ya Dumila kuona maendeleo ya Mafunzo ya Mifumo hiyo.
Bw. Daudi amesema kuwa, mafunzo hayo
yanalenga kuwaongezea watumishi wa umma ujuzi na ari ya kutumia mifumo ya
TEHAMA katika kupima utendaji kazi na utekelezaji wa shughuli mbalimbali Serikalini.
“Serikali ya Awamu ya Sita
inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu
Hassan inafanya juhudi kubwa katika kusimamia na kutoa stahiki na maslahi mbalimbali
kwa watumishi wa umma. Hivyo, ni jukumu la watumishi kumuunga mkono kwa kutoa
huduma bora kwa umma” alisema Bw. Daudi.
Aidha, Bw. Daudi ameongeza kuwa, moja
ya majukumu ya Ofisi ya Rais -UTUMISHI ni kusimamia utumishi wa umma, ndio
maana Serikali imebuni mifumo hiyo ambayo itaboresha utendaji kazi Serikalini
kwa kumpima mtumishi mmoja mmoja na taasisi.
Bw. Daudi amefafanua kuwa kupitia
mfumo wa PEPMIS kila Mwajiri atakuwa na uwezo wa kuona namna watumishi wake
wanavyofanya kazi kila siku.
Naibu
Katibu Mkuu huyo, amesema amefurahishwa na namna watumishi wa umma katika mkoa
wa Morogoro walivyoitikia wito wa kushiriki mafunzo hayo na wameonesha utayari
wa kutumia mifumo hiyo ili kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan
anayetaka kuona kunakuwa na utumishi wa umma bora na wenye kuhudumia wananchi kwa
ufanisi mkubwa.
Naibu
Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi akizungumza na baadhi ya Viongozi na Watumishi wa Halmashauri Wilaya
ya Kilosa Kanda ya Dumila (hawapo pichani) alipowatembelea
kuona maendeleo ya Mafunzo ya Mifumo ya PEPMIS, PIPMIS na HR Assesment kwa Mkoa
wa Morogoro.
Baadhi ya Viongozi na Watumishi wa Halmashauri
Wilaya ya Kilosa Kanda ya Dumila wakimsikiliza Naibu
Katibu Mkuu, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi alipowatembelea kuona
maendeleo ya Mafunzo ya Mifumo ya PEPMIS, PIPMIS na HR Assesment kwa Mkoa wa Morogoro.
Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA
Serikalini, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
ambaye pia ni Msimamizi Mkuu wa Mafunzo ya Mifumo ya PEPMIS, PIPMIS na HR
Assesment kwa Mkoa wa Morogoro, Bw. Priscus
Kiwango akimueleza Naibu Katibu Mkuu, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi maendeleo ya mafunzo ya
mifumo hiyo.
Wednesday, December 20, 2023
WATUMISHI WA UMMA KILOSA, MIKUMI NA DUMILA WAPATA MAFUNZO YA MATUMIZI YA MIFUMO YA TEHAMA
Na. Veronica Mwafisi- Kilosa, Mikumi na Dumila
Tarehe 19 Desemba, 2023
Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA Serikalini, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora
ambaye pia ni Msimamizi Mkuu wa Mafunzo ya PEPMIS, PIPMIS na HR Assesment kwa
Mkoa wa Morogoro, Bw. Priscus
Kiwango amewataka watumishi wa umma katika mkoa wa Morogoro kuzingatia
mafunzo wanayopewa ili kuboresha utendaji kazi wao na taasisi kwa jumla.
Bw. Kiwango amesema mifumo hii itawawezesha viongozi kusimamia utendaji kazi wa watumishi wao bila upendeleo ikiwemo kupanda vyeo kwa haki, kupima utendaji kazi wa Taasisi za Umma na kufanya Tathmini ya hali ya Rasilimaliwatu Serikalini kwa lengo la kuimarisha utoaji wa huduma kwa umma.
