Thursday, December 7, 2023

ZIARA YA MHE. WAZIRI SIMBACHAWENE KATIKA OFISI YA IDARA YA KUMBUKUMBU NA NYARAKA ZA TAIFA

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na baadhi ya watumishi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa wakati alipofanya ziara fupi katika ofisi hizo Jijini Dar es Salaam.

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene akisoma moja ya nyaraka muhimu alizozikuta katika Ofisi za Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa wakati wa ziara yake ya kikazi katika ofisi hizo Jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene akipitia moja ya vitabu alivyovikuta katika Ofisi za Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa wakati wa ziara yake katika ofisi hizo Jijini Dar es Salaam.





Mkurugenzi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa Bw. Firimin Msiangi na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Bi. Editha Beda wakifuatilia kwa makini maelekezo ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene (Hayupo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi katika ofisi hizo Jijini Dar es Salaam.




Tuesday, December 5, 2023

Monday, December 4, 2023

UZINDUZI WA RIPOTI YA AWALI YA KUTATHMINI KIPINDI CHA PILI CHA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI TANZANIA


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene akimkabidhi Katibu Mkuu Ofisi ya Rais IKULU Bw. Mululi Mahendeka Ripoti ya Awali ya Kutathmini Kipindi cha Pili cha Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Tanzania baada ya uzinduzi wa ripoti hiyo katika ukumbi wa NBS Jijini Dodoma. 



Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Juma Mkomi akiteta jambo na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais IKULU Bw. Mululi Mahendeka kabla ya uzinduzi wa ripoti ya Awali ya Kutathmini Kipindi cha Pili cha Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Tanzania katika ukumbi wa NBS Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Juma Mkomi akitoa neno la shukurani baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene kuzindua Ripoti ya Awali ya Kutathmini Kipindi cha Pili cha Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Tanzania katika ukumbi wa NBS Jijini Dodoma.