Thursday, September 4, 2014

WATANZANIA 30 WAPATA FURSA ZA KUSOMA SHAHADA ZA UZAMILI NCHINI JAPANI

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma  Bw.George D. Yambesi akiongea na Watanzania (hawapo pichani) waliopata ufadhili wa kusoma Shahada za Uzamili nchini Japani katika hafla fupi ya kuwaaga iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Sehemu ya Watanzania waliopata ufadhili wa kusoma Shahada za Uzamili nchini Japani.

Balozi wa Japani nchini Tanzania Bw. Masaki Okada akiwahutubia Watanzania (hawapo pichani) waliopata nafasi ya kusoma nchini Japani katika hafla fupi ya kuwaaga iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma  Bw. George D. Yambesi (katikati) akiongea na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam katika hafla fupi ya kuwaaga Watanzania waliopata fursa ya kusoma Shahada za Uzamili nchini Japani iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi  wa Umma Bw.George D. Yambesi (aliyetangulia) pamoja na Balozi wa Japani nchini Tanzania Bw.Masaki Okada wakiagana na sehemu ya Watanzania waliopata nafasi ya kusoma nchini Japani.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George D. Yambesi (katikati) ,Balozi wa Japani nchini Tanzania Bw. Masaki Okada (kushoto) na  Mwakilishi Mkazi Mwandamizi wa JICA Bw. Kuniako Amatsu katika picha ya pamoja na Watanzania waliopata fursa ya kusoma Shahada za Uzamili nchini Japani baada ya hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

1 comment:

  1. Nakupongezeni nyote mliopata fursa ya kusoma Japan. Mtuombee sisi pia kwani tuna nia hio!

    ReplyDelete