Tuesday, June 27, 2017

KATIBU MKUU - UTUMISHI AHITIMISHA MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2017 KWA KUKUTANA NA WATENDAJI WA MKOA WA SIMIYU NA KUTEMBELA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI MEATU.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (kushoto) akipata maelezo ya usindikaji maziwa kutoka kwa Mthibiti Ubora wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bw. Gerald Baruti alipotembelea Kiwanda cha kusindika Maziwa (Meatu Milk) kilichoanzishwa na vikundi vya vijana kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Meatu.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akiongea na Watendaji wa Mkoa wa Simiyu (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi na watumishi hao ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017. Kushoto kwake ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini na kulia kwake ni Mkurugenzi wa Sera, Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mathias Kabunduguru.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (Wa tatu kulia), akifuatilia taarifa ya utekelezaji iliyokuwa ikiwasilishwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (Wa pili kulia) kabla ya kukutana na Watendaji wa Mkoa wa Simiyu ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Sera, Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mathias Kabunduguru.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, Bw. Mariano Mwanyigu akitoa maoni wakati wa kikao kazi na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017.

Thursday, June 22, 2017

“NIDHAMU IWE NAMBA MOJA KATIKA UTUMISHI WA UMMA” DKT NDUMBARO



Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akisisitiza jambo kwa Watendaji na watumishi wa Mkoa wa Mwanza wakati wa kikao kazi na watumishi hao ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro, akifuatilia taarifa ya utekelezaji ya Mkoa wa Mwanza iliyokuwa ikiwasilishwa na Katibu Tawala Msaidizi Rasilimaliwatu wa Mkoa wa Mwanza, Bw. Projestus Rubanzibwa (hayupo pichani) alipokutana na Watendaji wa Sekretarieti ya mkoa wa Mwanza ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017. 

Sehemu ya Watendaji na Watumishi wa Mkoa wa Mwanza wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa kikao kazi na watumishi hao ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017. 

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro ameelekeza suala la nidhamu katika Utumishi wa Umma ni namba moja na lipewe uzito unaostahili ili kujenga Utumishi wa Umma wenye uadilifu.
Dkt. Ndumbaro aliyasema hayo wakati akizungumza na Watendaji na Watumishi wa Umma mikoa ya Singida, Shinyanga na Mwanza ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017.

KATIBU MKUU-UTUMISHI AWATAKA WAAJIRI KUFANYA MABORESHO YA TAARIFA ZA WATUMISHI MARA TU MABADILIKO YANAPOTOKEA ILI KUWA NA TAARIFA SAHIHI ZA KIUTUMISHI

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (wa kwanza kulia), akifuatilia taarifa ya utekelezaji ya Mkoa wa Shinyanga iliyokuwa ikiwasilishwa na Katibu Tawala Msaidizi Rasilimaliwatu wa Mkoa wa Shinyanga, Bw. Alfred Shayo (aliyesimama) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Sera, Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mathias Kabunduguru.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akisisitiza jambo kwa Watendaji na watumishi wa Mkoa wa Shinyanga wakati wa kikao kazi na watumishi hao ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017. Kushoto kwake ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Bw. Albert Msovela na kulia ni Mkurugenzi wa Sera, Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mathias Kabunduguru.

Sehemu ya Watendaji na Watumishi wa Mkoa wa Shinyanga wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa kikao kazi na watumishi hao ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017.

Katibu Msaidizi Tume ya Utumishi wa Walimu Wilaya ya Kahama, Bw. Bashemela Seif, akitoa maoni wakati wa kikao kazi cha Watendaji na Watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Shinyanga na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017.

Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Bw. Stephen Magoiga, akiwasilisha hoja wakati wa kikao kazi cha Watendaji na Watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Shinyanga na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017.

Afisa Tawala Mwandamizi kutoka Ofisi ya Rais – Utumishi, Bw. Leonard Tumua, akifafanua jambo kwa Watendaji na watumishi wa Mkoa wa Shinyanga wakati wa kikao kazi na watumishi hao ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017. Wa kwanza Kushoto kwake ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro na katikati ni Mkurugenzi wa Sera, Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mathias Kabunduguru.

Mkurugenzi wa Sera, Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mathias Kabunduguru. akifafanua jambo kwa Watendaji na watumishi wa Mkoa wa Shinyanga wakati wa kikao kazi na watumishi hao ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro na Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Bw. Albert Msovela.

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAFANYA MKUTANO KAZI NA WATENDAJI WA MKOA WA RUVUMA KUADHIMISHA YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2017

Katibu Tawala, Mkoa wa Ruvuma Bw. Hassan Bendeyeko akiwasilisha taarifa ya utendaji kuhusu mkoa wake wakati wa mkutano kazi uliowahusisha watendaji wa mkoa wa Ruvuma na Ofisi ya Rais - Utumishi wakati wa  Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017.

Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za mkoa wa Ruvuma wakijitambulisha wakati wa mkutano kazi uliowakutanisha na watendaji wa Ofisi ya Rais-Utumishi wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017 mkoani Ruvuma.

Sehemu ya watendaji wa Serikali mkoani Ruvuma wakisikiliza  hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma  na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) kuhusu uwajibikaji katika Utumishi wa Umma , iliyosomwa kwa niaba yake na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Issa Ngimba  mkoani Ruvuma ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2017.

Baadhi ya watendaji na Watumishi wa Umma mkoani Ruvuma wakiwa katika mkutano kazi uliowakutanisha na watendaji wa Ofisi ya Rais-Utumishi  wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017  mjini Songea.


Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma,  Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Issa Ngimba akisoma hotuba kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) ya kuhimiza uwajibikaji kwa viongozi na watumishi wa umma mkoani Ruvuma wakati wa kikao kazi cha  Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2017.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Bw. Hassan Bendeyeko akiwa na viongozi wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakati wa mkutano kazi wa Ofisi ya Rais-Utumishi na watendaji wa mkoa wa Ruvuma ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017.


Afisa Utumishi Mwandamizi wa Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Bw. Thadei Kimati akifafanua kuhusu taratibu zinazohusu masuala ya kiutumishi   kwa Watendaji na  watumishi wa umma mkoani Ruvuma  ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2017.