Tuesday, November 24, 2026

KAMATI YA UKAGUZI YAPATIWA MAFUNZO

 Na Antonia Mbwambo-Dodoma

Tarehe 24 Novemba, 2026

Wajumbe wa Kamati mpya ya Ukaguzi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wamepatiwa mafunzo kuhusu Muundo na Majukumu ya Ofisi hiyo ili kuwawezesha kutekeleza wajibu wao kwa ufanisi.

Mafunzo hayo yametolewa Novemba 24, 2026 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hiyo, Mtumba jijini Dodoma, na kufunguliwa na Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji wa Rasilimaliwatu Bi. Leila Mavika, kwa niaba ya Katibu Mkuu-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi.

Bi. Mavika amewataka washiriki kuzingatia Miongozo ya Ukaguzi na kutumia maarifa wanayoyapata kuboresha utendaji wa Kamati.

Amesema, kufahamu muundo na maeneo ya kiutendaji kutawasaidia kutimiza wajibu wao ipasavyo na kuimarisha usimamizi wa shughuli za Taasisi.

“Ninawahimiza mjenge msingi imara wa utendaji tangu mwanzo kwa kuzingatia taratibu zinazowaongoza, ili kamati iweze kutimiza matarajio yaliyowekwa na kuchangia usimamizi bora wa Ofisi,” amesema Bi. Mavika.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Bw. Dickson Austin, akizungumza kwa niaba ya wajumbe, amemshukuru Bi. Mavika kwa utangulizi na maelekezo aliyoyatoa na kuahidi kutumia elimu waliyopata kutekeleza wajibu wao kwa weledi na uadilifu.

 

Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji wa Rasilimaliwatu Bi. Leila Mavika akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Ukaguzi ya Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (hawapo pichani) wakati Mkurugenzi huyo akimwakilisha Katibu Mkuu UTUMISHI Bw. Juma Mkomi katika ufunguzi wa mafunzo ya kamati hiyo Mtumba jijini Dodoma





Mwenyekiti wa Kamati Kamati mpya ya Ukaguzi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Dickson Austin, akimshukuru Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji wa Rasilimaliwatu Bi. Leila Mavika (hayupo pichani) kwa maelekezo aliyoyatoa wakati wa mafunzo na kuahidi kutumia elimu waliyopata kutekeleza wajibu wao kwa weledi na uadilifu.


Wajumbe wa Sekretarieti kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakifuatilia mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji yaliyotolewa kwa Kamati ya Ukaguzi ya Ofisi hiyo Mtumba Jijini Dodoma


Mkaguzi wa ndani mwandamizi kutoka Wizara ya fedha Bw. Felix Kapesula akitoa wasilisho kuhusu majukumu na wajibu wa kamati ya Ukaguzi ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wajumbe wa kamati hiyo Novemba 24, 2026 jijini Dodoma
  

Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Dickson Austin akifafanua jambo kwa Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji wa Rasilimaliwatu wa Ofisi hiyo Bi. Leila Mavika (aliyekaa mbele) wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wanakamati hao yaliyofanyika Novemba 24, 2026 Jijini Dodoma


Katibu wa Kamati ya Ukaguzi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Edwin Bilikundi akieleza jambo , wakati wa mafunzo kwa kwa wajumbe wa kamati hiyo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyofanyika Novemba 24, 2026 Jijini Dodoma

Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji wa Rasilimaliwatu Bi. Leila Mavika,akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa kamati ya Ukaguzi ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawala Bora, mara baada ya Mkurugenzi huyo kufungua mafunzo ya uelewa kuhusu Muundo na majukumu ya Ofisi hiyo,Novemba 24, 2026 Mtumba, Dodoma

Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji wa Rasilimaliwatu Bi. Leila Mavika,akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa kamati ya Ukaguzi ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawala Bora, mara baada ya Mkurugenzi huyo kufungua mafunzo ya uelewa kuhusu Muundo na majukumu ya Ofisi hiyo,Novemba 24, 2026 Mtumba, Dodoma



Mkaguzi wa ndani mwandamizi kutoka Wizara ya fedha Bw. Felix Kapesula akitoa wasilisho kuhusu majukumu na wajibu wa kamati ya Ukaguzi ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wajumbe wa kamati hiyo Novemba 24, 2026 jijini Dodoma