Amesema hayo katika nyakati tofauti wakati wa mafunzo ya namna ya kutumia mifumo mipya ya PEPMIS, PIPMIS na HR Assesment kwa Watumishi wa Umma na taasisi zilizopo mkoani Morogoro katika Kanda tatu ikiwemo Mikumi, Kilosa Mjini na Dumila.
Mkurugenzi
Kiwango ameongeza kuwa mafunzo hayo yanaendelea kutolewa kwenye Halmashauri ya
Wilaya Kilosa, Gairo, Morogoro mjini na kwa baadhi ya taasisi na kwa watendaji
wa kata na vijiji, walimu wa sekondari na msingi, watumishi wa kilimo, mifugo
na ustawi wa jamii.
“Mpaka sasa kwa mkoa wa
Morogoro tumetoa mafunzo kwa taasisi 21 ikiwemo Ofisi ya RAS, Halmashauri ya
Morogoro DC, Manispaa ya Morogoro, Mvomero, Malinyi, Mlimba, Ifakara Ulanga,
Kilosa, Mikumi na Dumila na kwa mwenendo huu tutakamilisha mafunzo kwa wakati
uliopangwa”. Alisema Bw. Kiwango.
Kwa upande wake, Mkufunzi wa mafunzo hayo ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi
anayesimamia huduma za Uuguzi na Ukunga nchini, Wizara ya Afya, Bw. Paul
Mashauri amesema watumishi wa umma mkoa wa Morogoro wanaonesha utayari wa
kutumia mifumo hii katika utendaji kazi wao kutokana na uwazi uliopo katika
mifumo.
Naye, Mkurugenzi Msaidizi Mipango na Bajeti, Wizara ya Mifugo na
Uvuvi, Bi. Matilda Mtenga ambaye pia ni mkufunzi ameongeza kuwa, mwitikio
wa watumishi wa umma katika mkoa wa Morogoro ni mkubwa na wanafurahi kuona ujio
wa mifumo inayonesha uwezo wa kila
mtumishi wa umma.
Ofisi ya Rais-UTUMISHI inaendelea
kutoa Mafunzo ya PEPMIS, PIPMIS na HR Assesment katika Mikoa yote Tanzania Bara
na yanatarajiwa kuhitimishwa Desemba 31,2023.
Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA Serikalini, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambaye pia ni Msimamizi Mkuu wa Mafunzo ya Mifumo ya
PEPMIS, PIPMIS na HR Assesment kwa Mkoa wa Morogoro Bw. Priscus Kiwango akizungumza
na baadhi
ya Viongozi na Watumishi wa Halmashauri Wilaya ya
Kilosa Kanda ya Mikumi wakati akifungua
Mafunzo
ya Mifumo hiyo katika Ukumbi wa Veta mkoani humo.
Baadhi ya Viongozi na Watumishi wa Halmashauri
Wilaya ya Kilosa Kanda ya Mikumi wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA Serikalini, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora ambaye pia ni Msimamizi Mkuu wa Mafunzo ya Mifumo ya PEPMIS, PIPMIS na
HR Assesment kwa Mkoa wa Morogoro Bw. Priscus Kiwango (hayupo
pichani) wakati akifungua
Mafunzo
ya Mifumo hiyo.
Baadhi ya Viongozi na Watumishi wa Halmashauri
Wilaya ya Kilosa wakifuatilia Mafunzo ya Mifumo ya PEPMIS, PIPMIS na HR Assesment
yanayotolewa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
mkoani Morogoro.
Mkurugenzi Msaidizi
anayesimamia huduma za Uuguzi na Ukunga nchini, Wizara ya Afya, ambaye pia ni Mkufunzi
wa mafunzo ya PEPMIS, PIPMIS na HR Assessment, Bw. Paul Mashauri akiwaelekeza watumishi
wa Halmashauri Wilaya ya Kilosa, Kanda ya Mikumi mkoani
Morogoro
namna ya kuingia na kutumia Mifumo hiyo wakati wa mafunzo.
