Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bi. Dorothy Mwaluko akizungumza wakati
wa hafla fupi ya kumuaga aliyekuwa Mkurugenzi wa Sera, Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw.
Mathias Kabunduguru ambaye kwa sasa ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. Mathias Kabunduguru, ambaye alikuwa
Mkurugenzi wa Sera, Ofisi ya Rais-Utumishi akizungumza na watumishi wa Ofisi ya
Rais-Utumishi (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika
katika ukumbi wa mikutano wa Utumishi.
Baadhi ya Watumishi wa Ofisi
ya Rais-Utumishi wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Bw. Mathias Kabunduguru, (hayupo pichani) ambaye alikuwa
Mkurugenzi wa Sera, Ofisi ya Rais-Utumishi wakati wa hafla fupi ya kumuaga
iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Utumishi.
Naibu Katibu Mkuu,
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. Mathias Kabunduguru, ambaye
alikuwa Mkurugenzi wa Sera, Ofisi ya Rais-Utumishi akimkabidhi nyaraka za kiutendaji Kaimu
Mkurugenzi wa Sera, Bi Agnes Meena wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika
katika ukumbi wa mikutano wa Utumishi.
Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bi. Dorothy Mwaluko pamoja na Naibu
Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. Mathias
Kabunduguru wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya
Rais-Utumishi baada ya hafla fupi ya kumuaga Bw. Mathias Kabunduguru ambaye
alikuwa Mkurugenzi wa Sera Ofisi ya Rais-Utumishi.