Monday, November 23, 2026

WITO WATOLEWA KWA PSSSF KUWEZESHA WATUMISHI KUWEKEZA KABLA YA KUSTAAFU.

 Na. Antonia Mbwambo-Dodoma

Tarehe 23 Novemba, 2026

Mwakilishi wa Katibu Mkuu-UTUMISHI, ambaye ni Mkurugenzi wa Mipango wa Ofisi hiyo, Bw. Cosmas Ngangaji, ameiomba PSSSF kuimarisha utoaji wa elimu ya hifadhi ya jamii kwa watumishi na kuangalia uwezekano wa kuwawezesha wanachama kupata sehemu ya michango yao katika umri wa miaka 55 ili kuwapa nafasi ya kuwekeza na kupata uzoefu katika uwekezaji huo kabla ya kustaafu.

Bw. Ngangaji ametoa wito huo alipokuwa akimwakilisha Katibu Mkuu-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi, katika kuhitimisha mafunzo ya uelewa kuhusu huduma zinazotolewa na PSSSF kwa watumishi wa Ofisi hiyo, yaliyofanyika tarehe 23 Novemba 2026 katika eneo maalumu la Ofisi hiyo, Mtumba jijini Dodoma.

Amesisitiza kuwa sehemu ya michango hiyo atakayopewa mwanachama itamsaidia kujengea uwezo wa kiuchumi na kuwa na vyanzo endelevu vya mapato baada ya kumaliza utumishi wa umma na kuanza uwekezaji katika kipindi hicho.

“Endeleeni kutoa elimu kwa wanachama kuhusu manufaa ya hifadhi ya jamii ili waweze kufanya uamuzi sahihi kabla ya kustaafu. Elimu hii itawasaidia watumishi wa umma kujenga msingi imara wa maisha yao ya kiuchumi baada ya utumishi,” alisema Bw. Ngangaji.

Katika mafunzo hayo, Meneja wa Kanda ya Kati wa PSSSF, Bw. Lulyalya Sayi, ameeleza kuwa Mfuko huo ulianzishwa kwa lengo la kutoa huduma za hifadhi ya jamii kwa watumishi wa umma Tanzania Bara. Hivyo, amesisitiza waajiri na wanachama kutekeleza wajibu wao wa kuwasilisha na kufuatilia michango yao mtawalia.

Kwa upande wake, Afisa Matekelezo Mwandamizi wa PSSSF, Bw. Philipo John, amesema matumizi ya TEHAMA yamerahisisha huduma za Mfuko, ikiwemo usajili, uwasilishaji wa michango na madai, uhakiki wa wastaafu na ulipaji wa mafao kwa njia za kielektroniki, hivyo kuwawezesha wanachama kupata huduma bila kufika ofisini.

Mkurugenzi wa Mipango wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Cosmas Ngangaji,akimwakilisha Katibu Mkuu-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi, katika kuhitimisha mafunzo ya uelewa kuhusu huduma zinazotolewa na PSSSF kwa watumishi wa Ofisi hiyo, yaliyofanyika tarehe 23 Novemba 2026 katika eneo maalumu la Ofisi hiyo, Mtumba jijini Dodoma.

Baadhi ya Wakurugenzi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, walimsikiliza Mkurugenzi wa Mipango wa Ofisi hiyo Bw. Cosmas Ngangaji (hayupo pichani) wakati akihitimisha mafunzo kuhusu huduma zitolewazo na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma leo tarehe 23 Novemba Mtumba Jijini Dodoma Novemba 23, 2026 katika eneo maalumu la Ofisi hiyo Mtumba jijini Dodoma

Baadhi ya Watumishi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakimsikiliza Mwakilishi wa Katibu Mkuu-UTUMISHI, ambaye ni Mkurugenzi wa Mipango wa Ofisi hiyo, Bw. Cosmas Ngangaji wakati akihitimisha mafunzo kuhusu huduma zitolewazo na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma leo tarehe 23 Novemba Mtumba Jijini Dodoma

Baadhi ya Wakurugenzi na Watumishi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, walimsikiliza Afisa Matekelezo Mwandamizi wa PSSSF, Bw. Philipo John, akitoa wasilisho kuhusu matumizi ya TEHAMA yalivyorahisisha utoaji wa huduma za Mfuko huo Novemba 23, 2026 katika eneo maalumu la Ofisi hiyo Mtumba jijini Dodoma

Baadhi ya Wakurugenzi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, walimsikiliza Mkurugenzi wa Mipango wa Ofisi hiyo Bw. Cosmas Ngangaji (hayupo pichani) wakati akihitimisha mafunzo kuhusu huduma zitolewazo na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma leo tarehe 23 Novemba Mtumba Jijini Dodoma Novemba 23, 2026 katika eneo maalumu la Ofisi hiyo Mtumba jijini Dodoma

Baadhi ya Watumishi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakimsikiliza Mwakilishi wa Katibu Mkuu-UTUMISHI, ambaye ni Mkurugenzi wa Mipango wa Ofisi hiyo, Bw. Cosmas Ngangaji wakati akihitimisha mafunzo kuhusu huduma zitolewazo na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma leo tarehe 23 Novemba Mtumba Jijini Dodoma

Meneja wa Kanda ya Kati wa PSSSF, Bw. Lulyalya Sayi akizungumza na Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI kuhusu huduma zitolewazo na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma Novemba 23, 2026 wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji watumishi hao ambayo hufanyika kila jumatatu ya wiki katika eneo maalumu la Ofisi hiyo Mtumba jijini Dodoma

No comments:

Post a Comment