Mkurugenzi
Msaidizi Mipango na Bajeti, Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mkufunzi wa
mafunzo ya PEPMIS, PIPMIS na HR Assessment, Bi. Matilda Mtenga akiwaelekeza
watumishi Halmashauri Wilaya ya Kilosa, Kanda ya Mikumi mkoani Morogoro
namna ya kuingia na kutumia Mifumo hiyo wakati wa mafunzo.
Thursday, December 14, 2023
WATUMISHI WA UMMA WAASWA KUTOKUWA NA HOFU NA MFUMO MPYA WA TATHIMINI YA WATUMISHI
WATUMISHI WA UMMA WAASWA KUTOKUWA NA HOFU NA MFUMO MPYA WA TATHIMINI YA WATUMISHI.
Na Lusungu Helela-Dar es Salaam
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema Mfumo wa Mahitaji ya Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma (HRA) hauna lengo la kumuondoa kazini ama kuwaonea watumishi wa umma hivyo hawana sababu ya kuuhofia mfumo huo.
Mhe. Kikwete amebainisha hayo wakati wa ufungaji wa mafunzo ya siku tatu kwa watumishi wa umma kutoka Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) Shirika la Masoko Kariakoo na Bodi ya Sukari Tanzania yaliyofanyika MOI.
Amesema lengo la mfumo huo ni kuiwezesha kupima utendaji wa watumishi wake kwa njia rahisi na kuongeza ufanisi wenye tija kazini.
“Mfumo huu hauna lengo la kukomoa watu, tunatakuwa na utumishi wa umma unaotimiza majukumu, utawezesha kupamga utumishi wenye tija, huna sababu ya kuhofia” amesema Mhe: Kikwete
Amesema mifumo hiyo inakwenda kuonesha wapi kwenye mapungufu ili paweze kuboreshwa
Aidha aliipongeza MOI kwa kutoa huduma bora kwa Watanzania na kuitaka kuendelea na kasi hiyo kwa maslahi ya umma.
“MOI inaendelea kuwa bora hii yote ni juhudi zako Profesa Makubi na timu yako, hongera sana, tunahitaji utumishi wenye tija” amesema
Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Prof. Abel Makubi akimkaribisha Naibu Waziri huyo alimpongeza kwa kuitembelea MOI mara kwa mara na kwamba hatua hiyo inaongeza ari kwa watumishi kufanya kazi kwa umahiri.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza leo wakati wa ufungaji wa mafunzo ya siku tatu kwa watumishi wa umma kutoka Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) Shirika la Masoko Kariakoo na Bodi ya Sukari Tanzania yaliyofanyika MOI.
Mkurugenzi wa Uendelezaji Taasisi, Naolasci Kipanda ambaye pia ni Mwezeshaji wa Mafunzo ya Mfumo wa Mahitaji ya Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma (HRA) Nestory Kipanga akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Mhe.Ridhiwani Kikwete leo wakati wa ufungaji wa mafunzo ya siku tatu kwa watumishi wa umma kutoka Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) Shirika la Masoko Kariakoo na Bodi ya Sukari Tanzania yaliyofanyika MOI.
Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Prof. Abel Makubi akizungumza leo wakati wa ufungaji wa mafunzo ya siku tatu kwa watumishi wa umma kutoka Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) Shirika la Masoko Kariakoo na Bodi ya Sukari Tanzania yaliyofanyika MOI.
Tuesday, December 12, 2023
WATUMISHI WA UMMA KUJAZA KAZI WANAZOFANYA KATIKA MFUMO MAHALI POPOTE
Na. Rainer Budodi na Veronica Mwafisi- Dodoma
Tarehe 12 Desemba, 2023
Mkurugenzi wa Idara ya
Utawala wa Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais- UTUMISHI ambaye pia ni Msimamizi
Mkuu wa Mafunzo ya PEPMIS, PIPMIS na HR Assesment kwa Mkoa wa Dodoma Bi.