Wajumbe wa kamati ya Ukaguzi ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakifuatilia mafunzo mafunzo kuhusu Muundo na Majukumu ya Ofisi hiyo yaliyofanyika tarehe 24 Novemba, 2026 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi hiyo, Jijini Dodoma


Mkurugenzi wa Kitengo cha Ukaguzi wa ndani Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Martha Wililo akitoa neno la utangulizi kwa mwakilishi wa Katibu Mkuu-UTUMISHI ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji wa Rasilimaliwatu Bi. Leila Mavika (aliyekaa mbele) kabla ya Mkurugenzi huyo kufungua mafunzo ya kuwajengea uwezo Kamati ya Ukaguzi ya Ofisi hiyo, Mtumba Jijini Dodoma

Viongozi na wajumbe wa kamati ya Ukaguzi ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakifuatilia mafunzo mafunzo kuhusu Muundo na Majukumu ya Ofisi hiyo yaliyofanyika tarehe 24 Novemba, 2026 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi hiyo, Jijini Dodoma


Mkurugenzi wa Kitengo cha Ukaguzi wa ndani Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Martha Wililo akitoa neno la shukrani kwa mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji wa Rasilimaliwatu Bi. Leila Mavika, (hayupo pichani) kwa kufungua mafunzo hayo Novemba 24, 2026 Jijini Dodoma

Bottom of Form

 


Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji wa Rasilimaliwatu Bi. Leila Mavika,akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kamati ya Ukaguzi ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawala Bora, mara baada ya Mkurugenzi huyo kufungua mafunzo ya uelewa kuhusu Muundo na majukumu ya Ofisi hiyo,Novemba 24, 2026 Mtumba, Dodoma

MHE.RIDHIWANI AFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI MBALIMBALI

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mhe. Halima Okash, DED wa Chalinze Bw. Ramadhani Possi (Suti ya Kaki) na DED wa Bagamoyo Bw. Shauri Serenda ofisini kwake Mtumba, Dodoma tarehe 24 Novemba, 2026.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze Bw. Ramadhani Possi ofisini kwake Mtumba, Dodoma tarehe 24 Novemba, 2026.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze Bw. Shauri Serenda Msuya ofisini kwake Mtumba, Dodoma tarehe 24 Novemba, 2026.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mhe. Halima Okash ofisini kwake Mtumba, Dodoma tarehe 24 Novemba, 2026.

Monday, November 23, 2026

WITO WATOLEWA KWA PSSSF KUWEZESHA WATUMISHI KUWEKEZA KABLA YA KUSTAAFU.

 Na. Antonia Mbwambo-Dodoma

Tarehe 23 Novemba, 2026

Mwakilishi wa Katibu Mkuu-UTUMISHI, ambaye ni Mkurugenzi wa Mipango wa Ofisi hiyo, Bw. Cosmas Ngangaji, ameiomba PSSSF kuimarisha utoaji wa elimu ya hifadhi ya jamii kwa watumishi na kuangalia uwezekano wa kuwawezesha wanachama kupata sehemu ya michango yao katika umri wa miaka 55 ili kuwapa nafasi ya kuwekeza na kupata uzoefu katika uwekezaji huo kabla ya kustaafu.

Bw. Ngangaji ametoa wito huo alipokuwa akimwakilisha Katibu Mkuu-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi, katika kuhitimisha mafunzo ya uelewa kuhusu huduma zinazotolewa na PSSSF kwa watumishi wa Ofisi hiyo, yaliyofanyika tarehe 23 Novemba 2026 katika eneo maalumu la Ofisi hiyo, Mtumba jijini Dodoma.

Amesisitiza kuwa sehemu ya michango hiyo atakayopewa mwanachama itamsaidia kujengea uwezo wa kiuchumi na kuwa na vyanzo endelevu vya mapato baada ya kumaliza utumishi wa umma na kuanza uwekezaji katika kipindi hicho.

“Endeleeni kutoa elimu kwa wanachama kuhusu manufaa ya hifadhi ya jamii ili waweze kufanya uamuzi sahihi kabla ya kustaafu. Elimu hii itawasaidia watumishi wa umma kujenga msingi imara wa maisha yao ya kiuchumi baada ya utumishi,” alisema Bw. Ngangaji.

