JAMHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI
YA RAIS
Simu ya Upepo
"UTUMISHI", DSM. Menejimenti ya Utumishi wa Umma,
Simu: 2118531/4 au
2122908 Utumishi
House,
Barua Pepe:permsec@estabs.go.tz 8
Barabara ya Kivukoni,
11404 Dar
es Salaam.
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
WIKI YA UADILIFU
Ofisi
ya Rais –Menejimenti ya Utumishi wa Umma imenza Wiki ya Uadilifu katika
Utumishi wa Umma.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. HAB Mkwizu leo ameongoza zoezi la kutoa
Ahadi za Uadilifu kwa viongozi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa
Umma.
Bw. Mkwizu alisema zoezi
hilo ni endelevu na muhimu sana kwa Watumishi wa Umma hapa nchini.
“Tuishi viapo vyetu
tulivyoahidi leo” Bw. Mkwizu alisisitiza na kusema ahadi hiyo iwe sehemu ya
kazi ambapo inahusisha ujazaji wa fomu
ya Ahadi ya Uadilifu kwa Watumishi wa Umma (PL.4), ambayo mhusika husaini kwa
cheo alichonacho na Mtendaji Mkuu wa Taasisi yake.
Pamoja na masuala mengine,
fomu hiyo itatumika pia kwa Watumishi wapya katika Utumishi wa Umma, mtumishi
akibadilishwa cheo au kuhama ofisi.
Moja ya malengo ya fomu hiyo
ni kuendeleza dhana ya Uwajibikaji, Usikivu kwa Umma na kuzingatia weledi
katika Utumishi wa Umma. Fomu ya Ahadi ya Uadilifu inapatikana katika Tovuti ya
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma yenye anuani,
www.utumishi.go.tz.
Imetolewa na Kitengo
cha Mawasiliano Serikalini
Kny: KATIBU MKUU -
UTUMISHI