Thursday, November 17, 2016

MHE. KAIRUKI ATEMBELEA MRADI WA NYUMBA ZA BEI NAFUU KWA AJILI YA WATUMISHI WA UMMA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akisikiliza maelezo ya mradi wa nyumba za bei nafuu zilizojengwa kwa ajili ya watumishi wa umma kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Company, Dkt. Fred Msemwa (kulia).

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akitoa maelekezo ya namna ya kuboresha ujenzi wa nyumba za mradi wa bei nafuu zinazojengwa kwa ajili ya watumishi wa umma. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Company, Dkt. Fred Msemwa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Mhe. Hashim Mgandilwa wakati wa ziara ya kikazi ya Mhe. Kairuki ya kukagua mradi wa nyumba za bei nafuu zilizojengwa kwa ajili ya watumishi wa umma eneo la Gezaulole Kigamboni.

Baadhi ya Waandishi wa Habari na wafanyakazi wa Watumishi Housing Company wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo ya kukagua mradi wa nyumba za bei nafuu zilizojengwa kwa ajili ya watumishi wa umma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akiwa katika moja ya mradi wa nyumba za bei nafuu zinazojengwa kwa ajili ya watumishi wa umma. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Company, Dkt. Fred Msemwa akitoa maelezo kuhusu mradi huo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na Vyombo mbalimbali vya habari kuhusu mradi wa nyumba za bei nafuu zinazojengwa kwa ajili ya watumishi wa umma wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua mradi wa nyumba hizo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akipewa maelezo na Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Company, Dkt. Fred Msemwa kuhusu mradi wa nyumba za bei nafuu za Magomeni Dar es Salaam zinazojengwa kwa ajili ya watumishi wa umma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akisikiliza maelezo ya Mkandarasi Mshauri wa mradi wa nyumba za bei nafuu kwa Watumishi wa Umma, Bw. Edmund Kahabuka zilizopo eneo la Bunju B.

No comments:

Post a Comment