Katika mafunzo hayo, Meneja wa Kanda ya Kati wa PSSSF, Bw. Lulyalya Sayi, ameeleza kuwa Mfuko huo ulianzishwa kwa lengo la kutoa huduma za hifadhi ya jamii kwa watumishi wa umma Tanzania Bara. Hivyo, amesisitiza waajiri na wanachama kutekeleza wajibu wao wa kuwasilisha na kufuatilia michango yao mtawalia.

Kwa upande wake, Afisa Matekelezo Mwandamizi wa PSSSF, Bw. Philipo John, amesema matumizi ya TEHAMA yamerahisisha huduma za Mfuko, ikiwemo usajili, uwasilishaji wa michango na madai, uhakiki wa wastaafu na ulipaji wa mafao kwa njia za kielektroniki, hivyo kuwawezesha wanachama kupata huduma bila kufika ofisini.


Mkurugenzi wa Mipango wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Cosmas Ngangaji,akimwakilisha Katibu Mkuu-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi, katika kuhitimisha mafunzo ya uelewa kuhusu huduma zinazotolewa na PSSSF kwa watumishi wa Ofisi hiyo, yaliyofanyika tarehe 23 Novemba 2026 katika eneo maalumu la Ofisi hiyo, Mtumba jijini Dodoma.


Baadhi ya Wakurugenzi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, walimsikiliza Mkurugenzi wa Mipango wa Ofisi hiyo Bw. Cosmas Ngangaji (hayupo pichani) wakati akihitimisha mafunzo kuhusu huduma zitolewazo na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma leo tarehe 23 Novemba Mtumba Jijini Dodoma Novemba 23, 2026 katika eneo maalumu la Ofisi hiyo Mtumba jijini Dodoma


Baadhi ya Watumishi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakimsikiliza Mwakilishi wa Katibu Mkuu-UTUMISHI, ambaye ni Mkurugenzi wa Mipango wa Ofisi hiyo, Bw. Cosmas Ngangaji wakati akihitimisha mafunzo kuhusu huduma zitolewazo na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma leo tarehe 23 Novemba Mtumba Jijini Dodoma


Baadhi ya Watumishi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakimsikiliza Mwakilishi wa Katibu Mkuu-UTUMISHI, ambaye ni Mkurugenzi wa Mipango wa Ofisi hiyo, Bw. Cosmas Ngangaji wakati akihitimisha mafunzo kuhusu huduma zitolewazo na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma leo tarehe 23 Novemba Mtumba Jijini Dodoma


Mkurugenzi wa Mipango wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Cosmas Ngangaji,akimwakilisha Katibu Mkuu-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi, katika kuhitimisha mafunzo ya uelewa kuhusu huduma zinazotolewa na PSSSF kwa watumishi wa Ofisi hiyo, yaliyofanyika tarehe 23 Novemba 2026 katika eneo maalumu la Ofisi hiyo, Mtumba jijini Dodoma.

Baadhi ya Wakurugenzi na Watumishi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, walimsikiliza Afisa Matekelezo Mwandamizi wa PSSSF, Bw. Philipo John, akitoa wasilisho kuhusu matumizi ya TEHAMA yalivyorahisisha utoaji wa huduma za Mfuko huo Novemba 23, 2026 katika eneo maalumu la Ofisi hiyo Mtumba jijini Dodoma

Baadhi ya Wakurugenzi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, walimsikiliza Mkurugenzi wa Mipango wa Ofisi hiyo Bw. Cosmas Ngangaji (hayupo pichani) wakati akihitimisha mafunzo kuhusu huduma zitolewazo na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma leo tarehe 23 Novemba Mtumba Jijini Dodoma Novemba 23, 2026 katika eneo maalumu la Ofisi hiyo Mtumba jijini Dodoma


Baadhi ya Watumishi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakimsikiliza Mwakilishi wa Katibu Mkuu-UTUMISHI, ambaye ni Mkurugenzi wa Mipango wa Ofisi hiyo, Bw. Cosmas Ngangaji wakati akihitimisha mafunzo kuhusu huduma zitolewazo na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma leo tarehe 23 Novemba Mtumba Jijini Dodoma