Felista Shuli amesema Serikali imedhamiria kuimarisha Utumishi wa Umma kwa
kuhimiza uwajibikaji wa hiari wa mtumishi kwa kujaza kazi anazofanya kila siku
katika mfumo mahali popote ili kuongeza tija katika utoaji wa huduma kwa umma.
Ameyasema hayo leo tarehe
12 Desemba, 2023 wakati wa kufungua mafunzo ya matumizi ya Mfumo wa Kupima
Utendaji Kazi wa Watumishi wa Umma na Taasisi (PEPMIS na PIPMIS) na Mfumo
Maalum wa Tathmini ya hali ya Rasilimaliwatu Serikalini (HR Assesment) kwa
viongozi na watumishi wa Wizara ya Fedha katika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma.
Bi. Felista amefafanua
kuwa mfumo wa PEPMIS utawezesha viongozi
kusimamia utendaji kazi wa watumishi bila upendeleo na utaongeza ufanisi, PIPMIS itawezesha kupima utendaji kazi wa
Taasisi za Umma na HR Assesment itawezesha kufanya Tathmini ya hali ya Rasilimaliwatu
Serikalini na kuitumia ipasavyo.
Aidha, Bi. Shuli ameongeza kuwa hali
ya mafunzo kwa Mkoa wa Dodoma inaendelea vizuri na anaamini yatakamilika kama
ilivyopangwa kwa kuwa pande zote zinazohusika na mafunzo zinatoa ushirikiano mkubwa
kwa wakati.
“Wawezeshaji wote wako vizuri na
watumishi kutoka katika Wizara na Taasisi zote wanaitikia wito na wanakuja na kompyuta
ambazo ni kitendea kazi muhimu sana katika mafunzo haya” amesema Bi.Felista.
Vilevile, amesema mfumo wa
PEPMIS umekuja kuwa mbadala wa OPRAS ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais, Mhe.
Dkt. Samia Suluhu Hassan anayelenga kuimarisha mifumo ya uwajibikaji inayowezesha
viongozi na watumishi wa umma kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi
wakati na mahali popote.
Awali, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya
Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Wizara ya Fedha Bw. Renatus Msagira
amesema watumishi wako tayari kujifunza na kutumia mifumo hiyo kwa ufanisi kwa
maendeleo ya taifa.
“Tuko tayari na hatutakuwa kikwazo
katika utekelezaji wa jitihada hizi muhimu za Serikali ambazo lengo lake ni
kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora kwa wakati” amesisitiza Bw. Msagira.
Mafunzo ya PEPMIS, PIPMIS
na HR Assesment yanaendeshwa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora katika Mikoa yote Tanzania Bara na yatahitimishwa Desemba
31,2023.
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambaye pia ni Msimamizi Mkuu wa Mafunzo ya PEPMIS, PIPMIS na HR Assesment kwa Mkoa wa Dodoma Bi. Felista Shuli akizungumza na Viongozi na Watumishi wa Wizara ya Fedha wakati akifungua Mafunzo ya Mifumo hiyo katika Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.
Baadhi ya Viongozi na Watumishi wa Wizara
ya Fedha wakimsikiliza Mkurugenzi
wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora ambaye pia ni Msimamizi Mkuu wa Mafunzo ya PEPMIS, PIPMIS na HR Assesment
kwa Mkoa wa Dodoma Bi. Felista
Shuli (hayupo pichani) wakati akifungua Mafunzo ya Mifumo hiyo jijini Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi Sehemu
ya Utawala, Ofisi ya Rais UTUMISHI Bi. Nyasinde Mukono (Aliyesimama) akifafanua
jambo kwa Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, CPA. Habibu Suluo (Wa
kwanza kulia) wakati wa Mafunzo ya Mfumo wa Upimaji wa Utendajikazi wa Watumishi
Serikalini (PEPMIS) kwa Menejimenti ya LATRA
yaliyofanyika katika
ukumbi mdogo wa Bunge jijini
Dodoma.
