Friday, September 26, 2014

TIMU ZA NETIBOLI,KAMBA NA BAO ZA UTUMISHI ZAAGWA LEO

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais -Utumishi Bw.HAB Mkwizu akizungumza na timu za Ofisi ya Rais-Utumishi wakati wa hafla fupi ya kuaga timu hizo zinazoenda kushiriki mashindano ya SHIMIWI 2014 mjini Morogoro.Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw.Aloyce Msigwa (aliyesimama) akizungumza katika hafla fupi ya kuaga timu za Ofisi ya Rais-Utumishi zinazoenda kushiriki mashindano ya SHIMIWI 2014 mjini Morogoro. 
Mwenyekiti wa Michezo Ofisi ya Rais-Utumishi Bw.Lumuli Mtaki (aliyesimama)akitoa shukrani kwa uongozi wa Ofisi ya Rais-Utumishi kwa kufanikisha timu za Utumishi kwenda kwenye mashindano ya SHIMIWI 2014 mjini Morogoro.
Baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo Ofisi ya Rais-Utumishi wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw.HAB Mkwizu (hayupo pichani) wakati wa hafla fupi ya kuaga timu za Ofisi ya Rais-Utumishi zinazoenda kushiriki mashindano ya SHIMIWI 2014 mjini Morogoro

No comments:

Post a Comment