Meneja wa Kanda ya Kati wa PSSSF, Bw. Lulyalya Sayi akizungumza na Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI kuhusu huduma zitolewazo na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma Novemba 23, 2026 wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji watumishi hao ambayo hufanyika kila jumatatu ya wiki katika eneo maalumu la Ofisi hiyo Mtumba jijini Dodoma



 

Monday, November 16, 2026

NAIBU WAZIRI MHE. QWARAY AWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUZUIA UDANGANYIFU

 Na. Lusungu Helela- Arusha

 Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray amewataka watumishi wa umma kushiriki kikamilifu katika kuzuia udanganyifu na kulinda rasilimali za umma, huku akisisitiza umuhimu wa kushirikiana na wataalamu wa udhibiti wa vitendo hivyo.

 Mhe. Qwaray ameyasema hayo leo, Novemba 16, 2026, jijini Arusha, wakati akifungua mkutano na kongamano la mwaka la Taasisi ya Wataalamu wa Udhibiti wa Udanganyifu Tanzania (ACFE).

 Amesema mapambano dhidi ya udanganyifu hayapaswi kuachiwa wakaguzi pekee, bali kila mtumishi wa umma ana wajibu wa kuhakikisha rasilimali za umma zinatumika kwa kuzingatia sheria, taratibu na maadili ya utumishi.

 “Kila mtumishi wa umma ni mlinzi wa rasilimali za umma. Hivyo, jukumu la kuzuia udanganyifu si la wakaguzi pekee, bali ni la kila mtumishi kwa kuzingatia nafasi, mamlaka na wajibu wake katika taasisi,” amesema Mhe. Qwaray.

 Amesisitiza umuhimu wa maafisa utumishi, maafisa rasilimali watu na vyama vya kitaaluma kushirikiana na ACFE Tanzania katika kuwajengea uwezo watumishi wa kubaini viashiria vya udanganyifu na kuimarisha maadili mahali pa kazi.

 Mhe. Qwaray amesema utaalamu wa ACFE unaweza kusaidia kuimarisha mifumo ya upimaji wa utendaji kazi na kuzuia upotoshaji wa takwimu, ili taarifa zinazowasilishwa na taasisi za umma ziakisi matokeo halisi ya utekelezaji wa majukumu.

 Katika hatua nyingine, ameikaribisha ACFE kuwasilisha mapendekezo ya kitaalamu kwa Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora kuhusu maeneo yanayoweza kujengewa ushirikiano katika kuimarisha utendaji kazi, nidhamu na maadili ya watumishi wa umma.

 Akizungumzia maendeleo ya teknolojia, Mhe. Qwaray amesema matumizi ya akili mnemba na fedha za kidijitali yameibua vihatarishi vipya vya udanganyifu vinavyohitaji mbinu za kisasa za udhibiti.

 “Teknolojia haiwezi kuchukua nafasi ya uadilifu wa binadamu,” amesema.

 Pia, amesisitiza umuhimu wa kujenga mazingira salama kwa watumishi na wananchi kutoa taarifa kuhusu udanganyifu bila hofu ya vitisho au kulipiziwa kisasi.

 Naye Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhandisi Keneth Nindie amesema wizara hiyo imeunda mifumo mbalimbali ya kubaini vihatarishi vya udanganyifu na inaendelea kuwajengea uwezo wakaguzi wa ndani ili kuzuia vitendo hivyo kabla ya madhara kutokea.

 Amesema ili mifumo hiyo iwe na tija, ni muhimu taasisi mbalimbali kuhakikisha zinaitumia ipasavyo.

 Kwa upande wake, Rais na Mwenyekiti wa Bodi ya ACFE Tanzania, Bw. Ali Mabrouk Juma amesema kuwa na bajeti kubwa na watumishi wa kutosha hakutoshi iwapo taasisi haina mikakati madhubuti ya kupambana na udanganyifu.

 Amesema kasi ya maendeleo ya teknolojia inahitaji taasisi kuhuisha mbinu za udhibiti na kuwajengea uwezo watumishi kutumia mifumo ya kisasa kubaini udanganyifu.

 Bw. Juma amesema ACFE haikusudii kuchukua majukumu ya taasisi nyingine, bali kuongeza nguvu katika juhudi za kupambana na udanganyifu.