Menejimenti ya LATRA
ikiendelea na mafuzo ya
Mfumo wa Upimaji wa Utendaji kazi wa Watumishi Serikalini (PEPMIS) yanayoendeshwa na Ofisi ya Rais-UTUMISHI jijini Dodoma.
Baadhi ya Viongozi wa
LATRA wakifanya mafunzo kwa vitendo ya Mfumo wa Upimaji na Utendajikazi wa Watumishi
Serikalini (PEPMIS) yanayotolewa na Ofisi ya Rais-UTUMISHI
jijini Dodoma.
Afisa Utumishi
Mwandamizi, Idara ya Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Judith Abdallah akiwaelekeza washiriki wa Mafunzo ya Mfumo wa Upimaji wa Utendajikazi
wa Watumishi Serikalini (PEPMIS)
kutoka
TANESCO, REA na EWURA jijini Dodoma.
Washiriki kutoka TANESCO,
REA na EWURA wakiwa kwenye mafunzo ya Mfumo wa Upimaji wa Utendajikazi wa Watumishi
Serikalini (PEPMIS) yanayotolewa na Ofisi ya Rais-UTUMISHI katika Ukumbi wa
Jakaya Kikwete Convention jijini
Dodoma.
MHE. KIKWETE ASEMA USHIRIKIANO UTABORESHA OFISI YA NYARAKA ZANZIBAR
MHE. KIKWETE ASEMA USHIRIKIANO UTABORESHA OFISI YA NYARAKA ZANZIBAR
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza Wajumbe wa Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar waliofanya zaira leo katika Ofisi ya Rais, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Kanda ya Mashariki Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu wa namna ya kutunza na kuhifadhi nyaraka na kumbukumbu
Wajumbe wa Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakimsikiliza Mkurugenzi wa Vituo vya Kumbukumbu, Gasper Kileo wakati akiwaonesha baadhi ya Nyaraka na Kumbukuku muhimu zinazopatikana katika Ofisi hiyo leo wakati walipotembelea Ofisi ya Rais, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Kanda ya Mashariki Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu wa namna ya kutunza na kuhifadhi nyaraka na kumbukumbu
Mwenyekiti wa Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi
Zanzibar, Mhe. Machano Said akiwa kwenye picha
na baadhi ya wajumbe wa timu ya menejimenti ya Ofisi ya Rais, Idara ya
Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa pamoja na Wajumbe wa Kamati hiyo ya
Baraza la Wawakilishi
Zanzibar mara baada ya kufanya
ziara katika Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa,
Kanda ya Mashariki Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujifunza na kubadilishana
uzoefu wa namna ya kutunza na kuhifadhi nyaraka na kumbukumbu, wa pili kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete
Mkurugenzi Mkuu
Ofisi ya Rais, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Firmin
Msiangi akiwaonesha Wajumbe wa Kamati
ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa
Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi
Zanzibar baadhi ya Nyaraka muhimu zinazopatikana katika
Ofisi ya Rais, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Kanda ya
Mashariki Jijini Dar es Salaam wakati
Wajumbe wa Kamati hiyo wakati wakifanya ziara kwa lengo la kujifunza na kubadilishana
uzoefu wa namna ya kutunza na kuhifadhi nyaraka na kumbukumbu.
Naibu Waziri Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Mkurugenzi Mkuu
Ofisi ya Rais, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Firmin Msiangi
mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Rais, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka
za Taifa, Kanda ya Mashariki Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kukutana na Wajumbe wa Kamati ya Kusimamia Ofisi za
Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la
Wawakilishi Zanzibar waliofanya ziara leo Jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akiangalia baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar baadhi ya hotuba ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere aliyoitoa wakati wa harakati za kudai uhuru wa Tanganyika wakati Wajumbe walipofanya ziara leo ya kutembelea Ofisi ya Rais, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Kanda ya Mashariki Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu wa namna ya kutunza na kuhifadhi nyaraka na kumbukumbu,