Na. Veronica Mwafisi-Iringa
Tarehe 20 Februari, 2022
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Jenista Mhagama, amewataka Wataalam wanaotengeneza Mfumo mpya wa Usimamizi wa
Utendaji Kazi kwa Watumishi wa Umma kuzingatia maelekezo ya Mhe. Rais Samia
Suluhu Hassan ya kujenga mfumo rafiki na wenye uhalisia kati ya mtumishi
anayefanyiwa na anayefanya tathmini ili kuleta tija kwa taifa.
Waziri
Jenista ametoa maelekezo hayo wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Iringa ya
kukagua maendeleo ya ujenzi wa mfumo mpya wa Usimamizi wa Utendaji Kazi kwa
Watumishi wa Umma ambao umeanza kutekelezwa hivi karibuni na wataalam wa ndani
kufuatia maelekezo ya Mhe. Rais ya kuubadilisha Mfumo wa awali wa Utendaji Kazi na Tathmini katika Ngazi
ya Mtumishi (OPRAS) ambao alikuwa haridhishwi nao
kiutendaji.
Pamoja
na maelekezo ya Mhe. Rais, Mhe. Jenista amewataka wataalam hao kujenga mfumo
utakaochochea uwajibikaji wa hiari kwa kila mtumishi badala ya kufanya kazi kwa
mazoea na kwa kulazimishwa.
“Tujenge
mfumo ambao kila mtumishi wa umma ataona fahari ya kufanyiwa tathmini kwa
kuwajibika kwake kikamilifu na ajione yeye mwenyewe kuwa ni sehemu ya
utekelezaji wa majukumu ya taifa.” Mhe. Jenista amesisitiza.
Mhe.
Jenista ameongeza kuwa, mfumo mpya wa Usimamizi wa Utendaji Kazi kwa Watumishi
wa Umma unaojengwa hivi sasa unatakiwa kuwa chachu kwa watumishi wa umma
kupenda kufanyiwa tathmini kwa utendaji
kazi wao mzuri ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada kubwa anazozifanya Mhe.
Rais Samia Suluhu Hassan za kutafuta rasilimali fedha kwa lengo la kuleta
mageuzi makubwa ya kiuchumi.
“Mhe.
Rais amekuwa na jitihada kubwa katika kutafuta rasilimali fedha, hivyo tujenge
mfumo ambao watumishi wenyewe watajikuta wanapenda
kutekeleza majukumu yao
kikamilifu ili kuitendea
haki rasilimali fedha anayoitafuta Mhe. Rais kwa lengo la kuleta matokeo chanya katika nchi yetu” Mhe.
Jenista amesisitiza.
Mhe.
Jenista ameipongeza Menejimenti ya Ofisi yake kwa kuzingatia maelekezo yake ya
kuunda timu ya wataalam ya kujenga mfumo huo na kuielekeza timu hiyo kukusanya
maoni kutoka kwa wadau mbalimbali ili kuboresha zaidi mfumo huo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama
akizungumza na timu ya wataalam wanaoandaa mfumo mpya wa Usimamizi wa Utendaji
Kazi kwa Watumishi wa Umma wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani
Iringa ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mfumo huo. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya Mikataba ya Utendaji Kazi
Serikalini, Bw. Hassan Kitenge na kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya
TEHAMA Serikalini, Bw. Priscus Kiwango.
Mkurugenzi wa Idara ya Mikataba ya
Utendaji Kazi Serikalini, Bw. Hassan Kitenge akitoa neno la utangulizi kabla ya
kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama kuzungumza na timu ya wataalam wanaoandaa
mfumo mpya wa Usimamizi wa Utendaji Kazi kwa Watumishi wa Umma wakati
wa ziara yake ya kikazi Mkoani Iringa ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mfumo
huo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akiwa na
timu ya wataalam wanaoandaa mfumo mpya wa Usimamizi wa Utendaji Kazi kwa Watumishi
wa Umma wakati
wa ziara yake ya kikazi Mkoani Iringa ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mfumo
huo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama
akisikiliza maelezo mafupi ya namna ya kujaza fomu iliyokuwa ikitumika awali ya Utendaji Kazi na Tathmini katika Ngazi ya
Mtumishi (OPRAS) wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Iringa ya
kukagua maendeleo ya ujenzi wa mfumo mpya wa Usimamizi wa Utendaji
Kazi kwa Watumishi wa Umma.
Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA
Serikalini, Bw. Priscus Kiwango (katikati) akimuelezea Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama
namna mfumo mpya wa Usimamizi wa Utendaji Kazi kwa Watumishi wa Umma utakavyokuwa
ukifanya kazi wakati Waziri huyo alipowatembelea kuona maendeleo ya ujenzi wa
mfumo huo Mkoani Iringa.
Mmoja wa timu ya wataalam wanaoandaa
Mfumo mpya wa Usimamizi wa Utendaji Kazi kwa Watumishi wa Umma, Bw. Michael
Moshiro (wakwanza kulia) kutoka Chuo cha Mipango Dodoma akitoa maoni yake
kuhusu ujenzi wa mfumo huo mpya kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama wakati
wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo Mkoani Iringa iliyolenga kukagua maendeleo ya
ujenzi wa mfumo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akiwa
katika picha ya pamoja na timu ya wataalam wanaoandaa mfumo mpya wa Usimamizi
wa Utendaji Kazi kwa Watumishi wa Umma wakati wa ziara yake ya kikazi
Mkoani Iringa ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mfumo huo.
No comments:
Post a Comment