 Aidha, ameiomba Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kutambua kada ya wataalamu wa udhibiti wa udanganyifu, huku akimwomba Qwaray kuwa mlezi wa taasisi hiyo.

 Kongamano hilo linafanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), likijikita katika mikakati ya kudhibiti udanganyifu katika zama za akili mnemba, takwimu na fedha za kidijitali.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray, akisisitiza umuhimu wa Maafisa Utumishi na Maafisa Rasilimali Watu kushirikiana na ACFE Tanzania katika kujenga uwezo wa watumishi wa umma wa kubaini na kudhibiti udanganyifu, wakati wa Kongamano la Mwaka la ACFE, leo, Novemba 16, 2026, jijini Arusha.



Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray, akikabidhiwa tuzo na Rais na Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Wataalamu wa Udhibiti wa Udanganyifu Tanzania (ACFE) Bw. Ali Mabrouk Juma  ikiwa ni ishara ya shukrani ya kukubali ya kuwa mlezi  wa Taasisi ya  ACFE Tanzania mara baada ya kufungua  Kongamano la Mwaka la ACFE, leo, Novemba 16, 2026, jijini Arusha

 

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray, akikabidhi tuzo kwa  Msajili wa Hazina, Zanzibar, Bw. Waheed Sanya ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wake kwa Taasisi ya ACFE Tanzania mara baada ya kufungua  Kongamano la Mwaka la ACFE, leo, Novemba 16, 2026, jijini Arusha



 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray, akisubiliwa na baadhi ya  Wadhamini  wa Kongamano la Mwaka la ACFE, mara baada ya kufungua Kongamano hilo leo, Novemba 16, 2026, jijini Arusha

Baadhi ya Washiriki wa mkutano na kongamano la mwaka la Taasisi ya Wataalamu wa Udhibiti wa Udanganyifu Tanzania (ACFE) wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray wakati akifungua Kongamano hilo leo, Novemba 16, 2026, jijini Arusha


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray, akisalimiana na baadhi ya Waandaji wa Kongamano la Mwaka la ACFE, mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kufungua Kongamano hilo leo, Novemba 16, 2026, jijini Arusha


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray, akizungumza  baadhi ya Waandaji wa Mkutano na  Kongamano la Mwaka la ACFE, mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kufungua Kongamano hilo leo, Novemba 16, 2026, jijini Arusha

 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akisaini kitabu cha wageni mara mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kufungua Mkutano na  Kongamano la Mwaka la ACFE, Novemba 16, 2026, jijini Arusha

9



 

 

Friday, November 13, 2026

WATUMISHI WA UMMA WATAKIWA KUTUMIA MFUMO WA e-WATUMISHI KWA UADILIFU NA UWAJIBIKAJI

Na. Antonia Mbwambo – Dodoma

Tarehe 13 Novemba, 2026

Wakuu wa Idara za Utumishi na Utawala, Wahasibu, Wakaguzi wa Ndani na Maafisa Utumishi na Utawala wametakiwa kutumia Mfumo wa e-Watumishi kwa uadilifu, umakini na uwajibikaji ili kuboresha usimamizi wa rasilimaliwatu na mishahara katika Taasisi za Umma.

Wito huo umetolewa na Mwakilishi wa Katibu Mkuu – UTUMISHI, ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Mipango wa Ofisi hiyo Bw. Cosmas Ngangaji, Novemba 13, 2026 wakati akifunga mafunzo kuhusu mfumo huo yaliyofanyika katika Ukumbi wa St. Gaspa jijini Dodoma.

Bw. Ngangaji amewataka washiriki kujiepusha na vitendo vya ukiukwaji wa maadili ya kazi ikiwemo uzembe, matumizi ya lugha zisizofaa, kutoa taarifa za uongo na kufanya udanganyifu, akibainisha kuwa Mfumo Mpya wa e-Watumishi una uwezo wa kurekodi na kufuatilia shughuli zote zinazofanywa na watumiaji.

“Matumizi ya Mfumo Mpya wa e-Watumishi yanapaswa kuzingatia uadilifu  na uwajibikaji kwa kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma ili kuongeza ufanisi katika usimamizi wa rasilimaliwatu na kuboresha utoaji wa huduma kwa umma,” amesema Bw. Ngangaji.

Aidha Bw. Ngangaji ameongeza kuwa mfumo huo utarahisisha upatikanaji wa huduma za kiutumishi kwani utawawezesha Maafisa Utumishi kutatua changamoto za watumishi katika Taasisi zao na kupunguza usumbufu wa kufuata huduma Ofisi ya Rais – UTUMISHI.

Katika mafunzo hayo, washiriki wamejengewa uwezo wa kutumia mfumo huo maeneo mbalimbali ikiwemo ya Ajira, Payroll, pamoja na kushughulikia masuala ya likizo, maadili na upandishaji vyeo kwa mserereko. 


Mkurugenzi wa Idara ya Mipango Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Cosmas Ngangaji, akizungumza na Washiriki wa mafunzo ya  Mfumo wa e-Watumishi (hawapo pichani) yaliyolenga kuongeza uadilifu na uwajibikaji kwa Watumishi wa umma Novemba 13, 2026 katika ukumbi wa St. Gaspar jijini Dodoma. 


                                            

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Juma Senzota akifafanua jambo wakati wa mafunzo ya Mfumo wa e-Watumishi kwa Watumishi wa Umma yaliyofanyika Novemba 13, 2026 katika ukumbi wa St. Gaspar jijini Dodoma. 


Mkurugenzi wa Idara ya Mipango Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Cosmas Ngangaji (wa pili kutoka kulia) akiwasili katika ukumbi wa St Gaspar kumwakilisha Katibu Mkuu-UTUMISHI kufunga mafunzo ya  Mfumo wa e-Watumishi Novemba 13, 2026  jijini Dodoma                                    


Baadhi ya wajumbe wa Sekretarieti kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakifuatilia mada mada za mafunzo ya e-Watumishi kwa Watumishi wa Umma yaliyofanyika Novemba 13, 2026 jijini Dodoma

Mkurugenzi wa Idara ya Mipango Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Cosmas Ngangaji (wa pili kutoka kulia aliyekaa) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya mfumo wa e-Watumishi, mara baada ya Mkurugrenzi huyo kufunga mafunzo hayo jijini Dodoma 

Mkurugenzi wa Idara ya Mipango Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Cosmas Ngangaji  (wa pili kutoka kulia aliyekaa) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa sekretarieti wa Ofisi hiyo , mara baada ya Mkurugenzi huyo kufunga mafunzo ya mfumo wa e-Watumishi jijini Dodoma 

Wakuu wa Idara za Utumishi na Utawala, Wahasibu, Wakaguzi wa Ndani na Maafisa Utumishi na Utawala wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Mipango Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Cosmas Ngangaji (hayupo pichani) wakati akifunga  mafunzo ya  Mfumo wa e-Watumishi jijini Dodoma


Wakuu wa Idara za Utumishi na Utawala, Wahasibu, Wakaguzi wa Ndani na Maafisa Utumishi na Utawala wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Mipango Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Cosmas Ngangaji (hayupo pichani) wakati akifunga  mafunzo ya  Mfumo wa e-Watumishi jijini Dodoma



Wakuu wa Idara za Utumishi na Utawala, Wahasibu, Wakaguzi wa Ndani na Maafisa Utumishi na Utawala wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Mipango Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Cosmas Ngangaji (hayupo pichani) wakati akifunga  mafunzo ya  Mfumo wa e-Watumishi jijini Dodoma


Baadhi ya wajumbe wa Sekretarieti kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakifuatilia mada mada za mafunzo ya e-Watumishi kwa Watumishi wa Umma yaliyofanyika Novemba 13, 2026 jijini Dodoma


Wakuu wa Idara za Utumishi na Utawala, Wahasibu, Wakaguzi wa Ndani na Maafisa Utumishi na Utawala wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Mipango Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Cosmas Ngangaji (hayupo pichani) wakati akifunga  
mafunzo ya  Mfumo wa e-Watumishi jijini Dodoma


Mkurugenzi wa Idara ya Mipango Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Cosmas Ngangaji (kushoto) kwa niaba ya Katibu Mkuu-UTUMISHI akimtunuku cheti cha ushiriki wa mafunzo ya e-Watumishi Afisa Utumishi kutoka halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Bw. Francis Fusi (kulia) mara baada ya kuhitimisha mafunzo hayo jijini Dodoma